Wafanyabiashara wa kitanzania

Prodigal Son

JF-Expert Member
Dec 9, 2009
1,067
700
Wafanyabiashara wa kitanzania mnawaandaa watotowenu kuendeleza biashara zenu baada ya nyie kutangulia mbele ya haki?

Hili ni swala lakujadiliwa, kwani wafanyabiashara wengi ambao wamefanikiwa ila kinachosikitisha wanapoitwa mbele ya haki wengi biashara zao hazichukui muda zinakufa. Kwa kulijandili hili nawagawanya wafanyabiashara wakitanzaania kwenye makundi matatu

KUNDI LA KWANZA: Wale wafanyabiashara ambao wamefanikiwa wengine tena saana tu lakini hawana FORMAL eduacation. Kwenye hili kundi hili watu walijihitahidi na wengi walianza na biashara ndogondogo na kwa sasa wengi wana mabiashara makubwa na wengine wameenda mbali mpaka wamefungua biashara nje ya Tanzania.Wamejitahidi saana kwani ukiangalia background zao cha kusikitisha baadhi ya wafanyabiashara waliopo ndani ya hili kundi hawajali kuwaendeleza watoto wao kwa kuwapa elimu na ujuzi wakuendesha hizo biashara. Kuna baadhi wapo ndani ya hili kundi hata wake zao wenyewe hawajui biashara waume zao wanazofanya. (Mfano kuna mjasiriamali wa maduka kariakoo alipata ajali watoto bado wadogo mke alipoulizwa kuhusu mali za mume alikuwa anajua duka moja tu wakati mumewe alikuwa anamaduka matano na magorofa zaidi ya matatu).Ikumbukwe wengi waliopo ndani ya hili kundi wana mitaji mikubwa kiasi kwamba wangekuwa na elimu au kuwatumia Wataalamu wa biashara wangeweza kupanua biashara zai na kujikita kwenye kilimo, utalii, madini nk.kutakana na assert wanazomiliki wanaweza pata mikopo mikubwa saana ndani ya mabenki yetu ya kibiashara. Pia

KUNDI LA PILI: Hili linajumuisha Wanasiasa, Wasomi, na waliokuwa waajiriwa wa serekali ambao walihamua kuachana na kazi zao na kuhamua kuingia kwenye biashara. Linajumuisha waliokuwa ma CEO wa mashirika ya Umma yaliouzwa/kufa/na yaliyonunuliwa na wafanyakazi. Hili kundi bado ni dogo saana na wanajitahidi na kikubwa baadhi wanawaandaa watoto wao kwa kuwapa elimu na malezi mazuri kwa ajili ya kuja kusimamia biashara zao baada ya wao kuzeeka au kuitwa mbele yahaki. Kwakuwa hili kundi wanafanya biashara kisomi wanachangamkia fursa mbalimbali na wantoa ushindani mkubwa kwa wafnayabiashara wa kundi la TATU.

KUNDI LA TATU: Hili kundi linajumuisha wafanyabiashara Waasia/ wahindi ( naomba nisionekane mbaguzi). Ndani ya hili kundi wafanyabiashara wengi wamefanikiwa na wameridhi mitaji na biashara kutoka kwa Baba/babu zao. Mfano R M, Muhamed Dewgi na wengine lukuki.Hawa walipata upendeleo mkubwa saana tangu enzi za mkoloni na waliweza kutumia opportunities zilizokuwepo kwa uzuri kabisa. Jambo la uzuri kwao hawakuwekeza tu kwenye biashara ila waliwekeza na kwa watoto wao, waliwaandaa watoto wao ipasavyo kwa kuwapatia shule nzuri Ulaya na Marekani na kwa kiasi kikubwa watoto wao walipomaliza elimu pamoja na mbinu nyingine zikiwemo mbinu chafu kupanua biashara za wazazi wao na kuanzisha ma group of companies( mfano mzuri ni Sumaria, Muhamed enterprises etc). Hili kundi linasifika kwa kusaidiana na kupeana mbinu mbalimbali za kuendeleza biashara zao. Na ni wanyanyasaji wakubwa wa wafanyakazi na ni ngumu saana kufanya kazi kwao na kuweza kujiendeleza.

