Wakina Tundu Lissu na TLS yao waonywa Kuhusu Mgomo, wajiandae kujibu Mashitaka

Hivi hata kama hilo tukio wamelifanya polisi, hivi hawana akili kabisa waende wamevalia sare zao!???!

Hii TLS ilikosea sana kuchagua MTU ambaye yupo kwenye active politics! Anabwatuka tu akidhani yupo jukwaani.

Sent from Moto G
Unastaajabu nn!?mbna hushangai tukio Kama hili hadi Leo kweli!? walinzi hawajakamatwa hadi tunawaeleza waandish watusaidie kweli!? are we seriously..........!??????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati rais aliposimama kuhutubia siku ya sheria alitahadharisha chama cha wanasheria kumchagua mwanasiasa na angalizo lake lilihusu chama hicho kupoteza maana nzima na kuwa cha kisiasa wengi walikuwa na mtazamo tofauti na kujazwa chuki hatimae kura zilimuangukia mwanasiasa

hivi sasa TLS imekuwa ikipambana na rais na serikali kwa kutoa matamko yasiozingatia weledi na kusahau majukumu yake ya kisheria na kujaa siasa,

mfano mzuri ni kama huu wa kuwaambia mawakili wasiende kwenye kesi kwa siku mbili,bila ya sababu za msingi kisa tu rais wa wanasheria ni mwanasiasa na anapambana na utawala wa nchi

Tunashukuru rais kwa kuliona hilo mapema na watu wangetumia busara wala uhuni wa matamko tusingeusikia!
 
Hivi hata kama hilo tukio wamelifanya polisi, hivi hawana akili kabisa waende wamevalia sare zao!???!

Hii TLS ilikosea sana kuchagua MTU ambaye yupo kwenye active politics! Anabwatuka tu akidhani yupo jukwaani.

Sent from Moto G
Kelele wewe mchumia tumbo Na Nyinyiem yako Fyoko Fyoko Kama we una akili prove hapa kwenye uzi watu wakujue we mwanaume Lissu ameshindwa kesi ngapi Dhid ya serikali? alafu ujue nan amebwatuka na nani ame prove felia kilaza mkubwa wewe. Rud Bush Brother mji unahitaji waliosoma hiki sio kipind cha umande.
 
Hivi kwa mfano Hospital binafsi mojawapo ikilipuliwa na bomu, chama cha madaktari kitatoa tamko madaktari wagome? Au benki mojawapo ikilipuliwa bankers watagoma nao?
 
yaa
Kitendo cha tukio hilo kuwa na harufu ya mkono Wa Serikali kile kinachosemekana kuwa wanafanya uchunguzi ni hadaa kwa Watanzania itapotra kama yalivyopotea matukio mengine kama LA kutekwa kwa Loma
yaani uandishi wako tu unaakisi upeo wako. unaposema uchunguzi ni hadaa... vp yale mliyoambiwa na kina Lissu kwamba serikali inahusika yamethibishwa wapi na nani?
 
Hivi hata kama hilo tukio wamelifanya polisi, hivi hawana akili kabisa waende wamevalia sare zao!???!

Hii TLS ilikosea sana kuchagua MTU ambaye yupo kwenye active politics! Anabwatuka tu akidhani yupo jukwaani.

Sent from Moto G

Mimi nadhani hata wewe kidogo utakuwa huna akili za kutafakari mambo......

Tundu Lissu kwa tuliomsikiliza na kusoma tamko la mawakili, hakuna sehemu wamesema kuwa kuwa polisi ndiyo walioenda kulipua ofisi za mawakili hao...

Kilichosemwa ni "........watu waliovalia sare za askari polisi.... "

Sasa kwa statement hii haina maana kuwa hao watu lazima wawe polisi kwelikweli kwa sbb mtu yeyote anaweza kwenda kufanya uhalifu kwa fake forged identity......

