Wakopeshaji wa vifaa vya kilimo na ujenzi (EFTA) ni wahuni?

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,240
4,466
Kuna hii taasisi inaitwa Equity for Tanzania (EFTA) inayodai inakopesha vifaa vya ujenzi imenipa utata.

Dada yangu ni mjasiriliamali wa kutengeneza matofali, nyanda za juu kusini. Hivi karibuni alinishirikisha kwamba anataka kuchukua mkopo wa milioni 30 wa vifaa vya ujenzi kwa hao EFTA tawi la Mbeya, ambapo wanashirikiana na Equity Bank Mbeya mjini. Kitu ambacho kimetushangaza ni kwamba hiyo ofisi inayodaiwa ni ya EFTA Mbeya mjini wanataka 20% ya milioni 30 ilipwe ofisini cash (ati ni pesa ya ofisi) kabla ya mkopo kuwa processed. Cha ajabu ni kwamba hata hizo mashine hawatengenezi wao, bali inabidi uwasiliane na mtengenezaji, ambaye inabidi akupe invoice, ambayo ndiyo itapelekwa benki.

Huhitaji kuwa na akili kubwa sana kujua kuwa huu ni uhuni, lakini najiuliza kama huu uhuni ni wa wafanyakazi wa EFTA tawi la Mbeya au EFTA kwa ujumla?

Inabidi tujuzane ili watu wasije wakalizwa...
 
Dada yangu ni mjasiriliamali wa kutengeneza matofali, nyanda za juu kusini. Hivi karibuni alinishirikisha kwamba anataka kuchukua mkopo wa milioni 30 wa vifaa vya ujenzi kwa hao EFTA. Kitu ambacho kimetushangaza ni kwamba hiyo ofisi inayodaiwa ni ya EFTA Mbeya mjini wanataka 20% ya milioni 30 ilipwe ofisini cash (ati ni pesa ya ofisi) kabla ya mkopo kuwa processed. Cha ajabu ni kwamba hata hizo mashine hawatengenezi wao, bali inabidi uwasiliane na mtengenezaji, ambaye inabidi akupe invoice, ambayo ndiyo itapelekwa benki.

Huhitaji kuwa na akili kubwa sana kujua kuwa huu ni uhuni, lakini najiuliza kama huu uhuni ni wa wafanyakazi wa EFTA tawi la Mbeya au EFTA kwa ujumla?

Mkuu, huu sio utaratibu mzuri wa kutafuta taarifa za mashirika ya kibiashara. Nakushauri:
  • Jirekebishe, wewe una access ya internet na hivyo una nafasi ya kutafta taarifa za namna kampuni hiyo inavyofanyakazi kwenye website yao kabla hujaja kuwaita wahuni humu;
  • Mshauri huyo dada yako aliyeko Nyanda za Juu aende ofisini kwao (EFTA, tawi la Mbeya) akawaulize maofisa wao kama kuna wateja ambao tayari wanafanya nao kazi ili apate ushuhuda wa uhuni unaousema.
Ninavyofahamu ni kwamba; EFTA ni kampuni inayotoa mikopo ya mitambo ya kufanyia kazi (Equipment Financing) kwa wajasiriamali bila kuhitaji dhamana. Unatoa 10% ya mkopo (down payment) kwa mitambo isiyohamishika na 20% kwa mitambo inayohamishika (mobile equipment, e.g: tractor, stone crushers, mining equipment, etc.) ikiwa tayari umeidhinishiwa mkopo na umeshakubaliana bei na Supplier wa hiyo mitambo.

Eng. WFM
 
Taratibu mkuu. Usikurupuke. Nakushangaa sana 'engineer'. Sina uhakika kama kweli wewe ni engineer ambaye ningetegemea uwe na uwezo wa kuchambua mambo.

Engineer kwa hiyo wewe kila kinachoandikwa kwenye internet ndio taarifa sahihi. Au unamaanisha niingie kwenye website yao EFTA ndiko nitapata taarifa sahihi? Mtu ambaye nataka kujua kama ni mkweli, nikamsome alivyojiandika. Au unataka niperuzi page za yahoo, google, facebook ili nipate ukweli wa mtu ambaye sina uhakika naye.

Ni sawa na researcher kutumia Wikipedia kwenye tafiti zake. BTW hapa tunatumia internet na tunapata taarifa, na wewe umetoa taarifa. Hivi huwa waona watu wanaandika review ya huduma au product fulani? Unadhani huwa zinasaidia nini?

Kama wewe ni mwajiriwa au mmiliki au ndugu wa mmiliki wa EFTA njoo utoe taarifa sahihi.
 
Mtoa uzi nafikir kunasehemu haujaelewa au umepata taarifa za hao EFTA kwa mtu mwenye taarifa zisizo kamil. Hakuna utapel wowote mm nilohudhuria semina yao nikiwa nahitaj mashine ya kusaga na kukoboa.

Kwa mkopaji wa mwanzo au mara ya kwanza kuna asilmia ya thaman ya mashne au mtambo unalipia mfano 10% so hyp 90% inayobakia wanalipia wao moja kwa moja kwa muuuzaji. Kumbuka gharama za installation za mtambo ni zako au za muuzaji.
 
Kiukweli mtoa uzi huu kakurupuka kwa kweli na usipokuwa makini utashtakiwa na sijui kama una hata wakukuwekea dhamana. Usiwe unasikiliza watu wanayosema nakukurupuka. Mimi baada yakusoma taarifa hii kwakuwa namfahamu rafiki yangu ambae amekopa huko niliamua kufanya utafiti kidogo.

Nilisearch nikapata website ya EFTA www.efta.co.tz, kwenye website pana contact page ambako wameweka matawi yao, makao makuu yaliyopo Moshi na kila tawi lina namba ya simu.

Niliamua kupiga simu matawi matatu Mwanza, Mbeya na Dar nikpewa maelezo ya taratibu za mkopo zinazofanana, nikamuuliza mshikaji wangu tuliesoma nae anaefanya BOT kujua kama wanaitambua EFTA akanipa majibu baada ya siku tatu kuwa imeandikishwa kihalali BOT na ina vigezo vakutoa mikopo ya mashine tu .

Nikawatembelea EFTA ofisini kwao Dar jengo la IT Plaza posta mpya ghorofa ya 5 nikakutana na Manager anaitwa Victor akanipa taratibu zakukopa na kuwa huwa mikopo yao haina dhamana bali kuna malipo ya awali yanayotolewa na yana kuwa kati ya 10%,20% na 30% hakuna rushwa wala gharama zingine hadi unapata mkopo wako na hzi asilimia ni (commitment fee) na ni sehemu ya ule mkopo.

Haya ndiyo uliyotakiwa kuyafahamu mtoa post kabla ya kuja kutulisha sumu na hata wakikuamulia wakikushtaki kwa kutumia cyber crime law utawalipa fidia hadi uuze na ukoo wenu kwa kuwakashfu bila ushahidi na kwa kutoa taarifa za uongo , sali wasikumbane na hii post wampe mwanasheria wao.

Tuwe makini tutumie fursa ya habari kuwepo mtandaoni kupeana taarifa zenye afya ndugu zangu.

Bahati nzuri kakuta watu wote walioisoma hatukuwa vilaza tunajua kuutafuta ukweli na hatukurupuki.

Information is power!

Kuna hii taasisi inaitwa Equity for Tanzania (EFTA) inayodai inakopesha vifaa vya ujenzi imenipa utata.

Dada yangu ni mjasiriliamali wa kutengeneza matofali, nyanda za juu kusini. Hivi karibuni alinishirikisha kwamba anataka kuchukua mkopo wa milioni 30 wa vifaa vya ujenzi kwa hao EFTA tawi la Mbeya, ambapo wanashirikiana na Equity Bank Mbeya mjini. Kitu ambacho kimetushangaza ni kwamba hiyo ofisi inayodaiwa ni ya EFTA Mbeya mjini wanataka 20% ya milioni 30 ilipwe ofisini cash (ati ni pesa ya ofisi) kabla ya mkopo kuwa processed. Cha ajabu ni kwamba hata hizo mashine hawatengenezi wao, bali inabidi uwasiliane na mtengenezaji, ambaye inabidi akupe invoice, ambayo ndiyo itapelekwa benki.

