Wafungwa Guantanamo Vituko Vitupu!

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Wafungwa watano, akiwemo anayedaiwa kupanga mashambulizi ya Septemba kumi na moja mjini New York, Halid Sheik Mohammed walikataa kufika mahakamani.
Hii ilitakiwa kuwa mara ya kwanza kwa washukukiwa hao kufika mahakamani tangu Barack Obama awe rais.
Ingawa Rais Obama amesimamisha kesi za washukiwa walioko Guantanamo bay bado zile za utangulizi zinaendelea.
Washukiwa hao wa ugaidi walitakiwa kuwepo mahakamani lakini Jaji alipofika viti vyao vilikuwa vitupu.
Jaji huyo hata hivyo alipinga pendekezo la mwendesha mashataka kuwa watolewe kutoka walipozuiliwa kwa nguvu.
Baada ya mahakama kuihairishwa kwa muda, washukiwa watatu walifika mbele ya jaji huyo.
Lakini mmoja wao, Mustafa al Hassawi aliomba kutoka mahakamani alipoambiwa kuwa hatapewa fursa ya kuzungumza.
Kesi hiyo ilitakiwa kubaini ikiwa Mustafa Al Hassawi na mwenzake Ramsey Bin Alsheeb wana akili timamu na uwezo wakujitetea.
Wakili wa Bin Alsheeb alielezea mahakama kuwa anatatizo la akili baada ya kuzuiwa kulala, lakini wakati alipokuwa anafafanua zaidi kipaza sauti cha mahakama kilizimwa.
Washukiwa hao walionyesha wazi kuwa wanadharau mahakama hiyo na hata mmoja alimchezea mwenzake kwa kumrushia mfano wa ndege aliotengeneza na karatasi bila kujali.

SOURCE: BBC (SWAHILI SERVICE)
 
Kweli Wanyamwezi sasa ni kama bongo. lol


Kwamara yangu ya kwanza nakubaliana na wewe, You are right!! tena afadhali Bongo. wanyamwezi wanakutungia kesi, wanatesa, wana-kidnap namengineyo. Na hii ndo kazi ya CIA imeundwa kwa sababu hizo
 
Back
Top Bottom