Wajasiriamali changamkieni tenda

MUNYAMAKWA

Member
Jun 15, 2012
59
5
Nimetembelea Mikoa hasa Wilaya zinazozalisha mpunga kwa wingi hapa nchini nikagundua kuna haja kubwa ya kutumia na kuziendeleza fursa ambazo hazijatumika ipafasavyo katika baadhi ya Wilaya hizi ikiwemo KILOMBERO .Mfano ,hatujaweza kugundua namna ya kubadali pumba za mpunga na kuziweka katika bidhaa nyingine kama vile chanzo mbadala cha nishati,malisho ya mifugo n.k.Kwa kufanya hivi tutakuwa tunaongeza vipato na kupunguza athari za uharibifu wa mazingira utokanao na mrundikano wa pumba hizi na pia kupunguzia wanachi utegemezi wa kuni kama chanzo kikuu cha nishati na kupunguzia wananchi kero kutokana na mrundikano wa taka hizi.SHIME WATANZANIA tulione hili(kilimo cha mpunga) kama fursa ,na sio kero .'HAKUNA LISILOWEZEKANA CHINI YA JUA'
SOURCE:MUNYAMAKWA
 
ni wazo zuri..likifanyiwa kazi linaweza kutufikisha mbali sana hasa kwa suala la nishati..mimi mwenyewe sijawahi kulifikiria suala hili
 
pumba za mpunga kama ilinyo kwa saw dust na pumba za kahawa ni good source ya energy. kinachotakiwa ni kudesign jiko zuri litakalo tumia hizo pumba na kuwavutia watu
 
pumba za mpunga kama ilinyo kwa saw dust na pumba za kahawa ni good source ya energy. kinachotakiwa ni kudesign jiko zuri litakalo tumia hizo pumba na kuwavutia watu

Wakuu kwetu tumeanza kuchomea tofali miaka mingi sana iliyopita,maranda ya mbao tunakaangia mihogo na chips mitaa ya uswahilini. Kwa hiyo hapa inabidi tushauriane namna ya kuboresha majiko ya kukaangia chips uswahilini. Majiko yapo tayari labda tuyaongezee ufanisi.
 
sawa kabisa, hayo majiko ya pumba za mpunga tulianza kuyatumia vijijini miaka 15 iliyopita, yana moto mkali sana unaodumu kwa muda mrefu. Tatizo ni kifua tu kutokana na ule moshi
 
Back
Top Bottom