Wafahamu Wanefili (majitu makubwa) walioitesa dunia hadi Mungu akaamua kuwaangamiza

Wanefili ni nani? wanefili maana yake ni majitu makubwa, hawa majitu kama Goliathi, Ahimani, sheshai, Talmai, Safu, Lahmi nk walijulikana katika agano la kale.

Hawa walikuwa ni wanadamu waliozaliwa kutokana na mahusiano ya kimapenzi kati ya wana wa Mungu na binadamu, wana wa mungu hawa walikuwa ni malaika walioanguka(mapepo) ambao walioa wanawake binadamu waliwapata kwa nguvu za giza za mapepo hayo uhusiano huu ulisababisha kuzaliwa watoto Wanefili (MAJITU MAKUBWA) mwanzo 6:4.

Wanefili walikuwa kizazi kikubwa sana cha mashujaa maarufu ambao walifanya vitendo vya uovu mkubwa sana. Ukubwa na nguvu zao ulitokana na mchanganyiko wa chembe za damu ya mapepo na binadamu.

Hata hivyo kizazi hichi kiliangamizwa na gharika wakati wa NABII NUHU

View attachment 411514View attachment 413488 View attachment 413489 View attachment 413491
.
Katika uzao wa Adamu kuna mwendelezo wa uzao wa mwanamke na wa nyoka. Hata Bwana Yesu alikua akirifaa kwa kuwaambia baadhi ya watu "...enyi uzao wa nyoka..."
Hawa alidanganywa na kuangushwa na nyoka na baada ya jambo hili tuliona hawa akiwa na ujauzito na ni kipindi yeye pamoja na Adamu walifukuzwa paradiso.
Siri iliyopo hapa ni kwamba nyoka baada ya lile tukio la Edeni alibadilishwa maumbile.
Hivyo basi manafeli ni watoto waliotokana na kuona kati ya uzao wa Seti na kaini.
 
Mh mbona hiizi ni pics za movies
Which comes first movies or story?Hizo pic ni za medieval age back. Kipindi waliishi wachoraji magenius.Unadhani kwanini watu wanaheshimu elimu za kale?Hapakuwa na shule na computer km leo ila watu walitengeza hadi formula kwa anga za mbali. Watz Leo tuu mnalia eti wakenya walisoma siku nyingi hata anayekupiga bao akiwa mtoto wa class 8.
 
Sipendi kubishana na maandushi au mtazamo wa mtu ila huwa naingiaga potini kusaka ukweli hakisi.

Ukweli ni kwamba ikiwa unaamini Biblia basi tutakuwa pamoja na kukubaliana kuwa jamii hii ya wanefili ipo na ilikuepo.

Kitabu cha mwanzo 6:1-4 inatoa mtiririko mzma wa vile jamii hii ilivyotokea navkuwepo hapa duniani, binti za wanadamu walipoingiliana kingono na wana wa Mungu na kuzaa nao watoto ambao walikuwa hodari na wenye sifa enzi hizo. Pia biblia inakiri wazi kuwa kizazi hiki kilikuwa ni watu wenye maumbo makubwa sana, hata ukutacwa yeriko wanefili ndio walioujenga kwa mujibu wa Biblia maana Yoshua alipo watuma wapelelezi kwenda kuipeleleza nchi ya kanaani kalebu akiwepo kwenye kundi hili walirudisha ripot kwa wana wa israeli kuwa huko wanaishi wana wa anaki ambao ndio jamii ya wanefili tena anasema sisi kwao wametuona kama mapanzi hii inaonyesha ni jinsi gani walivyokuwa na maumbo makubwa sana. Tena wanasema hatuwezi kwenda huko kwani watu waishio humo hula watu yaani wanakulana wenyewe kwa wenyewe. Na ikumbukwe hiki kizazi ni cha ibilisi yaani nyoka, nyoka humaanisha ibilisi/shetani Mungu alipomlaani nyoka alimwambia naweka uadui kati ya uzao wako na uzao wa mwanamke, swali la kujiuliza ikiwa nyoka alimuwakilisha shetani je uzao wa shetani ni upi? Yesu aliwaambia mafarisayo na masadukayo enyi kizazi cha nyoka mwawezaje kunena mema mkiwa wabaya? Hapo yesu alidhihirisha kuwa nyoka/shetani ana uzao wake hapa duniani. Biblia imezungumzia wanefili kwa upana sana sema tu ss ni wavivu wa kusoma. Biblia imekiri wazi kuwa hawa ndio watu waliokuwa hodar na wenye sifa enzi hizo. Pia ikumbukwe baada ya muingiliano wa kingono kati ya binti za wanadamu na wana wa Mungu, Mungu alikasirika sana na kusema Roho yangu haitashindana mwanadamu milele... Kilichofanyika kilikuwa ni kitendo kiovu sana ambacho kilimfanya Mungu ashindwe kuvumilia uovu huo wa wanadamu na kukiangamiza kwa gharika enzi za Nuhu laki cha kustaajabisha kizazi hiki kinaonekana mbele tena baada ya gharika tena kikiishi kanaani na wakati wana wa israeli wanapelekwa kuirithi nchi wanakutana kizazi hiki huko. Tusomeni tusiishie kusomavwalichosoma wenzetu.
Kma wanefili walikufa kwenye gharika je mijitu kma Goliath ilitokea wapi tena ??
 
