Waishio na Virusi vya Ukimwi nchini wakata tamaa. Serikali haina fedha za vipimo vya CD4

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Wagomjwa wengi nchini hasa wale wanaosihshi na virusi vya Ukimwi wamekata tamaa na kuishangaa serikali ya nchi hii kwa kukosa vipimo vya CD4 kwa wagonjwa hao. Baadhi ya Wagonjwa katika wilaya ya Biharamulo maeneo ya Nyakahura wamelalamika na kusema kuwa hawaelewi kama inabidi waanza dawa au la maana vipimo vya CD4 ni tatizo.

Watu hao wanadai kuwa itakuwa ni hasara kwa serikali kuacha wananchi hao wapoteze maisha na kuacha yatima wakati wazazi wawili wenye virusi vya Ukimwi kama wakitambua Idadi ya CD4 zao na kuanza dawa mapema wanauwezo wa kuwalisha watoto wao na kuwasomesha hata kama ni 7 kuliko watu wawili kufa serikali ikaja kuhangaika na yatima 7.

Wanaopata huduma eneo la Nyakahura - Mzani wilaya ya Biharamulo wamesema kuwa taarifa walizopata ni kwamba serikali haina fedha za kuwezesha kubeba damu kutoka nyakahura hadi biharamulo mjini kwa ajili ya kupima CD4. DMO wa Wilaya hiyo anasema hakuna bajeti kwa ajili aya mafuta ya kuchukua damu za watu waoishi mbali na Biharamulo mjini ili waweze kupimwa. Kwa maana hiyo vituo vingi na wagonjwa wengi wana hali ngumu maana hawajui mustakabali wao utakuwaje.

Mbali na kukosekana na mafuta na vipimo vya CD4, hata vipimo vya kupimia Virusi vya Ukimwi ni Tatizo......zikiwemo determine na Uni Gold. Watu wengi wanahudhuria huduma za VCT lakini wanarudi nyumbani kwao bila kupima. Kila daktari aliyrko kituo chochote cha Afya hapa nchini atakuwa shahidi. Vipimo vya Ukimwi nchini ni taaabu kweli. HAkuna wa Kukanusha kwa hili. Chanzo cha vipimom kukosekana ni kuwa Serikali haina fedha za kununua vipimo hivyo kupitia MSD kama ilivyo kawaida.

Sasa kama hadi vipimo hivi navyo vinakosekana, mafuta kwa ajili ya kuchukua damu kwa ajili ya kupima CD4 hakuna, serikali kipi inakimudu nchi hii? hata panadol hakuna mahali pengine.
 
Hii ni part gazeti, kuna habari kuwa Global Fund ambao ndio wanaolipia gharama za kunua ARVs wanasimamisha ufadhili wao mwakani. hakuna serikali inayoweza kugharimia hilo. What will be the situation then!
 
Hali kweli si shwari...........thread hii ni serikali kukosa fedha za kuwahudumia waishio na Virusi vya Ukimwi lakini Mods kaweka JF Doctor........sasa ngoja tuone jibu litakalotoka. Hii sio thread ya kuomba tiba kwamba nina jipu sehemu za mwili wangu bali ni la uwajibikaji wa Serikali....irudishe Jukwaa la siasa wanaohusika wawajibike........Ofisi ya DMO kukosa mafuta ya kufuata damu unalileta JF Doctor!!!!!! Kweli nchi hii hatuponi na inawezekana wote tunakunywa viroba
 
Back
Top Bottom