Hitimisho nini kifanyike kuondoa tatizo hili. Je tunaweza jenga biashara endelevu hata mwanzilishi wake kama hayupo biashara inabakia kuwepo na kuendelea? Hawa wajasiriamali ambao wameanzia mbali na kupata mafanikio makubwa lakini wanapokufa wanaondoka na biashara zao wasaidiweje tatizo ni mfumo au ni nini????.Je serekali inalitambua hili? Na taasisi kama Business school ya UDSM kitengo chake cha ujasiriamali wameshaliona hili????? Nini Jukumu la wafanyabiashara waliopo kwenye kundi la pili na la Tatu kuwasaidia wanzao wa kundi la kwanza???

Naamini wadau mkitoa mawazo yenu yanaweza yakatoa changamoto kwa hili tatizo
 
PG, Univumilie,

Labda nianze kwa kukosoa hayo makundi yako ma3 uliyoyaweka katika dhana hii!

Kwa Tanzania ya sasa, MACHINGA wanachukua asilimia kubwa sana ya biashara ya nchi hii...Umewaweka kwenye kundi gani?

Hata kama biashara yao hairithishwi kwa watoto wao, basi ungeainisha hivyo, kwamba hawa biashara zao ni za hand-to-mouth...basi!...maana heading inasema "wafanyabiashara wa Tanzania"..right?
 
Wamachinga wapo kwenye kundi la kwanza, sasa machinga aliyebahatika kujikusanyia mtaji akajipanua kibiashara huwezi mlinganisha na wafanyabiashara wa kundi la pili kwani bado swala la shule kwake litakuwa ni kikwazo, na ukumbuke wanafanya mambo kwa kumwangalia mwenzake ambaya walianza nae anafanya nini kama amenunua kiwanja akajenga hoteli na yeye atafanya hivyo hivyo bila kufikiria kwanza kama itamletea faida na hasara gani.
 
PG, Univumilie,

Labda nianze kwa kukosoa hayo makundi yako ma3 uliyoyaweka katika dhana hii!

Kwa Tanzania ya sasa, MACHINGA wanachukua asilimia kubwa sana ya biashara ya nchi hii...Umewaweka kwenye kundi gani?

Hata kama biashara yao hairithishwi kwa watoto wao, basi ungeainisha hivyo, kwamba hawa biashara zao ni za hand-to-mouth...basi!...maana heading inasema "wafanyabiashara wa Tanzania"..right?

PJ labda kwa hao wa kundi la kwanza naweza wagawanya kwenye makundi matatu

Kundi la kwanza lutajumuisha wale ambao hawana mtaji/ au wanamtaji kidogo na wanategemea kwenda kuchukua bidhaa na kuuza then ndo wanapeleka pesa kwa waliowapa

Kundi la pili ni wale ambao wameshapata mtaji na kuwa na biashara rasmi iliyosajiliwa

Na kundi la Tatu ni wale ambao wameshapata mtaji mkubwa na wanabiashara kubwa na wengine wanasafiri kufuata bidhaa kwa producers kama UAE, China nk.

