Wajanja walitafuna fedha za mafuta ya jenereta lita 800-uwanja wa taifa-Mh Mnyika

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Wakati watanzania wakihangaika kujua nini kilichotokea kuhusu upumbavu uliofanyika kwenye fainali ya kagame
na umeme kukatwa wakati kombe likitolewa mh mnyika mbunge wa ubungo amefichua siri hiyo ambayo imepelekea mh waziri kudai kuunda stupid tume kama walivyozoe kutafuta sababu nini

hata hivyo wakati tume hiyo imetajwa aijakabidhiwa hata per diem mh mnyika amewaambia kilichofanyika ni ufisadi mtupu amekuwa akifwatilia na kuongea na baadhi ya wah wa tff na kuwaambia wao walichofanya walikaa kwenye kikao na wahusika wa uwanja ule kutoka wizaran..baaada ya hapo ikazuka swala la umeme kukatika wakaandikiana kutoa lita 800 ambazo mpaka mechi imebaki dk 10 azikuwapo uwanjani wakahisi zitaletwa kipindi cha dk 30 za nyongeza akuonekana hata mhusika mmoja wa wizara si wa uwanja na simu zao kuzimwa

mh mnyika ameenda mbali na kusema mh waziri anahusika na kashfa hii maana mmoja wa watu wake alikuwepo kwenye kikao cha pre match na hata uwanjani ila ilipomalizika dk 90 akamwacha wazirina kuondoka

alisema serikali kupitia wizara ya michezo inapaswa kutoa kauli ni kwa nini upuuzi huo utokee wakati fedha za mafuta zilitolewa na zimeenda wapi iwapo ayakuwepo hata kwenye uwanjan wakati wa mechi?? Alisema kukatika uwanja ni aibu kwa taifa na aibu kwa fifa kumbuka umati uliokuwepo pale wamelipa na iwapo umeme umekatika wabaya wanaweza sogea saa yoyoyte na kuleta uharibifu usiokuwa na maana

mh mwenyekiti mh waziri lazima aje aseme kama zile lita 800 za disele waligaiana wakina na nani na kama kuna mgao basi wabunge tukaribishwe kwenye pre match huku watu wakicheka.....

Kazi ipo hii ndio serikali ya kikweete na haya ni madogo ujaenda kwenye makaratasi yao ..mnamkumbuka cag alisema kuhusu wizara hii ./.....kwasababu waliosemwa akuna kilichofanyika basi nikae kimya
 
Aibu kubwa sana na sisi wegine tulipoteza kamera zetu baada tu umeme kukatika.
 
Sasa tume juu ya nini? Si wanajulikana? Wawajibishwe! Tume ni kutafuna pesa tu.
 
tanzania kila siku matatizo pamoja na wizi wa hali ya juu kila kona...tume kuchunguza nn? Halaf iweje? Waache ujinga..
 
shida ya nchii hii inaletwa na watu wenye uroho wa madaraka na walafi wa ela, na haitaisha mpaka uwepo mfumo madhubuti wa kuwaondoa wasikaribie uongozi.
drc na tanzania zinafanana, wazungu wanachuma mali wanawaacha muumizane na shida zenu hawakemei wala kuzuia, we mpaka mmarekani anaingia katika mambo ya nishati na kujifanya atamaliza shida ya umeme. symbion kampuni ya usa inayotambulika na serikali ya usa badala ya kuja na mitambo yao mipya tena yenye uwezo mkubwa wananunua mitumba ya dowans hapo ni kujiuliza badala ya waje na mfumo mzima wa kuzalisha umeme ulio madhubuti kama coal ,gas, hydroelectric power, geo thermal, wind power nk wanakuja na njia mkato wanaiita umeme wa dharura vijenereta vyenye uwezo mdogo .
 
Back
Top Bottom