Huhitaji kuwa na akili kubwa sana kujua kuwa huu ni uhuni, lakini najiuliza kama huu uhuni ni wa wafanyakazi wa EFTA tawi la Mbeya au EFTA kwa ujumla?

Inabidi tujuzane ili watu wasije wakalizwa...
 
Uhuni wa EFTA upo kwenye riba, yani unatoa 10%-20% ya mkopo halafu wao wanatoa 80%-90% lakini riba inakuwa calculate kwa kutumia 100% ya mkopo badala ya kutumia Hiyo 80%-90% waliyotoa wao.
In either case sio ishu kubwa kwa mfanyabiashara, kumbuka riba ni on reducing balance, so kama machine unayotaka ni ya million 30, down payment ya let say million 6 (20%) inakuwa na effect kwenye principal na interest on the very first month
 
sio uhuni ndo masharti ya kula lazma uliwe.yupo jamaa yangu aliomba mkopo wa machinery gari yenye friza tani 2 na nusu.alifanikiwa na alipitia hatua kama ivo na 5 percent ya mkopo alilipa+takrima.it takes slopes&hills to succeed.no paths are so clear
Hata mimi nilikua EFTA jana kufuatilia uwezekano wa kupata gari ya freezer gani 2 na nusu.Jamaa yako ilimkost kiasi gani kupata hiyo gari? Alipata gari ya aina gani?
 
Kiukweli mtoa uzi huu kakurupuka kwa kweli na usipokuwa makini utashtakiwa na sijui kama una hata wakukuwekea dhamana. Usiwe unasikiliza watu wanayosema nakukurupuka. Mimi baada yakusoma taarifa hii kwakuwa namfahamu rafiki yangu ambae amekopa huko niliamua kufanya utafiti kidogo.

Nilisearch nikapata website ya EFTA www.efta.co.tz, kwenye website pana contact page ambako wameweka matawi yao, makao makuu yaliyopo Moshi na kila tawi lina namba ya simu.

Niliamua kupiga simu matawi matatu Mwanza, Mbeya na Dar nikpewa maelezo ya taratibu za mkopo zinazofanana, nikamuuliza mshikaji wangu tuliesoma nae anaefanya BOT kujua kama wanaitambua EFTA akanipa majibu baada ya siku tatu kuwa imeandikishwa kihalali BOT na ina vigezo vakutoa mikopo ya mashine tu .

Nikawatembelea EFTA ofisini kwao Dar jengo la IT Plaza posta mpya ghorofa ya 5 nikakutana na Manager anaitwa Victor akanipa taratibu zakukopa na kuwa huwa mikopo yao haina dhamana bali kuna malipo ya awali yanayotolewa na yana kuwa kati ya 10%,20% na 30% hakuna rushwa wala gharama zingine hadi unapata mkopo wako na hzi asilimia ni (commitment fee) na ni sehemu ya ule mkopo.

Haya ndiyo uliyotakiwa kuyafahamu mtoa post kabla ya kuja kutulisha sumu na hata wakikuamulia wakikushtaki kwa kutumia cyber crime law utawalipa fidia hadi uuze na ukoo wenu kwa kuwakashfu bila ushahidi na kwa kutoa taarifa za uongo , sali wasikumbane na hii post wampe mwanasheria wao.

Tuwe makini tutumie fursa ya habari kuwepo mtandaoni kupeana taarifa zenye afya ndugu zangu.

Bahati nzuri kakuta watu wote walioisoma hatukuwa vilaza tunajua kuutafuta ukweli na hatukurupuki.

Information is power!
ASANTE SANA KWA KUTUPA UELEWA ULIOSHIBA, UBALIKIWE
 
Mleta mada kwanini unakuwa mpumbavu?