Sare za polisi zinavaliwa sana na watu hata wasiokuwa polisi kwa kuigizia, kufanya uhalifu nk...
 
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini, wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi, vinavyochunguza tukio la mlipuko, uliotokea kwenye ofi si za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Profesa Juma alisema TLS hawana haki ya kutoa agizo kwa mawakili, kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza mengine, kwa kuwa kila wakili ana mkataba binafsi na mteja wake.

Profesa Juma alisema uhuru wa mahakama ni pamoja na kuheshimu mamlaka nyingine za nchi zinapokuwa zinafanya kazi zake. Alisema kwa kuwa tukio la kulipuliwa kwa ofisi za Mawakili wa Immma ni tukio la kihalifu, hivyo wanasheria waiache Polisi na vyombo vingine vya upelelezi kufanya kazi yao.

“Kama kutatokea wateja watakaolalamika kuwa mawakili wao hawakufika mahakamani siku ya Jumanne na Jumatano, hatua za kisheria dhidi ya mawakili hao zitachukuliwa ikiwemo kuwapeleka kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili,” alieleza Kaimu Jaji Mkuu.

Kauli ya Jeshi la Polisi Kwa upande wao, Jeshi la Polisi limesema liachwe liendelee na kazi ya uchunguzi, badala ya kulihusisha na tukio hilo. Msemaji wa Jeshi hilo Makao Makuu, Kamishina Msaidizi Barnabas Mwakalukwa alisema Jeshi la Polisi ndicho chombo chenye mamlaka ya kufanya uchunguzi na hivyo kama kuna mtu yeyote mwenye taarifa yoyote kuhusu tukio hilo, anatakiwa kuzitoa polisi badala ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Kauli hizo za Polisi na ya Kaimu Jaji Mkuu, zimekuja baada ya Rais wa TLS, Tundu Lissu kuwaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa Baraza lao la Uongozi lina taarifa kuwa kikundi cha watu wenye silaha za moto, wakiwa wamevalia sare za Jeshi la Polisi, kiliwateka nyara walinzi binafsi wa Kampuni ya IMMMA na kuingia ndani ya eneo la ofisi hizo.

Lissu alidai watu hao baada ya kuingia ndani, walitega milipuko na madumu manne ya mafuta ya petroli katika maeneo kadhaa ya jengo la ofisi hizo. Alidai muda mfupi baadaye, milipuko hiyo ililipuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa jengo la ofisi za IMMMA Advocates zilizoko Upanga pamoja na majengo jirani.

“Kama Lissu ana hizo taarifa alitakiwa azilete polisi kwa kuwa ndicho chombo cha uchunguzi badala ya kuzungumza na vyombo vya habari. Kazi ya polisi ni kufanya uchunguzi wa kina na ndiyo maana Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu alisema atatoa taarifa uchunguzi ukikamilika, hivyo watu wanapaswa kusubiri taarifa kamili, nje ya hapo tunakuwa tunafanya kazi nje ya utawala wa sheria,” alieleza Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mwakalukwa.

Mwakalukwa alivitaka vyombo vya habari, kuwatafuta walinzi hao ambao Lissu alidai walitekwa na watu wanaodhaniwa kuwa polisi ili waeleze tukio lilivyokuwa na ikibidi walinzi hao kutoa taarifa za kutekwa kwao polisi.

Alisema jambo hilo siyo dogo, hivyo watu waviache vyombo vya uchunguzi, viendelee na kazi yake kwani uchunguzi pekee ndiyo utakaobaini chanzo na wahusika. Ili kuonesha mshikamano, Baraza la Uongozi la TLS limewataka mawakili wote ambao ni wanachama wao nchini, wasuse kuhudhuria mahakamani na kwenye mabaraza ya aina zote kwa siku mbili, kesho na keshokutwa.

