Wakati wa kupiga kura nini huwa unazingatia?

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Wana JF
Hebu tujiulize,wakati unavyokwenda kupiga kura ni vitu gani unavizingatia ili uweze kumchagua raisi ama mbunge wako?

1.je unazingatia vyama vilivyoshiriki ktk uchaguzi husika?
2.je unazingatia sera ya chama?
3.ama unazingatia mtu aliyegombea nafasi husika?
 
Nafuatilia mjadala BBC,ni kweli swala la kuzingatia sera bado hawajalielewa.

Nimekumbushwa yapasa kujenga ufahamu wa watu juu ya hili.
 
Mwanzo nilikuwa naangalia sera ila kwa sasa nakuwa against chama tawala maana kimeishiwa sera na baada ya kukiangusha narudi kwenye sera
 
Nafuatilia mjadala BBC,ni kweli swala la kuzingatia sera bado hawajalielewa.

Nimekumbushwa yapasa kujenga ufahamu wa watu juu ya hili.

Ni kweli kwa upande wa vijijini bado ni issue kubwa sana,kwani wapigakura waliowengi maeneo hayo bado hupiga kura kwa kulipa fadhira ya kile walichopewa

lakini swala la sera kimsingi halipo na hili hata mijini,unaweza kuwa na sera nzuri lakini bado watu wakapiga kura kwa lengo la kumwondoa mlengwa ambae labda hakufanya vyema ktk kipindi kilichopita cha uongozi wake
 
Mwanzo nilikuwa naangalia sera ila kwa sasa nakuwa against chama tawala maana kimeishiwa sera na baada ya kukiangusha narudi kwenye sera

utaangalia kwa nafasi ya uraisi peke yake ama ni hata ktk nafasi za ubunge?

kingine nadhani waliowengi huenda kupiga kura kwa kulipa fadhira ya pesa walizopewa ama pombe walizo nunuliwa,sasa usiwe ni mmoja wao
 
mi huwa naangalia chadema iko wapi, naweka tick. 2010 nilisafiri kwenda kuchagua bila kusikia wala kumwona mbunge wala diwani
 
mi huwa naangalia chadema iko wapi, naweka tick. 2010 nilisafiri kwenda kuchagua bila kusikia wala kumwona mbunge wala diwani

hata mimi diwani sikuwa namjua wala hata jina sikuwahi lisikia,niliweka full suti,niliangalia wapi iko chadema nikaanza kushuka na tiki....lengo ni kumuondoa nduli sisiemu kwanza alafu sera itazingatiwa baadae !!
 
First priority ya wengi kwa sasa ni kuiondoa CCM then sera zinafuata baadae iwe vijijini au mjini.
 
Back
Top Bottom