Mimi nimeshiriki kwenye hiyo biashara!

Ni ajabu mteja kuambiwa aweke amana kwenye mkopo wake?
Pia unashangaa eti kwanini wao EFTA hawatengenezi hizo mashine bali unatakiwa kwenda dukani kuchukua invoice, sasa cha ajabu nini hapo? EFTA wana legal binding agreements na maduka wanakokuelekeza, ndio maana unapewa warranty ya ubora na maintenance where required!

Wabongo tuna changamoto nyingi sana, ndio maana biashara zinafeli!
 
In either case sio ishu kubwa kwa mfanyabiashara, kumbuka riba ni on reducing balance, so kama machine unayotaka ni ya million 30, down payment ya let say million 6 (20%) inakuwa na effect kwenye principal na interest on the very first month
Hii haina tofauti na unaenda kwa Mganga akupe Utajiri nae anakuambia utoe hela umpe yeye,
 
Hata mimi nilikua EFTA jana kufuatilia uwezekano wa kupata gari ya freezer gani 2 na nusu.Jamaa yako ilimkost kiasi gani kupata hiyo gari? Alipata gari ya aina gani?
Samahan mkuu, hayo magari ni kwa ajili ya nini?
 
Kiukweli mtoa uzi huu kakurupuka kwa kweli na usipokuwa makini utashtakiwa na sijui kama una hata wakukuwekea dhamana. Usiwe unasikiliza watu wanayosema nakukurupuka. Mimi baada yakusoma taarifa hii kwakuwa namfahamu rafiki yangu ambae amekopa huko niliamua kufanya utafiti kidogo.

Nilisearch nikapata website ya EFTA www.efta.co.tz, kwenye website pana contact page ambako wameweka matawi yao, makao makuu yaliyopo Moshi na kila tawi lina namba ya simu.

Niliamua kupiga simu matawi matatu Mwanza, Mbeya na Dar nikpewa maelezo ya taratibu za mkopo zinazofanana, nikamuuliza mshikaji wangu tuliesoma nae anaefanya BOT kujua kama wanaitambua EFTA akanipa majibu baada ya siku tatu kuwa imeandikishwa kihalali BOT na ina vigezo vakutoa mikopo ya mashine tu .

Nikawatembelea EFTA ofisini kwao Dar jengo la IT Plaza posta mpya ghorofa ya 5 nikakutana na Manager anaitwa Victor akanipa taratibu zakukopa na kuwa huwa mikopo yao haina dhamana bali kuna malipo ya awali yanayotolewa na yana kuwa kati ya 10%,20% na 30% hakuna rushwa wala gharama zingine hadi unapata mkopo wako na hzi asilimia ni (commitment fee) na ni sehemu ya ule mkopo.

Haya ndiyo uliyotakiwa kuyafahamu mtoa post kabla ya kuja kutulisha sumu na hata wakikuamulia wakikushtaki kwa kutumia cyber crime law utawalipa fidia hadi uuze na ukoo wenu kwa kuwakashfu bila ushahidi na kwa kutoa taarifa za uongo , sali wasikumbane na hii post wampe mwanasheria wao.

Tuwe makini tutumie fursa ya habari kuwepo mtandaoni kupeana taarifa zenye afya ndugu zangu.

Bahati nzuri kakuta watu wote walioisoma hatukuwa vilaza tunajua kuutafuta ukweli na hatukurupuki.

Information is power!
Acha mkwara, mtoa mada anahitaji taarifa kutokwa kwa wanufaika na sio watoaji, kwani mara ngapi makampuni makubwa yamekuwa yakiwaibia wateja wake ? Taarifa ambazo ni negative hawawezi kuziweka maana zitawaangusha kibiashara thats why muda mwingine maoni ya mnufaika yanahitajika tujue ukweli wa pande zote, mtoa mada wasikupige mkwara kama kuna madudu umeyagundua yaanike hii ndio JF ili mradi ziwe taarifa za kweli hata wakiliamsha tuweze kukutetea huko mahakamani
 
Back
Top Bottom