Waislam wapigania Uhuru, ni Waislam kweli?

Nyamtwee

New Member
Nov 11, 2023
4
6
Ninasoma Kitabu hiki cha Mzee Mohamed Said kuhusu Waislam kutengwa katika Historia rasmi ya wapigania uhuru.

Hapa chini nimeweka nukuu kutoka kitabu cha Maisha ya Abdulwahid Sykes ambacho kinaeleza namna waislam walivyotengwa na historia ya Uhuru. Nukuu hii ikionyesha kuwa Aziz Ally na Kleist Sykes walikuwa ndio 'waafrika weusi' pekee waliokuwa na vibali vya Kunywa pombe.

Je, hawa ni Waislam kweli?

Screenshot_20231111-185554.jpg
 
Nyam...
Kunywa pombe hakumtoi mtu kwenye Uislam lau pombe ni haramu.

Kuna Waislam achilia pombe hata kusali hawasali na bado ni Waislam.

Hii ndiyo mitihani ya dunia.

Turudi kwa Aziz Ally na Kleist Sykes.

Katika ile wagawe watawale wakoloni walikuwa na mengi wakifanya kuwagawa wanaowatawala na mojawapo ni kuwa upendeleo wa vitu ambavyo wala havina maana sana.

Aziz Ally licha ya kuwa na license ya kunywa bia alikuwa na license ya contractor ya kujenga majumba.

Kleist Sykes alikuwa Mwafrika pekee katika Chamber of Commerce na pia mjumbe wa Dar-es-Salaam Town Council.

Nakushukuru kwa kulileta hili jambo hapa kwani inasaidia kuelewa kwa nini watoto wa wazee hawa wawili Abdul, Ally Abbas, Dossa, pamoja na watoto wa Affande Plantan, Schneider na Ramadhani Mashado Plantan wakawa na uwezo mkubwa wa fedha na nguvu ya kuunda TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hawa wakafutwa katika historia ya uhuru.

Mimi nikaandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kueleza historia yao.
 
Walikua walevi ndo maana Nyerere aliwazidi sana calculation
Mpaji...
Mjadala huu unaweza ukavutia wengi tukiwa wastaarabu.

Kipi kinakufanya wewe uone kuwa Nyerere alizidi sana wengine?

Nyerere kuwa rais wa TAA historia yake nimeieleza kwenye kitabu cha Abdul Sykes kwa kirefu sana.

Muhimu ilikuwa kuepusha TANU na harakati za uhuru kuwa jambo la Waislam.

Waingereza wangewashawishi Wakristo na wao kuunda chama na hili lingefanyika tungeingia katika kudai uhuru Tanganyika ikiwa na vyama viwili vilivyojijenga katika dini kuu mbili.

Hii ndiyo ilikuwa hofu ya Hamza Mwapachu (1913 - 1962) na ndiyo sababu ya kuwaagiza Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe kuhakikisha kuwa Nyerere anachukua uongozi wa TAA 1953 na 1954 TANU inaundwa.

Vinginevyo yangetokea yaliyotokea India baina ya Congress Party ya Nehru na Ghandi na Muslim League ya Mohamed Ali Jinnah.

Bahati mbaya sana Mwalimu akitaabishwa kidogo na historia hii na hakupenda kuizungumza hata pale alipoombwa aandike historia ya maisha yake.

Ndiyo sababu kitabu cha Abdul Sykes, (1998)kimevunja rekodi ya vitabu vyote vilivyopata kuandikwa kuhusu historia ya TANU.

Yapo mengi ya kuelezana katika historia ya nchi.yetu.

Muhimu ni tuwe waungwana na tujadiliane kwa adabu.

Angalia picha za harakati za uhuru.
Nyerere siku zote kazungukwa na Waislam.
 
Walikua walevi ndo maana Nyerere aliwazidi sana calculation
Mpaji...
Soma hayo hapo chini yatakuongezea maarifa katika historia ya uhuru wa Tanganyika:

HISTORIA YA CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA NA ABDUL SYKES

Kipindi cha uongozi wa Abdul Sykes kati ya 1950 – 1954 hiki kilikuwa kipindi muhimu sana katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kuanzia mwaka wa 1951 baada ya Gavana Edward Twining kupokea mapendekezo ya katiba kutoka kwa TAA yaliyotayarishwa na TAA Political Subcommitee ambao wajumbe wake walikuwa Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Kamati hii ndiyo iliyokuwa inaweka msingi wa kuundwa kwa TANU wakati ukifika.

Rafiki wa Abdul Sykes Mwanasheria Earle Seaton alikuwa ndiye mshauri mkuu wa TAA katika mambo ya siasa na alisaidia sana katika kuandika yale mapendekezo ya katiba.

