Wadogo zetu wa sasa wana ujasiri sana, sio waoga kabisa

Ivan Stepanov

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
4,891
15,956
Niende moja kwa moja kwenda jambo la msingi.

Ninayezungumza hapa pia ni kijana sio kwamba ni mtu mzima sanaa kivile, hapana. Naanza kwa kusema hili; ili kuondoa ile dhana ambayo kwa sasa inalalamikiwa na vijana wengi mitandaoni kwamba "Wazee" na "Watu wazima waliofanikiwa" wanawaonea vijana kwa kuwasema sema na kuwanyanyasa kama hivi post ambazo kwasasa zimetapakaa mitandaoni 👇👇👇

IMG-20231016-WA0021.jpg


Na hata hapa jukwaani kuna kijana mmoja juzi kati kaleta hoja kwamba "Mabroo" wamekuwa wakiwasakama tu ila hawatoi michongo yoyote pindi wanapoombwa kufanya hivyo, uzi huu ulioletwa na member Natafuta Ajira 👇👇👇


Lakini kiukweli, vijana kwasasa wana tatizo la kujiamini kupitiliza kiasi kwamba tafsiri rahisi na ya haraka unayoweza kupata ni kwamba "Don't care". Sijui sababu ni nini hasa maana kunaweza kuwepo na zaid ya moja, mfano;

1. Kujikinai/kujikatia tamaa

Sababu ya kuleta hoja hii ni tukio nililokutana nalo ofisini kwangu juzi siku ya mechi ya Simba na Waarabu. Iko hivi;

Kwa mwezi mzima toka September kuna kijana wa chuo alikuja kuomba kufanya field, na baada ya kum-study nikagundua kuwa ni mtu ambaye alichelewa kuanza field na mpaka wakati huo hakuwa amepata.

Sababu ni nyingi lakini moja wapo ni ishu ya kipato mambo ya nauli alikuwa amelenga kupata hapa centre ambako atapanda gari 1 tu kwenda na kurud nyumbani kuepuka ghara nyingi za usafiri na hana mkopo shuleni, hivyo hana fungu la field toka bodi.

Nilimu-asses kwa namna nilivyotaka ili kujiridhisha kisha nikaona sio mbaya akatu-join afterall uhitaji wa mtu kama wake kwetu ungetupa manufaa katika namna fulani.

Basi bwana tukafanya kazi weee mpaka juzi kati ambapo akawa amemaliza field yake na vyuo vinafungua so anaenda kumaliza masomo yake.

So hii siku ya mwisho nikawa na mazungumzo nae kwa ajil ya tathimini mbali mbali kulingana na majukumu aliyokuwa nayo ofisini ili kupata feedback, lakini pia kuangalia namna gani ya kuingiza tathimini hizo katika Logbook yake ili ikasahihishwe na supervisor wake.

Sasa hii siku ndio ilikuwa inachezwa mechi ya Simba na Mwarabu, na mida kama hii ya 11 kwenda 12 ndio tulikuwa kwenye discussion. Sasa katikati ya mazungumzo, kwanza dogo full time kuchat chat.

Hii kitu nilishawahi kumuona nayo hata katika vikao vya kawaida vya ofisi na nikampa warning na kumfunza ni namna gani anapaswa kuwa ana-behave anapokuwa katika mazingira ya kikazi haswa kwenye vikao akiwa na sie seniours wake.

Sasa siku hii aliniacha hoi huyu bwana mdogo, ghafla katikati ya maongezi akainuka na kusema "Bosi, nafikiri hayo mengine nitatafuta muda mwingine tumalizie, mimi nataka niwahi kumuona Rais wa FIFA hapo Taifa maana muda umeenda sana na mechi itaanza sitaki kuikosa, unaonaje Boss?" 😂😂😂😂😂😂

Honestly, nilipigwa na butwaa sana kwa hizi guts alizonazo huyu dogo, nikamtazamaa kisha nikasema sawa haina shida, unaweza kwenda.

Alipotoka ofisini nilijikuta nacheka sana lakini hakikuwa kicheko cha furaha bali ni mshangao na huruma pia. Nikajiuliza hivi ni mimi tu ndio nilikuwa fala linapokuja suala la kazi au? Hivi huu ni ujasiri au recklesness?

I was about to let him know kwamba we would love him to join us us next year akimaliza chuo maana mapungufu yale madogo madogo ningejua namna ya kum-shape maana bado ana mindset ya kitoto kama mwanafunzi, ila kwa hiki kilichotokea nikashindwa hata kufika huko kote.

Sasa hapa vijana unawaza, unasema hivi wanataka nini tena?

Anyway ni hayo tu, na by the way sio vijana wote wako hiv!
 
Niende moja kwa moja kwenda jambo la msingi.

Ninayezungumza hapa pia ni kijana sio kwamba ni mtu mzima sanaa kivile, hapana. Naanza kwa kusema hili ili kuondoa ile dhana ambayo kwa sasa inalalamikiwa na vijana wengi mitandaoni kwamba "wazee" na "watu wazima waliofanikiwa" wanawaonea vijana kwa kuwasema sema na kuwanyanyasa kama hiv post ambazo kwasasa zimetapakaa mitandaoni 👇👇👇

View attachment 2790127

Na hata hapa jukwaani kuna kijana mmoja juzi kati kaleta hoja kwamba "mabroo" wamekua wakiwasakama tu ila hawatoi michongo yoyote pindi wanapoombwa kufanya hivyo katika uzi huu ulioletwa na member Natafuta Ajira 👇👇👇

LAKINI KIUKWELI , vijana kwasasa wana tatizo la kujiamini kupitiliza kiasi kwamba tafsiri rahisi na ya haraka unayoweza kupata ni kwamba "DON'T CARE".
Sijui sababu ni nini hasa maana kunaweza kuwepo na zaid ya moja mfano
1. Kujikinai/kujikatia tamaa

SABABU YA KULETA HOJA HII ,ni tukio nililokutana nalo ofisin kwangu juzi sikubya mechi ya Simba na Waarabu.

Iko hivi, kwa mwez mzima toka September kuna kijana wa chuo alikuja kuomba kufanya field, na baada ya kum study nikagundua kuwa ni mtu ambaye alichelewa kuanza field na mpaka wakat huo hakua amepata. Sababu ni nyingi lakini moja wapo ni ishu ya kipato mambo ya nauli alikua amelenga kupata hapa centre ambako atapanda gari 1 tu kwenda na kurud nyumban kuepuka ghara nying za usafiri na hana mkopo shulen hivyo hana fungu la field toka bodi.

Nilimu asses kwa namna nilivyotaka ilibkujiridhisha kisa nikaona sio mbaya akatu join afterall uhitaji wa mtu kama wake kwetu ungetupa manufaa katika namna flani.

Basi bwana tukafanya kazi weee mpaka juz kati ambapo akawa amemaliza field yake na vyuo vinafungua so anaenda kumaliza masomo yake.

So hii siku ya mwisho nikawa na mazungumzo nae kwa ajil ya tathimin mbali mbali kulingana na majukum aliyokuwa nayo ofisini ili kupata feedback lakin pia kuangalia namna gani ya kuingiza tathimin hizo katika Logbook yake ili ikasahihishwa na supervisor wake.

Sasa hii siku ndio ilikua inachezwa mechi ya simba na mwarabu, na mida kama hii ya 11 kwenda 12 ndio tulikuwa kwenye discussion . Sasa katikat ya mazungumzo , kwanza dogo full time kuchat chat. Hii kitu nilishawah kumuona nayo hata katika vikao vya kawaida vya ofis na nikampa warning na kumfunza ni namna gani anapaswa kuwa ana behave anapokua katika mazingira ya kikaz haswa kwenye vikao akiwaa na sie seniours wake.
Sasa siku hii aliniacha hoi huyu bwana mdogo, ghafla katikar ya maongezi akainuka na kusema "BOSS, NAFIKIRI HAYO MENGINE NITATAFUTA MUDA MWINGINE TUMALIZIE, MIMI NATAKA NIWAHI KUMUONA RAIS WA FIFA HAPO TAIFA MAANA MUDA UMEENDA SANA NA MECHI ITAANZA SITAKI KUIKOSA, UNAONAJE BOSS?"
😂😂😂😂😂😂

Honestly, nilipigwa na butwaa sanaa kwa hiz guts alizonazo huyu dogo, nikamtazamaa kisha nikasema sawa haina shida, unaweza kwenda.

