Wakati Wananchi Wakilia Upigaji , Serikali Yatenga Mabilioni Kununua Magari ya Ma RC na Ma DC

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,779
50,562
Hii ndio Hali inayoendelea Kwa Sasa ,Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.

Nchi Ina Vipaombele vya hovyo sana hii.

---

Waziri wa TAMISEMi, Angellah Jasmine Kairuki amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 leo April 14,2023 ambapo amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, TAMISEMI imetengewa Tsh. Bilioni 16.58 kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa “Kati ya magari hayo, magari 5 ni ya Wakuu wa Mikoa, magari 2 ni ya Makatibu Tawala wa Mikoa na magari 74 ni ya Wakuu wa Wilaya”

Waziri Kairuki pia amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, Ofisi ya Rais - TAMISEMI imetengewa Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa boti 4 katika Halmashauri za Wilaya za Ludewa, Buchosa, Nyasa na Sumbawanga ili kuimarisha doria, ulinzi na ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri hizo.

“Hadi Februari, 2023, Tume imepokea Shilingi Bilioni 7.83. Majukumu yaliyotekelezwa ni pamoja na kusajili walimu 9,800, kupandishwa vyeo walimu 1,003, Walimu 3,347 wamethibitishwa kazini na Walimu 3,388 wamebadilishiwa vyeo”

“Kuhuisha TANGE za walimu kwenye Wilaya zote 139, vikao 300 vya mashauri ya nidhamu kwa walimu vya kisheria vimefanyika, Mashauri 273 ya nidhamu ya walimu yamefanyiwa uchunguzi na kuwasilishwa kwenye Kamati za Wilaya kwa ajili ya kutolewa uamuzi”
 
Nchi masikini na watu wake masikini lakina viongozi wetu hawaumii Wala hawasumbuki na umasikini wa watanzania ndio maana wanafuja fedha.

Unawezaje kutenga 16Billioni kwa ununuzi wa magari ya gharama kubwa wakati zipo gari za Bei ya chini na Zina mudu safari!!!!!

Jamani viongozi wetu kuweni na huruma japo kidogo, mnapo panga mipango ya matumizi Serikalini jaribuni kubana matumizi kadiri iwezekanavyo maana nchi yetu bado ni masikini bado tunategemea misaada zaidi tuache ufahari usio wa lazima.
 
Hapo kwenye bajeti ya boti za Doria 1.5billion kwa boti 4, kila boti ni 375million. Zitatengenezwa za bajeti ya 250m au pungufu 125m inawekwa mfukoni
Huko 250 mbali hapo wananunua engine m13 na body la fiber kama m20 so mchakato wote ni kama 40 m kwa boti moja zingine zinawekwa kibindoni.

Nilishawahi kuiona moja ya Rubondo island n huzun kwakweli
 
Nchi masikini na watu wake masikini lakina viongozi wetu hawaumii Wala hawasumbuki na umasikini wa watanzania ndio maana wanafuja fedha.

Unawezaje kutenga 16Billioni kwa ununuzi wa magari ya gharama kubwa wakati zipo gari za Bei ya chini na Zina mudu safari!!!!!

Jamani viongozi wetu kuweni na huruma japo kidogo, mnapo panga mipango ya matumizi Serikalini jaribuni kubana matumizi kadiri iwezekanavyo maana nchi yetu bado ni masikini bado tunategemea misaada zaidi tuache ufahari usio wa lazima.
Nchi na Serikali isiyojitambua. Unadhani hata ule msiba wa malkia ingekuwa Tanzania, kuna Rais ambaye angepandishwa kwenye basi. Zingenunuliwa hata V8 400, ili kila Rais apande gari pekee yake, na jingine la eskoti yake.

Ujinga na upumbavu ni mzigo mzito sana kuliko mizigo yote hapa Duniani.
 
Back
Top Bottom