Changamoto kwenye hili kundi kuanzia kundi la pili na la tatu je wanawaandaa watoto au ndugu zao kuzichukua hizo biashara baada ya wao kuchoka au kufa??? kama wenzao Wahindi wanavyofanya??
 
u have a good point
 
mawazo mazuri, changamoto walengwa yatawafikiaje??? kwani huku wanapitia???? i have doubt??? nadhani mawazo mengi yanaishia hapahapa tu

any way good idea
 
Mkuu malezi ndo shida unategemea nini mwanao mdogo anaposogelea dukani na kukuuliza hichi nini na kile nini unampa pipi au biskuti na kumwambia kacheze na wenzio nje.atakulia ktk mazingira hayo ya kuamini kuwa hiyo ni kazi ya baba naye haimhusu. Hata kukimpeleka shule ghali kwa uwezo wako atakachohitaji ni starehe tu maana anaamini baba anazo na ndo mwanzo wa kuwa teja.wenzetu waasia wanakuwa sambamba na wana wao kwenye kazi zao za kila siku na kuwapima mwelekeo wao mapema kwamba huyu anamwelekeo wa biashara ufundi au michezo.
 
Wafanyabiashara wa kitanzania mnawaandaa watotowenu kuendeleza biashara zenu baada ya nyie kutangulia mbele ya haki?

Hili ni swala lakujadiliwa, kwani wafanyabiashara wengi ambao wamefanikiwa ila kinachosikitisha wanapoitwa mbele ya haki wengi biashara zao hazichukui muda zinakufa. Kwa kulijandili hili nawagawanya wafanyabiashara wakitanzaania kwenye makundi matatu

KUNDI LA KWANZA: Wale wafanyabiashara ambao wamefanikiwa wengine tena saana tu lakini hawana FORMAL eduacation. Kwenye hili kundi hili watu walijihitahidi na wengi walianza na biashara ndogondogo na kwa sasa wengi wana mabiashara makubwa na wengine wameenda mbali mpaka wamefungua biashara nje ya Tanzania.Wamejitahidi saana kwani ukiangalia background zao cha kusikitisha baadhi ya wafanyabiashara waliopo ndani ya hili kundi hawajali kuwaendeleza watoto wao kwa kuwapa elimu na ujuzi wakuendesha hizo biashara. Kuna baadhi wapo ndani ya hili kundi hata wake zao wenyewe hawajui biashara waume zao wanazofanya. (Mfano kuna mjasiriamali wa maduka kariakoo alipata ajali watoto bado wadogo mke alipoulizwa kuhusu mali za mume alikuwa anajua duka moja tu wakati mumewe alikuwa anamaduka matano na magorofa zaidi ya matatu).Ikumbukwe wengi waliopo ndani ya hili kundi wana mitaji mikubwa kiasi kwamba wangekuwa na elimu au kuwatumia Wataalamu wa biashara wangeweza kupanua biashara zai na kujikita kwenye kilimo, utalii, madini nk.kutakana na assert wanazomiliki wanaweza pata mikopo mikubwa saana ndani ya mabenki yetu ya kibiashara. Pia

KUNDI LA PILI: Hili linajumuisha Wanasiasa, Wasomi, na waliokuwa waajiriwa wa serekali ambao walihamua kuachana na kazi zao na kuhamua kuingia kwenye biashara. Linajumuisha waliokuwa ma CEO wa mashirika ya Umma yaliouzwa/kufa/na yaliyonunuliwa na wafanyakazi. Hili kundi bado ni dogo saana na wanajitahidi na kikubwa baadhi wanawaandaa watoto wao kwa kuwapa elimu na malezi mazuri kwa ajili ya kuja kusimamia biashara zao baada ya wao kuzeeka au kuitwa mbele yahaki. Kwakuwa hili kundi wanafanya biashara kisomi wanachangamkia fursa mbalimbali na wantoa ushindani mkubwa kwa wafnayabiashara wa kundi la TATU.

