Wafanyabiashara wamkataa na kumpinga Tundu Lissu na CHADEMA yake. Wasema Serikali Ya CCM ni sikivu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu watanzania,

Wafanyabiashara wengi sana wameendelea kuonyesha msimamo wao wa kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais Samia kutokana na usikivu wake katika kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uendeshaji wa biashara zao. Wanasema kuwa serikali wakati na muda wote imetoa nafasi ya majadiliano na mazungumzo kufanyika pale panapojitokeza changamoto na wakati wote wamekuwa wakisikilizwa na kupata ufumbuzi.

Wanasema Tundu lissu na chadema yake wakati wote wamekuwa Ni watu wa kupandikiza chuki na migogoro kwa wafanyabiashara ili wafanye migomo, wametolea mfano kauli ya Tundu lissu aliyoitoa Mkoani kigoma miezi michache iliyopita akiwahamasisha wafanyabiashara kufanya migomo Jambo ambalo hata hivyo halikufanikiwa kutokana na wafanyabiashara kumdharau na kumpuuza hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa watu wanafahamu kuwa lissu na chadema yake ni matapeli, wababaishaji,wasio na misimamo, wanafiki, watu wa ndimi mbili na wasio na uzalendo wa Aina yoyote Ile kwa Taifa letu.

Wafanyabiashara wanasema kuwa kwa Sasa serikali ya Rais Samia imeweka mazingira mazuri ya kibiashara na wanafanya biashara kwa amani na utulivu pasipo bughudha Wala kero, wanasema kuwa kwa Sasa wanajiona fahari na huru sana kufanyia biashara Tanzania na kulipa Kodi kwa hiyari, wanasema wanakadiriwa Kodi kwa haki kabisa na penye shida wanasikilizwa kupitia meza ya mazungumzo.

Wanasema hawawezi kukubali kwa Sasa kutumika hovyo Kama walivyokuwa wanatumiwa miaka kadhaa iliyopita ,wanasema wapo bega kwa bega na mh Rais na wanaendelea kumuunga mkono katika juhudi zake za kuinua uchumi wa Taifa letu.

Wanasema kwa Sasa Hakuna mwenye Akili Timamu atakayeweza kuiunga mkono chadema chama ambacho kimefirisika kisera na kiajenda, lchama kilicho kosa Dira na muelekeo, chama ambacho hakina Safu ya uongozi yenye kuleta matumaini kwa watu na chenye kutanguliza mbele maslahi yao binafsi.

Rai yangu kwa akina lissu na chadema yao ni kuwa wakati Ni ukuta, kwa Sasa wapo nje ya wakati, Hakuna wa kuwaunga mkono , watanzania wa leo hawadanganyiki Wala kupotoshwa, kwa Sasa chadema wakae kwa kutulia kuangalia nchi inavyo paa kiuchumi chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Pia soma
- Tundu Lissu aonekana Kariakoo, atangaza opereshani rejesha Bandari za Tanganyika kutoka kwa Sultan wa Dubai imeanza
 
Waambie waliokutuma kuwa

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Hakuna kiongozi ambae hajafanya makubwa nchi hii...
Viongozi nao ni watu, sio malaika.
Ndio maana nawapongeza Sana viongozi wangu na serikali yetu kwa kazi kubwa waliyoifaya katika ujenzi wa Taifa letu, katika ubinadamu wao wanejitahidi Sana ndio maana kwa juhudi kubwa walizofanya inakuwa vigumu Sana kwa watu Aina ya lissu kupata uungwaji mkono kutoka kwa watanzania, hasa pale wanapotumia lugha za uchochezi.
 
Ndio maana nawapongeza Sana viongozi wangu na serikali yetu kwa kazi kubwa waliyoifaya katika ujenzi wa Taifa letu,katika ubinadamu wao wanejitahidi Sana ,ndio maana kwa juhudi kubwa walizofanya inakuwa vigumu Sana kwa watu Aina ya lissu kupata uungwaji mkono kutoka kwa watanzania ,hasa pale wanapotumia lugha za uchochezi
Tumefika mbali sana...
 
Kuna wakati watu humu walisema wewe ni ndondocha , lakini kwa andiko hili naamini waliyosema wadau
🙏🙏🙏😆 Sawa mkuu Nashukuru. Vipi naomba unijibu je Mara ngapi chadema yako imekuwa ikihamasisha maandamano na migomo hapa nchini? Unakumbuka lissu aliwataka wafanyabiashara kule kigoma wafanye mgomo? Kama wangekuwa wanawasikiliza na kufuata akili za lissu si wangegoma? Unafikiri kwanini walikataa?

Jibu ni kwa kuwa chadema kwa Sasa haina ushawishi wa Aina yoyote Ile kwa watanzania. Haikubaliki na haiungwi mkono na watanzania,ndio maana lolote itakalowaambia watanzania wafanye linapingwa kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom