Wafanyabiashara wa sukari zaidi ya 51 kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kuhodhi sukari na uhujumu uchumi

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
Wafanyabiashara zaidi ya 51 waliokamatwa kwa makosa ya kuuza sukari kwa bei juu tofauti na bei elekezi ya serikali watafikisha mahakamani muda wowote kuanzia sasa kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Hayo yamebainisha na waziri wa kilimo leo, alipokuwa akikagua shehena ya sukari tani 2900 iliyowasili bandarini Dar es salaam.

Wafanya biasha hao watafikisha mahakamani kwa makosa ya kuhodhi sukari na kupandisha bei kinyume na maelekezo ya serikali.

Waziri amesisitiza kuwa kwasasa hakuna tena upungufu wa sukari nchini hivyo sukari itauzwa kwa bei elekezi ya serikali.

Waziri ameeleza kuwa tani 21000 za sukari kutoka nchini Uganda zimewasili jana kwenye bandari ya mwanza, pia tani 38000 zinatarajiwa kuwasili bandari ya Dar es salaam hivi karibu hivyo kumaliza kabisa tatizo la upungufu wa sukari.
Amesema kuchelewa kwa sukari hiyo kulitokana na meli nyingi kuahirisha safari zake kwasababu ya Janga la Covid-19.

Waziri ameonya wafanya Biashara wenye tabia ya kuficha sukari kuwa serikali itawachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni za biashara.

Chanzo; TBC.

===
WAFANYABIASHARA 51 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kuuza sukari kinyume na bei elekezi.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, alisema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza jijini Dar es Salaam jana, kukagua na kujionea hali ya upatikanaji wa sukari.

Alisema serikali imeweka mbinu kali za kuwabaini wafanyabiashara wanaokiuka bei elekezi na kwamba itaendelea kuwatafuta na kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Waziri huyo alisema wapo wafanyabiashara nchini wanaotumia uwapo wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (covid-19) unaosababishwa na virusi vya corona, kuhodhi sukari iliyopo kwenye mzunguko na kuuza kwa bei ya juu zaidi ya bei ya ukomo ambayo ni kati ya Sh 2,600 hadi 3,200.

Alisema serikali imefanya marekebisho ya bei elekezi ya sukari kwa mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Singida na Tabora.

Alisema katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga bei ya sukari haitakiwi kuzidi Sh 2,800 kwa kilo moja na mikoa ya Singida, Tabora na Dodoma bei ya sukari haitakiwi kuzidi Sh 2,900 kwa kilo, huku katika mkoa wa Dar es Salaam bei ikitakiwa kutozidi Sh 2,600 kwa kilo moja.

Upatikanaji sukari Hasunga alisema hali ya upatikanaji wa sukari nchini imeendelea kuimarika baada ya tani 40,000 zilizoagizwa na wazalishaji wa ndani kwa ajili ya kuziba pengo la uzalishaji wa msimu wa mwaka 2019/2020 kuanza kuingia nchini.

Alisema tatizo la upungufu wa sukari lililotokana na sababu mbalimbali lilikwishapatiwa ufumbuzi na kuwataka wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya kupatikana bidhaa hiyo muhimu.

Alitolea mfano kampuni ya Alnaeem Enterprises, alisema imekuwa na sukari kiasi cha tani 1,400 tangu Jumatano iliyopita, lakini mkoani Dar es salaam kumekuwa na malalamiko ya kukosekana kwa bidhaa hiyo.

Hasunga alisema, wakati msimu mpya wa sukari ukitarajiwa kuanza mwishoni mwa Juni, serikali kupitia Bodi ya Sukari imefanya mazungumzo na kiwanda cha sukari Kilombero, ambacho kimekubali kuanza uzalishaji Mei 21, mwaka huu, huku ikiendelea kufanya mazungumzo na wazalishaji wengine ili kuanza uzalishaji mapema

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Prof Keneth Bengesi, alisema bodi hiyo itaendelea kufanya mawasiliano na Mamlaka ya Bandari Tanzania ili kuhakikisha sukari yote inayoingia bandarini kutoka nje inatolewa haraka ili iweze kusambazwa na kuwafikia watumiaji haraka iwezekenavyo.

Alisema katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, serikali imeweka mikakati ya kujitosheleza kwa sukari nchini, ambapo kutakuwa na ongezeko la uzalishaji wa miwa na sukari kupitia miradi ya Bagamoyo Sugar, Mkulazi II, S.J Sugar Mtwara, Morogoro Sugar, na shamba la Hekta 25,000 lililopo Kigoma.
 
Zitto anaposema 5 years of incompetence yuko sahihi.

Leo hii karne ya 21 eti kila mwaka kuna upungufu wa sukari.

Hii nchi sijui itaendelea lini.
Ni tatizo kubwa sana hili mkuu
 
Kesi za uhujumu uchumi huwa upewi nafasi ya kujitetea lengo kuu zilianzishwa ili kukomoa matajiri kwa kuwafanya wawe masikini kabisa ili watawaliwe
 
Hivi kama umenunua sukari kilo 3000 tsh kwa bei ya jumla halfu serikali iseme uuze 2800 tsh.
Ukikataa ndio umehujumu uchumi eti?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilichokigundua katika umri wangu huu ni kuwa Serikali za Kiafrika huwa hazijifunzi kutokana na makosa
Yaani ni experiment ambayo haiishi kiongozi mpya anakuja anarudia makosa ya kiongozi yule wa zamani
Haya mambo ni yale Makosa ya Nyerere lakini na huyu wa sasa nae anayarudia tena na tena
 
Nilichokigundua katika umri wangu huu ni kuwa Serikali za Kiafrika huwa hazijifunzi kutokana na makosa
Yaani ni experiment ambayo haiishi kiongozi mpya anakuja anarudia makosa ya kiongozi yule wa zamani
Haya mambo ni yale Makosa ya Nyerere lakini na huyu wa sasa nae anayarudia tena na tena
Nyerere ndie muasisi wa uovu wote nchi hii kwa kucopy mfumo la hovyo toka china
 
Ni wakati km nchi kuwa serious sasa na issues ndogo km izi,tufanye utafiti ni kiwango gani cha sukari kinahitajika kwa siku,viwanda vya sukari vinazalisha tani ngapi kwa siku na zinatosha kufeed watz wa ngap then tutapata gap.

Tukipata gap hapo ndo pakupafanyia kazi kama viwanda vilivyopo nchini kuongeza production au kuongeza viwanda zaidi ili kuclear hili suala maana ni la aibu mno.

Hitimisho:Tukitaka Tz iliyo bora ni lazima tupunguze vilaza kwenye system.Narudia tena kukosa sukari ni aibu hasa kwa taifa lenye sera ya viwanda.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichokigundua katika umri wangu huu ni kuwa Serikali za Kiafrika huwa hazijifunzi kutokana na makosa
Yaani ni experiment ambayo haiishi kiongozi mpya anakuja anarudia makosa ya kiongozi yule wa zamani
Haya mambo ni yale Makosa ya Nyerere lakini na huyu wa sasa nae anayarudia tena na tena
Tatizo ni chama kilekile fikra zilezile
CCM ni janga la taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nchi sasa inatakiwa iongozwe na msomi mwenye kutumia logic katika maamuzi. hii ya sasa ya kuambiw watu wapige nyungu ina watu wa primitive mno.
 
Back
Top Bottom