KUNDI LA TATU: Hili kundi linajumuisha wafanyabiashara Waasia/ wahindi ( naomba nisionekane mbaguzi). Ndani ya hili kundi wafanyabiashara wengi wamefanikiwa na wameridhi mitaji na biashara kutoka kwa Baba/babu zao. Mfano R M, Muhamed Dewgi na wengine lukuki.Hawa walipata upendeleo mkubwa saana tangu enzi za mkoloni na waliweza kutumia opportunities zilizokuwepo kwa uzuri kabisa. Jambo la uzuri kwao hawakuwekeza tu kwenye biashara ila waliwekeza na kwa watoto wao, waliwaandaa watoto wao ipasavyo kwa kuwapatia shule nzuri Ulaya na Marekani na kwa kiasi kikubwa watoto wao walipomaliza elimu pamoja na mbinu nyingine zikiwemo mbinu chafu kupanua biashara za wazazi wao na kuanzisha ma group of companies( mfano mzuri ni Sumaria, Muhamed enterprises etc). Hili kundi linasifika kwa kusaidiana na kupeana mbinu mbalimbali za kuendeleza biashara zao. Na ni wanyanyasaji wakubwa wa wafanyakazi na ni ngumu saana kufanya kazi kwao na kuweza kujiendeleza.

Hitimisho nini kifanyike kuondoa tatizo hili. Je tunaweza jenga biashara endelevu hata mwanzilishi wake kama hayupo biashara inabakia kuwepo na kuendelea? Hawa wajasiriamali ambao wameanzia mbali na kupata mafanikio makubwa lakini wanapokufa wanaondoka na biashara zao wasaidiweje tatizo ni mfumo au ni nini????.Je serekali inalitambua hili? Na taasisi kama Business school ya UDSM kitengo chake cha ujasiriamali wameshaliona hili????? Nini Jukumu la wafanyabiashara waliopo kwenye kundi la pili na la Tatu kuwasaidia wanzao wa kundi la kwanza???

Naamini wadau mkitoa mawazo yenu yanaweza yakatoa changamoto kwa hili tatizo
Naomba nitofautiane na wewe kuhusu kundi la kwanza.
Unasema km kundi hilo lingepata wataalam basi biashara zao zingestawi. Huu si ukweli hata kidogo ni wataalam wangapi wamefanikiwa kuendesha biashara kwa ufanisi? Hii mie naona ni kukariri theory tu na kuamini kuwa zinaweza kufanya kazi katika mazingira yoyote.
Binafsi naamini katika natural formation ya business especially kwenye developing world. Huko hakuna mifumo ndio maana hata Taasisi nyingi haziendeshwi kimfumo. Biashara inatakiwa igrow naturally mwenye business afikiri kutokana na mazingira na si theory zilizopo. Ipo mifano kadhaa ya biashara ambazo aidha zimefeli au hazikui kutokana na kuendekeza theory za kisomi. Ukweli ustawi wa kundi la kwanza ni wa maana zaidi kwa nchi zetu tena bila kukumbatia theory za kisomi.
 
Mkuu malezi ndo shida unategemea nini mwanao mdogo anaposogelea dukani na kukuuliza hichi nini na kile nini unampa pipi au biskuti na kumwambia kacheze na wenzio nje.atakulia ktk mazingira hayo ya kuamini kuwa hiyo ni kazi ya baba naye haimhusu. Hata kukimpeleka shule ghali kwa uwezo wako atakachohitaji ni starehe tu maana anaamini baba anazo na ndo mwanzo wa kuwa teja.wenzetu waasia wanakuwa sambamba na wana wao kwenye kazi zao za kila siku na kuwapima mwelekeo wao mapema kwamba huyu anamwelekeo wa biashara ufundi au michezo.

Biashara nyingi za Wahindi Tanzania ukiangalia baada ya kuwasomesha watoto wao waliweza kuzitransform kabisa mfano mzuri ni Chande, RA, MO, Manji na wengineo wengi, babu/baba zao walianza na biashara ndogo lakini wanao waliporudi shule waliweza kuja na mawazo mapya nakuzifanya zikawa himaya. kwa Wanyamwezi wanalitambua hilo,ni wangapi wanakufa na biashara zao hata mke wanaolala kitanda kimoja hajui biashara za mume wake, hili ni tatizo kubwa ni kwa kuwa halijawekwa wazi
 
Back
Top Bottom