Lissu alidai kuwa lengo la kususa huko ni kupeleka ujumbe kwa jamii kuwa tukio lililotokea kwenye ofisi za IMMMA siyo dogo na hivyo wananchi ambao ni wateja wao hawana budi kwa siku hizo mbili kuungana nao kupinga jambo hilo. Alisema watamwandikia Kaimu Jaji Mkuu barua ya kumfahamisha kusudio lao la kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza yote kwa siku hizo mbili.

“Tunatambua kuwa wateja wetu wataathirika, na hiyo ndiyo maana ya kufikisha ujumbe wetu kwa jamii. Tunafahamu kuwa wajibu wa kwanza wa wakili ni kumwakilisha mteja wake mahakamani, lakini kama mawakili hawako salama, uwezo wa kuwawakilisha wateja wao mahakamani unakuwa haupo,” alieleza Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema.

Aidha, alililaani tukio hilo na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama, kuchunguza kwa kina ili wahusika wajulikane na kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi yao. Alisema mawakili wa IMMMA wanapaswa kupatiwa ulinzi dhidi ya vitisho au vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wao au kuwazuia kutekeleza wajibu wao wa kitaaluma.

Kwa mujibu wa Lissu, Baraza la Uongozi la TLS litakutana na uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Kaimu Jaji Mkuu, Waziri wa Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuzungumzia vitendo vya kushambuliwa mawikili wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kisheria.

Naye Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Omar Shaaban alisema wanaungana na TLS kulaani shambulio hilo kwenye ofisi za IMMMA. Alisema IMMMA wana tawi lao Zanzibar na ndiyo maana aliamua kuungana na TLS kulaani tukio hilo.

Usiku wa kuamkia juzi kulitokea milipuko kwenye ofisi za IMMMA Advocates zilizopo Upanga katika Barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam na kusababisha uharibifu. Imeelezwa kuwa vyombo vya uchunguzi vinaendelea na uchunguzi kubaini chanzo na wahusika wa tukio hilo.

Chanzo: Habari leo
huyo kaimu jaji hajielewi hafai kukaa kwenye nafasi hiyo afutiwe uwanachama na wanasheria kama walivyofanya madaktari walimfuta Dr Mtasiwa baada ya kuona ana wapuuza
 
Usitarajie kauli ya Mtu ikakubaliwa na jamii yote. Kupinga au kukubali ni hiyari ya raia aliye kwenye nchi huru kama Tz. Kuna somo hapa tunaweza kulipata. Kama ukishangaa kupingwa kwa Tundulisu basi mawazo yako yalitaraji atakubaliwa na wenzake wote. Si ktk ubinaadamu huo.
Hata kwenye kupiga kura hakupigiwa na wote ina wezekana huyo Tungaraza Ali vote no kwa Lisu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mtaalamu wa jinai ninashawishika sana kusema ni tukio la kuunda na lawama zangu naelekeza kwa IMMA ADVOCATES & LISSU lengo lao ni kupata coverage kwa nchi za magharibi kwamba Tanzania haikaliki na hakuna rule of law.

IMMA wametumika hapa sababu wanajua mteja wao ACCACIA lazima ata sympathise nao kuwa wanaonewa sbb ya case yao.

Jamani hii ni nchi yetu sote nguvu kubwa mnazotumia kuibomoa mkae mkijua hata nyie mkiingia mlowatoa watatumia mbinu hizohizo kuwatoa. Mtatawala nini na kwa maslahi ya nani?

Hivi kweli polisi wenye uniform wakatekeleze uhalifu wa aina hii kweli inaingia akilini?

Tambua polisi ndio wataalamu wa kuandaa matukio ya kihalifu kutokana na taaluma yao iweje wajikamatishe kijinga ivi.

Liheshimuni jeshi hili kwani uwepo wake ndoo umekufanya uitishe hyo press conference kwa kujiamini.

Nyambafuuu....!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni tukio la kuundwa unasubiri nini kupeleka ushahidi polisi ili wawakamate waliojiundia tukio hilo???
 
Back
Top Bottom