Wakili kesi ya uporaji wa gari ya Paul Makonda ajitoa

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Tuna siasa za kupakana matope sana, waliosema wana ushahidi wa maovu ya Makonda wanakimbia balaa wakisikia Makonda anapita

Hata Sabaya amewashinda kesi zote, sasa wameumbuka na uongo wao wamebaki kuhonga mahakimu tu lakini ushahidi hawana.!
---

Wakili wa kujitegemea, Wabeya Kung'e anayemwakilisha Patrick Kamwelwe amejiondoa katika kesi ya tuhuma za uporaji wa gari aina ya Range Rover inayomkabili aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda, akidai kutopewa kuwa hajapewa taarifa sahihi ya mteja wake.

Mbali na Makonda, mshitakiwa mwingine ni mmiliki wa blogu ya Lemutuz, William Malecela, ambapo mfanyabiashara Kamwelwe anadai alipwe fidia ya zaidi ya Sh240 milioni ambazo ni gharama za kodi thamani ya gari hilo la kifahari.

Pia wakili Kung'e amejiondoa kwenye kesi ndogo namba 160 ya mwaka 2022 na 179 ya mwaka 2022 ambapo Makonda na mwenzake William Malecela wamepeleka maombi madogo katika mahakama hiyo, wakidai kuwa shaka na uraia wa Kamwelwe.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Richard Kabate jana Desemba 8, Wakili Kung'e ameiomba mahakama hiyo ajitoe kumwakilisha Kamwelwe kwenye kesi ya msingi na maombi madogo yaliyowasilishwa kwa kuwa hajapewa maelezo sahihi na mteja wake.

Kung'e amedai Novemba 11, 2022 alipewa siku 14 na mahakama hiyo kuwasilisha kiapo kinzani baada ya Makonda na Lemutuz kupeleka maombi madogo ya kuwa na mashaka na uraia wa Kamwelwe lakini ameshindwa kuwasilisha kutokana alikosa ushirikiano kutoka kwa mteja wake.

"Nimeshindwa kuwasilisha kiapo kinzani kama mahakama ilivyonitaka kwa sababu nimekosa ushirikiano na nimejaribu kufanya mawasiliano na mteja wangu lakini sipati majibu kutokana na mazingira hayo naomba kujitoa kwenye kesi ya msingi na maombi madogo," amedai Kung'e.

Kwa upande wake Wakili wa kujitegemea anayemwakilisha Makonda, Gift Joshua amesema kuwa wamepeleka maombi baada ya kuwa na mashaka ya uraia wa mfanyabiashara huyo na kutokuwa na mali zisizohamishika nchini, ambapo mleta maombi huyo anatakiwa kutoa gharama za uendeshaji wa kesi ambayo ni kwa mujibu wa sheria.

"Kwa mtu ambaye siyo raia anakuwa hana mali ndani ya nchi, lakini mtu akiwa raia wa Tanzania lazima atakuwa na mali endapo tutakwenda kudai gharama za uendeshaji wa kesi ataweza kutulipa au kama anayo mali atauza na kutulipa," alidai Joshua.

Joshua amedai hawana pingamizi kwa kujitoa wakili huyo kwenye kesi ya msingi na maombi madogo kwa kuzingatia mtoa maombi ana wajibu wa kuwakilishwa wameiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ili aweze kutafuta wakili mwingine.

Akijibu maombi hayo, Hakimu Kabate amemkubalia Kung’e kujiondoa na kwamba maombi madogo yatasikilizwa upande mmoja kwa sababu wakili anayemwakilisha Kamwelwe ameshindwa kuleta kiapo kinzani hivyo amekiuka mahakama hiyo

Kabate ameahirisha shauri hilo hadi Januari 31, 2023 na itaposikilizwa upande mmoja.

Katika kesi ya msingi Kamwelwe anadai kuwa yeye na Lemutuz ni marafiki alitumia urafiki wake kumkabidhi Makonda gari aina ya Range.
 
Mbona sijaona mahali Chadema wakipagawa. Halafu kesi hii inahusu vipi chadema? Au huyu kamwelwe ni chadema?
 
Haujui wewe figisu za mawakili ,sasa nakuambia Le Mutuz Boma Ye Nye nye nye na Makonda wamemnunua huyo wakili wa PK ndio maana kajitoa...Haya mambo yapo sana!
 
Back
Top Bottom