Alipotoka ofisin nilijikuta nacheka sana lakin hakikua kicheko cha furaha bali ni mshangao na huruma pia. Nikajiuliza hiv ni mimi tu ndio nilikua fala linapokuja suala la kazi au? Hiv huu ni ujasiri au recklesness? .

I was about to let him know kwamba we would love him to join us us next year akimaliza chuo maana mapungufu yale madogo madogo ningejua namna ya kum shape maana bado ana mindset ya kitoto kama mwanafunzi, ila kwa hik kilichotokea nikashindwa hata kufika huko kote. ..

Sasa hapa vijana unawaza unasema hivi wanataka nini tena.

Anyway ni hayo tu na by the way sio vijana wote wako hiv!.

VIJANA wengi ndio wapo hivyo.
Hao ambao hawapo hivyo ni mmoja mmoja.

Bora Wanawake kidogo wananidhamu kazini. Kiufupi kuna hatari ya vijana kuzidiwa na mabinti hasa katika kufanya kazi
 
VIJANA wengi ndio wapo hivyo.
Hao ambao hawapo hivyo ni mmoja mmoja.

Bora Wanawake kidogo wananidhamu kazini. Kiufupi kuna hatari ya vijana kuzidiwa na mabinti hasa katika kufanya kazi
Yeah brother , you are right.
I have one intern ofisn , a lady fresh from school, ana behave smart&proffesional mpaka dah!!! Katika kaz , mabint wako loyal zaid
 
Niende moja kwa moja kwenda jambo la msingi.

Ninayezungumza hapa pia ni kijana sio kwamba ni mtu mzima sanaa kivile, hapana. Naanza kwa kusema hili ili kuondoa ile dhana ambayo kwa sasa inalalamikiwa na vijana wengi mitandaoni kwamba "wazee" na "watu wazima waliofanikiwa"

Anyway ni hayo tu na by the way sio vijana wote wako hiv!.
Tukiona vijana wamepotea njia basi wazazi na watu wazima ndani ya jamii wanatakiwa kulaumiwa.
 
Niende moja kwa moja kwenda jambo la msingi.

Ninayezungumza hapa pia ni kijana sio kwamba ni mtu mzima sanaa kivile, hapana. Naanza kwa kusema hili ili kuondoa ile dhana ambayo kwa sasa inalalamikiwa na vijana wengi mitandaoni kwamba "wazee" na "watu wazima waliofanikiwa"
Wewe ni mvumilivu kmzidi anaye tajwa kuwa Yesu.
Mimi nisingeli mpatia hata hiyo nafasi nyingine ya kuongea wala kumfungia data zake.
 
Tukiona vijana wamepotea njia basi wazazi na watu wazima ndani ya jamii wanatakiwa kulaumiwa.
Inawezekana pia.Parenting katika manners za kawaida kama hiz ina play part..sasa utafanyaje na wakat kwasasa ukijaribu kuwalea watoto kama tulivyolelewa sisi jamii inaanza kukuona kama mkatili na mnyanyasaji ..mara sijui wasije pata stress wakajinyonga ? 😂 kwahiyo nowadays malez ni "JUNIOR STYLE OF PARENTING" kwenda mbele
 
Katuka mambo nayo najitahidi kuwajengea vijana wangu ndugu hata na watoto wangu wadogo basi ni uwezo wa kubehave kama watu wazima huku wana umri mdogo.

Yani leo kijana wa miaka 18 inatakiwa awe ni mtu anayejua vi,uri kuishi na watu,na kubehave vizuri.

Yaani inatakikana kijana wa miaka 18 awe na uwezo wa kuvaa suti na kukaa bungeni na kujenga hoja mbalimbali za nchi.

Lakini wazazi hasa wababa hawana muda wa kukaa na watoto wao kuwajengea uwezo wa kufanya mawqsiliano(communicstion skills) na uwezo wa kujenga hoja na uwezo wa kuzungumza vizuri na watu.

Wazazi wako bize kutafuta kula watoto wale huku kichwani watoto ni mabogus.
 
Back
Top Bottom