Wakati mwingine kukataa ujauzito au mtoto inatokeaga tu na sio kwa kupenda

Wamamba

Senior Member
Jan 5, 2024
125
226
Habari zenu wakuu

Nianze moja kwa moja nisiwapotezee mda

Mwaka juzi mwishoni nilirudi mtaani nilipokuwa naishi baada ya kusafiri na kukaa miaka 5 , nilifurahi kukutana na ndugu na marafiki kwa siku nyingi

Katika mizunguuko nikakutana na kasichana kazur nacho nilikuwa nakajuaga zamani tukaelewana tukawa tunatoka na nilimuuliza kama hayupo kwenye mahusiano na alinithibitishia kuwa yupo singo nikaanza naye mahusiano

Baada ya miezi miwili, nikapokea simu ya jamaa akiniulizia huyo msichana na kunambia kuwa kama yupo kwangu au laah , baada ya kuongea akanambia kuwa ni mtu wake wa miaka mingi sana na amegombana naye kwa kukuta chat zangu kwenye simu ya huyo msichana na amenuna na kuondoka na hajui ameenda wapi?

Tulizungumza kama wanaume tukamalizana

Baada ya wiki kale kasichana kakanipigia na kuniomba msamaha kwa yaliyotokea, nikamkubalia ila nilihoji why ukunambia kama upo kwenye mahusiano akajing’ata ng’ata yakaisha ila nikamwambia kuwa aendelee na mtu wake mie nitakuwa namega kisela akakubali; kisichana ni kizuri sanaa aisee

Kwenye tendo nilikuwa nazingatia sana kinga

Nikapata safar na nikasafir sikumuaga, akawa ananipigiaga kawaida anipati kuna siku akaniulizia akaambiwa nimesafiri, akanitafuta whatsapp akanipata akaniuliza why nimesafiri bila ya kumuaga nikamplease yakaisha

Tukawa hatuna stori wala nn

Baada ya miezi mitano akanitafuta akanambia kuwa ana mimba yangu, nikakubali kwa mashart kuwa nikirudi nitakuja kuchek DNA mtoto akizaliwa ila nikamuomba ajitahidi ajihudumie kulea ujauzito sababu kuna ugumu wa kutuma pesa nilipo ila nikirudi nitampa pesa kama fidia- mtego

Tukawa tunaukaribu wa kuchat na kupigiana simu sababu ya ujauzito, baada ya mwezi akanitumia sms kuwa ujauzito sio wangu na akanambia ni wa yule jamaa aliyenipigia sim kuwa yeye ni msichana wake ila jamaa alikataa mimba tangu ina mwezi mmoja - nikakubali bila ya kulalamika na nikampa polee

Sasa hivi amejifungua mtoto ana mwezi mmoja ananipigia simu na sms na kuwapa namba yangu ndugu zake wanibembeleze kuwa mtoto ni wangu, mimi sijajibu sms hata moja ila simu nilipokea na kumwambia kuwa hivi Karibuni nitarudi tutakuja kupima DNA ila mtoto asipokuwa wangu atanilipa fidia

Yule mwanaume wake alikataa ujauzito mbele ya kikao cha familia mbili, waliekaga kikao jamaa akaenda kumtia haibu huyu msichana mbele ya umati wa watu.


Akili ikipoa ntawaretea mrejesho kutoka jela, nilileta uzi hapa kuwa jumanne naenda kumuangalia rafiki yangu jela nijiandae na nini?

Jela nilikuta watanzania wawili na nikaandikisha kuwavisit wote wawili mmoja ana kisa kama hicho hapo juu ndio kilichompeleka jela huyo mwingine ndio ile inshu ya kulawiti mtoto.

Kumruku
 
Mimi kwa maoni yangu kusema ukweli mimi naona ukweli usemwe tu maana naona naweza nikaongea na katika hatua hii ndugu zangu nafikiri na naona kabisa kuwa kwa muda huu naona na natamani niongee kuhusu haya na nina mengi ya kusema moyoni lakini kuhusu hili acha nichangie hoja kwa kusema ni kweli mnayosema na mimi sina la kusema😁
 
Mimi kwa maoni yangu kusema ukweli mimi naona ukweli usemwe tu maana naona naweza nikaongea na katika hatua hii ndugu zangu nafikiri na naona kabisa kuwa kwa muda huu naona na natamani niongee kuhusu haya na nina mengi ya kusema moyoni lakini kuhusu hili acha nichangie hoja kwa kusema ni kweli mnayosema na mimi sina la kusema

mpmbv wew
 
Back
Top Bottom