.
Katika uzao wa Adamu kuna mwendelezo wa uzao wa mwanamke na wa nyoka. Hata Bwana Yesu alikua akirifaa kwa kuwaambia baadhi ya watu "...enyi uzao wa nyoka..."
Hawa alidanganywa na kuangushwa na nyoka na baada ya jambo hili tuliona hawa akiwa na ujauzito na ni kipindi yeye pamoja na Adamu walifukuzwa paradiso.
Siri iliyopo hapa ni kwamba nyoka baada ya lile tukio la Edeni alibadilishwa maumbile.
Hivyo basi manafeli ni watoto waliotokana na kuona kati ya uzao wa Seti na kaini.
Kwahyo hao wanefili na kizazi chao kiliishia wapi
 
Kwahyo hao wanefili na kizazi chao kiliishia wapi
.
Manafeli tunaweza sema waliishia katika maangamizi ya gharika ya nuhu(phisically)
Lakini spiritually kuna muendelezo wa hichi kizazi kwani katika safina ya Nuhu kulikuwa na wana watatu wa Nuhu na walikuwa na wake zao kutoka katika jamii iliyowazunguka.
Ndio maana unakuta bado uasi au wana wa Mungu walioanguka wakiendelea baada ya safina ya Nuhu.
Sasa hivi wana wa uasi ndio wamechukua nafisi ya majitu.
 
.
Kitabu kilichowaongelea manafeli kwa kina na asili yao ni kitabu cha Henoko na kiliondolewa na kufichwa kisiwe sehemu ya biblia na manafeli hao hao.
.
Yuda 1
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.
.
Ila ukikitafuta hichi kitabu chenye huo unabii kuwahusu ndani ya biblia hukipati.
Kama kwenye biblia haukipati je wewe ulikisoma wapi?
 
Ukimchukua Hashim Thabit ukamuweka na Kichuya... Utasema Hashim Thabit ni Mnefili eti mkuu!!!!
Heheheheh wanefili wapo hadi Leo nenda NBA marekani wapo kibao akina Yao Ming ,shaquille O'Neal ,Hashim thabit,Javale McGhee, Manure Bol ,yaaani chezaji yeyote mwenye futi saba kwenda juu ni mnefili tu tutake tusitake

Nilikuwa nawaza tu
 
Kama kwenye biblia haukipati je wewe ulikisoma wapi?
Mkuu Matola hiki kitabu kipo google, nishawahi kukisoma pia, kinaitwa "a book of eenoch".. Hebu google utakiona, kinasisimua sana, ila tu sasa swali je ni kweli kiliandikwa na Enoch mwenyewe?

Pia kuna Gospel of Thomas..
 
Mkuu Matola hiki kitabu kipo google, nishawahi kukisoma pia, kinaitwa "a book of eenoch".. Hebu google utakiona, kinasisimua sana, ila tu sasa swali je ni kweli kiliandikwa na Enoch mwenyewe?
Pia kuna Gospel of Thomas..
Ni cha kiswahili au kizungu ?
 
Heheheheh wanefili wapo hadi Leo nenda NBA marekani wapo kibao akina Yao Ming ,shaquille O'Neal ,Hashim thabit,Javale McGhee, Manure Bol ,yaaani chezaji yeyote mwenye futi saba kwenda juu ni mnefili tu tutake tusitake
Nilikuwa nawaza tu
umeanza miyeyusho wewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom