Wafanyabiashara watakiwa kuchangamkia fursa kuchukua maduka kwenye soko la Kimataifa la Biashara linalojengwa Ubungo na EACLC

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Wafanyabiashara nchini wamehaswa kuchangamkia fursa kwenye mradi wa soko la Kimataifa unajengwa eneo la Ubungo ilipokuwa stendi ya Mkoa zamani, ambapo wametakiwa kulipia maduka mapema ili kuepuka kujilaumu siku za mbeleni mara baada ya ujenzi wa mradi huo kukamilika na kuanza kufanya kazi.

Wito huo umetolewa na wadau mbalimbali akiwemo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martine Mbwana alipokuwa akizungumza katika hafla ya utiaji saini kwa wadau mbalimbali ambao tayari wamelipia maneo ya kibiashara katika mradi huo unaodelea katika hatua za ujenzi.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Balozi wa mradi huo amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa kwenye uwekezaji huo ambao amedai kuwa utakuwa wa kisasa na wenye tija kwa pande zote ikiwa ni pamoja na kuwaondolea usumbufu Wafanyabiashara kwenda China kufuata bidhaa.

"Hapa (EACLC)panaitwa ni chuo kikuu kipya cha biashara kwetu, mimi nipo Kariakoo nimebatika pia kuishi china na nimeona masoko yaliyoko kule kuna masoko makubwa sana pale, sasa masoko hayo yamekuja huku lakini kwa sababu moja au mbili tatu, Moja Serikali ya China imepunguza watu kwenda nchini mwao imewafungulia zaidi wachina wake huku Afrika, lakini pia kutoka na changamoto za Corona na haya masuala ya kiuchumi imepunguza zaidi mwingiliano"amesema Mwenyekiti huyo

Amkiendelea kueleza amesema"Hawa EACLC wanafanya usafirishaji pia wananunua mazao kupeleka nje ya Nchi pamoja kwamba mizigo yao ambayo tunaenda kufuata China itakuwepo hapa, kwahiyo pia sisi tutaweza kuuza mizigo kwao kwa kutumia EACLC, itasaidia masuala ya ubadilishaji fedha (exchange rate) kufanya dhamani ya Shilingi yetu iendelee kuwepo kwamba tunafanya biashara kwa kutumia pesa zetu wenyewe"

Pia Mwenyekiti huyo amefafanua utaratibu moja wapo ambao utatumika baada ya mradi huo kuanza kufanya kazi, ambapo amedai kuwa Wafanyabiashara watakuwa wanapata bidhaa Moja kwa moja kutoka kwenye maghala ya wachina yatakayokuwa nchini.

"Hao wenzetu wanachokifanya wanaingia kwenye maghala ya wale ambao wana viwanda China wamekuja huku wamechukua machukua maghala wanaweka bidhaa zao, ukiwa kwenye duka la EACLC haya maduka ni kisasa sio kama yale tuliyoyazoea kwamba unakuwa na stoo kubwa ya mzigo una sampo nyingi umeweka kule ndani unashindwa hata kutambua bidhaa zako hapana, haya yatakuwa maduka ya sampo ambapo unaweza kutoa oda hapo hapo ikatoka kwenye maghala kwahiyo Wafanyabiashara wengi wa china watakuwa na maghala wazawa tutakuwa tunakaa kwenye maduka lakini kwa kuwa na brandi ya bidhaa wanazozaliza wao kwahiyo wanaowai kuchukua maduka mapema ni faida kwao kumiliki brandi."amesema Mwenyekiti huyo

Aidha Mwakilishi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)-Kanda ya Mashariki amewataka watanzania kutumia kituo hicho kama chachu ya kukuza uwekezaji, huku akiwataka wawekezaji kuendelea kujitokeza ili kuwekeza nchini ambapo amesema kuwa Rais Samia ameweka ameweka unafuu wa gharama kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza hivyo ametaka yeyote mwenye dhamira hiyo kufika kwenye ofisi zao kunufaika na unafuu huo.

"Niwaombe watanzania wenzangu karibuni sana katika kituo cha uwekezaji Tanzania ili wote tuweze kunufaika na fursa hizi ambazo Mh. Rais ametupatia."amesema Mwakilishi huyo wa TIC

Amesema kuwa katika ujenzi wa Soko hilo wameshiriki kuanzia hatua za awali, ambapo amedai kuwa mradi huo ni mkubwa kwa sababu unachochea uchumi kukua, hivyo amewasihi Wafanyabiashara kujitokeza kuchukua maeneo ya kibiashara mapema.

Mkuu wa Idara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji katika Manispaa ya Ubungo, Marry Mwakyosi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, amesema kuwa mradi huo una manufaa kwa Manispaa ya Ubungo pamoja na kwa watanzania kwa ujumla.

"Kupitia Mradi huu Manispaa ya Ubungo itakuwa mnufaika kutokana ukodishaji wa eneo ambalo mradi umejengwa, lakini watanzania kwa ujumla pia ni wanufaika wa huu mradi"amesema Mwakilishi huyo

Mkurugenzi wa Kampuni ya EACLC Ndg. Catty Wang amesema kuwa soko hilo litakuwa na maduka zaidi ya 2000, ambapo amedai kuwa mradi huo ujenzi wake ulienza Desemba 2022 na kuwa unatarajiwa kukamilika June 2024 .

Amesema kuwa wamekuwa wakishiriki katika masuala mbalimbali kuutangaza mradi huo ikiwemo kuweka mabango, kutoa vipeperushi, kutumia vyombo vya habari pamoja na kushiriki maonesho ikiwemo ya sababa.

Lakini EACLC imetangaza kuwa wateja watakaochukua maduka mapema watagharamikia kuwapeleka China na kuwazungusha kwenye maeneo manne maalumu ya viwanda pamoja na kuwarejesha nchini.

Ikumbukwe akizindua Mradi huo Aprili 2023, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema kuwa mradi huo utakuwa na tija kwa kuongeza ajira na kuchochea kukua kwa uchumi, ambapo aliwataka Wafanyabiashara nchini kuchangamkia fursa kwa kuchukua maeneo ya kibiashara.

Hafla hiyo pia imewakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara ambao tayari wameonesha dhamira ya kuwekeza kwenye mradi huo, taasisi za kibenki pamoja na taasisi za kifedha ambazo zimeeleza namna zinavyokusudia kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara pamoja na wananchi katika mradi huo kwa lengo la kurahisisha huduma.
View attachment 2817328
IMG_20231117_164528_364.jpg
IMG_20231117_180302_333.jpg
IMG_20231117_152504_395.jpg
 
Kwa maana kwamba na wachina watafungua maduka hapo?
Itakuwa sio biashara ni unyonyaji kwa wafanyabiashara wa kitanzania.
 
Back
Top Bottom