Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,957
- 20,497
Source: RwandAir- Ndege hiyo mpya ikiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali.
Shirika la ndege la Rwanda Rwandair Ijumaa ilopita ilipokea ndege ingine mpya kubwa ya Airbus A330-200 kutoka Ufaransa.
Ndege hiyo itakuwa ikisafiri masafa marefu kwenda barani Ulaya na Mashariki ya Kati.
Lakini ni nini siri ya mafanikio ya shirika hili la ndege ambalo serikali ya Rwanda inamiliki kwa asilimia 100?
Baada ya nchi kutulia kutoka katika vita ya wenyewe kwa wenyewe serikali ya Rwanda iliketi na kubuni mipango mingi ya kuiendeleza nchi.
Moja ya mipango hii ilikuwa ni kulifufua shirika la ndege la Rwanda liloitwa wakti huo Rwandair Express kwa kusimamia uendeshaji wake ni pia kubadili jina ili shirika liende na wakti na liwe lajulikana kimataifa zaidi. Hapo ndipo lilipozaliwa Rwandair na baadae mwaka 2016 ikapata kibali cha kimataifa kijulikanacho kama ISAGO.
Ukiwa na kibali cha ISAGO shirika la ndege laweza kufanya shughuli zote za uendeshaji katika viwanja vya kimataifa pamoja na kulaza ndege ikisubiri kuruka kwenda sehemu zingine. Pia waweza kuwa na wafanyakazi katika uwanja wa kigeni ambao watafanya shughuli kama cha kuhakiki checki-ns na mengine.
Rwanda kabla ya mwaka 2011 ilikuwa ikitumia ndege za kukodi au kununua ndege ambazo zilikuwa zimetumika lakini zilizokidhi viwango vya kimataifa, pamoja na ndegemoja tu ya aina ya Boeing 737-500. Hivyo mwaka huo Rwanda ikanunua ndege mpya ingine moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji yaani Boeng na ndege ya aina ya 737-800.
Hii ndege ya 737 -800 ilikuwa ni ndege pekee barani Afrika kwa ubora na uimara na baadae mwaka huohuo wa 2011 inanunua ndege ingine ya aina hiyohiyo ya 737-800 New generation, ikifuatiwa na ndege zingine mbili ndogo za aina ya CRJ-900NGs.
Hizi ndege mbili ndogo zilikuwa ni za kushika nafasi ya ndege za zamani aina ya CRJ200 ambazo ziliuzwa na Rwandair kupata fedha zaidi za kujiendesha, waona akili hiyo?
Tokea mwaka 2015 Rwandair ilipopata kibali cha IATA na kuwa mwanachama hai walianza kurusha ndege kwenda China na kupata pia kibali cha ukaazi wa kudumu nchini Beninambapo Ndegeza Rwandair zinaweza kuegeshwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cotonou bila shida na kufanyiwa matengenezo pale na ukarabati wa hapa na pale.
Mwaka juzi yaani 2020 shirika la ndege la Qatar limenunua hisa zaidi ya asilimia 60 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Busegera hali inoruhusu Qatar Airways kuwa na base katika uwanja huo na pia kuegesha ndege zake zinoruka sehemu mbalimbali. Pia Qatar Airways wapo wazungumza na serikali ya Rwanda ili kununua hisa ya asilimia 49 katika Rwandair hivyo kuboresha masuala katika ufanisi wa shughuli zake na mafunzo kwa wahudumu wa ndege na kadhalika, nadhani waona hii hapa?
Pia Rwandair lina ubia na kampuni moja ya kimarekani ambayo inaruhusu mteja kununua tiketi ambayo itamruhusu abiria huyo kusafiri katika tarehe ambayo ataichagua yeye. Hii yafanya tiketi kuuzwa kwa bei nzuri na pia kuwapa abiria uhuru wa kusafiri siku yoyote wanoitaka bila shida.
Kuna umoja wa ndege wa Kenya Airways, Ethiopia Airlines na Qatar Airways (wafadhili) ambao waitwa Oneworld ambapo mashirika haya husaidiana katika masuala mengi tu liliwemo kuwahudumia abiria wa kimataifa ambao husafiri mara kwa mara.
Mwisho ni bodi ya wakurugenzi ya Rwandair ambayo inaunda wataalam na washauri mbalimbali. Hawa kazi yao kubwa ni kuhakikisha utawala wa Rwandair wafuata mwongozo au "framework" kuhakikisha shirika laendeshwa kwa ufanisi unoleta faida khasa kwa wanahisa na kuhakikisha zatafutwa njia zaidi za uboreshaji wa biashara.
Hivi ndivyo shirika la ndege la Rwandair linavyofanya kazi yake kwa ufanisi wa hali ya juu na hadi leo hakuna ndege yoyote iloegeshwa pale BIA wala kelele za ooh zimenunuliwa ndege mbovu.
Shirika letu la ndege la ATCL lina mengi ya kujifunza kutoka kwa jirani zetu Rwanda na namna wanavyohakikisha rasilimali kama shirika la ndege zinatunzwa na kuenziwa kuwa moja ya vyanzo vya mapato ya taifa, ukuzaji utalii na mengine.
Reference: Rwandair, Aviation week, Travel week, flightglobal and wikipedia.