Barua za Seaton kwa Abdul Sykes katika miaka ile ni sehemu ya nyaraka nilizosoma wakati wa utafiti na zikaathiri sana fikra zangu.

Katika kipindi hiki ndipo Abdul Sykes akawa na mazungumzo na Chief Kidaha Makwaia kumtaka ajiunge na TAA wamchague kuwa Rais na kisha waunde TANU.

Chief Kidaha alikuwa chief mkubwa sana Usukumani akiwa na machifu 50 chini yake na alikuwa na heshima kubwa kwa serikali ya kikoloni kiasi walimteua kuwa mjumbe wa LEGCO mwaka wa 1945.

Chief Kidaha akiwa na majukumu haya hakuweza kumkubalia Abdul kujiondoa katika uongozi wa watu wake na kujiunga na siasa za TAA.

Historia inaonyesha kuwa kwa kipindi cha takriban miaka mitatu Abdul Sykes hakuitisha mkutano mkuu wa mwaka wa TAA akabakia yeye akiongoza TAA kama Kaimu Rais na Katibu.

Lakini inaelekea Hamza Mwapachu baada ya Abdul kushindwa kumleta Chief Kidaha Makwaia katika uongozi wa TAA, Hamza Mwapachu ndipo alipokuja na jina la Julius Nyerere kuingizwa katika uongozi ule wa juu badala ya Chief Kidaha.

Nyerere mweyewe hakupata hata siku moja kueleza uhusiano wake na Abdul Sykes na Hamza Mwapachu katika kupigania uhuru wa Tanganyika, ukiondoa alipomtaja Abdul Sykes katika hotuba yake ya kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam mwaka wa 1985 aliposema kuwa aliyempeleka kwa Abdul Sykes ni Joseph Kasella Bantu.
 
Mpaji...
Mjadala huu unaweza ukavutia wengi tukiwa wastaarabu.

Kipi kinakufanya wewe uone kuwa Nyerere alizidi sana wengine?

Nyerere kuwa rais wa TAA historia yake nimeieleza kwenye kitabu cha Abdul Sykes kwa kirefu sana.

Muhimu ilikuwa kuepusha TANU na harakati za uhuru kuwa jambo la Waislam.

Waingereza wangewashawishi Wakristo na wao kuunda chama na hili lingefanyika tungeingia katika kudai uhuru Tanganyika ikiwa na vyama viwili vilivyojijenga katika dini kuu mbili.

Hii ndiyo ilikuwa hofu ya Hamza Mwapachu (1913 - 1962) na ndiyo sababu ya kuwaagiza Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe kuhakikisha kuwa Nyerere anachukua uongozi wa TAA 1953 na 1954 TANU inaundwa.

Vinginevyo yangetokea yaliyotokea India baina ya Congress Party ya Nehru na Ghandi na Muslim League ya Mohammed Jinna
Mohamed..

Abdul alitaka Nyerere ashike Uongozi wa TAA kwa sababu ya ELIMU KUBWA NA UWEZO WA KUJENGA HOJA WA NYERERE na Abdul hakuwa kabisa na time na hayo masuala ya dini (He was a really Nationalist). Hata wakati ambao wapinzani wa Nyerere walipotumia hoja ya udini, Mufti na Masheikh kama Chaurembo waliridhia maazimio ya TAA/TANU kuwa chama hicho hakina dini—SECULAR PARTY.

Soma nukuu hii hapa;
The TAA leadership was clever enough to realise the value of Nyerere's education and its potential to the future leadership of the association and the country. Abdulwahid confided with the TAA executive that having the most educated African in the land as the president of the Association would strengthen its leadership and portray a good image before the eyes of the colonial government and the United Nations Visiting Missions. Nyerere is quoted as having said that it had been his intention to teach for a while then enter politics."

Pia hii;

In Abdulwahid, Mwalimu Nyerere found a person of high intellect, selflessness and a likeable character. In Julius Nyerere, Abdulwahid found a highly educated person with admirable debating skills. Nyerere was exposed to the world and sharpened by the politics of the Fabian Society during his student days in Britain. Very constructive debates evolved in the Sunday discussions when Abdulwahid's intellect and political experience were pitted against Nyerere's legendary debating skills.
 
Walikua walevi ndo maana Nyerere aliwazidi sana calculation
Nyerere pia alikuwa ni Mlevi(kama ulevi ni kunywa Pombe).

Nyerere alipewa kiti cha Uongozi kwa sababu mitazami ya kitaifa na mipana waliyokuwa nayo kina Abdulwahid, Dosa Aziz na Mwapachu. Halafu sijui hii hoja ya udini inatoka wapi, ukisoma kitabu cha Maisha ya Sykes, huoni mahala Uislam kama dini(kupitia taasisi na mifumo yake) umetumika kupigania uhuru.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom