Waendasha mashtaka nchini Misri wanataka Hosni Mubarak na Mkuu wa zamani wa Usalama wanyongwe.

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,371
33,019
Dah kweli waarabu kwa visasi siwawezi. Hatimaye waendesha mashtaka katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Misri ambaye aling'olewa madarakani kwa maandamano ya wananchi wanataka rais huyo wa zamani na aliyekuwa mkuu wake wa Usalama wanyongwe hadi kufa...kweli hujafa hujaumbika...Wamisri mwoneeni huruma jamani mtu mwenyewe yuko hoi muda wowote atajifia.


CAIRO: The prosecutor in the trial of Hosni Mubarak on Thursday demanded the death penalty for the ousted Egyptian leader on charges of complicity in the killing of protesters during last year's uprising against his rule.Mustafa Khater, one of a five-member prosecution team, also asked the judge for the death sentence for Mubarak's security chief and six top police commanders being tried in the same case.

"Retribution is the solution. Any fair judge must issue a death sentence for these defendants," said Khater on the third and final day of the prosecution's opening statement.

Mubarak's two sons, one-time heir apparent Gamal and Alaa, face corruption charges in the same trial along with their father and a close family friend who is a fugitive.

mid_mubarak.jpg














Prosecutor wants death for Mubarak, security boss - Arab News
 
Waendesha mashtaka katika
kesi ya rais wa zamani wa
Misri Hosni Mubarak
wametaka apewe adhabu ya
kifo. Bw Mubarak anashtakiwa
mjini Cairo kwa makosa ya
kuamrisha mauaji ya
waandamanaji, wakati wa
ghasia zilizosababisha rais
huyo kuondolewa madfarakani mwaka jana. Waendesha mashtaka pia
wanataka adhabu ya kifo
itolewe kwa waziri wa
mambo ya ndani ya nchi
Habib el-Adly na wakuu sita
wa zamani wa usalama. Zaidi ya waandamanaji 800
waliuawa katika siku 18 za
maandamano kabla ya Bw
Mubarak kuondolewa
madarakani Februari 11. "Hukumu yoyote ya haki
lazima iwe ya kifo kwa
washtakiwa hawa,"
amesema Mustafa Khater
akikaririwa na shirika la
habari la AFP. "Kamwe hawezi, kama
kiongozi wa nchi, kudai
kuwa hakufahamu
kinachoendelea," amesema
mwendesha mashtaka mkuu
Mustafa Suleiman akiiambia mahakama. "Anahusika na lazima abebe
majukumu ya kisheria na
kisiasa kwa kilichotokea",
ameongeza. Kwa kutazama ukubwa wa
mashtaka, kulikuwa na
uwezekano mkubwa wa
kutaka adhabu ya kifo
itolewe, lakini wananchi
wengi wa Misri watashitushwa kwa kusikia
madai hayo yakitolewa
waziwazi kwa mara ya
kwanza katika kesi hii,
anasema mwandishi wa BBC
mjini Cairo, Jon Leyne. Hata hivyo, iwapo Bw Mubarak
atauawa au hata kukutwa na
hatia ni swala tofauti, kwani
upande wa mashtaka
umelalamika ukosefu wa
ushirikiano kutoka wizara ya mabo ya ndani katika kutoa
ushahidi na kesi hiyo
imedhoofika kutokana na
shahidi mkuu kubadili
ushahidi wake, amesema. Upande wa mashtaka
umesema umechukua
ushahidi kutoka kwa watu
2,000, wakiwemo maafisa wa
polisi ambao walijadili amri
zilizotoka juu za kuwa na silaha na kuzitumia dhidi ya
waandmanaji. Baadhi ya watu waliokuwa
na nguvu nchini MIsri
wametoa ushahidi wao tangu
kesi hiyo ilipoanza mwezi
Agosti.
 
Back
Top Bottom