engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
Wadau wa Kimataifa wa maendeleo nchini wametia saini kuchangia katika bajeti ijayo ya Serikali dola za Marekani milioni 562 (zaidi ya shilingi bilioni 840/- za Kitanzania).
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo katika mkutano wa pamoja kati ya Serikali na wadau hao uliofanyika katika hoteli ya St. Gasper, nje kidogo ya mji wa Dodoma, alisema kwamba kiasi hicho cha fedha ni zaidi ya kilichotolewa katika bajeti inayomalizika ya mwaka wa fedha 2010-2011, ambapo wadau hao walichangia shilingi bilioni 812/-
Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya (EU) wametoa jumla ya dola za Marekani milioni 109.
Nchi za Uholanzi na Uswisi hazijatoa fedha kuchangia bajeti hiyo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za msukosuko wa kiuchumi duniani.
Uholanzi na Uswisi zimesema pamoja na kutochangia moja kwa moja bajeti ya Serikali, zitaendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali.
Wadau waliochangia bajeti ya Serikali ni nchi za Canada, Denmark, Finland, Ireland, Japan, Ujerumani, Norway, Sweden, Uingereza, Umoja wa Ulaya (European Union - EU) pamoja na Benki ya Dunia (World Bank - WB) na Benki ya Afrika (Africa Development Bank - AfDB).