Wadhamini wasweka rumande kwa kuvaa suruali mlegezo

Xuma

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
683
196
Wadhamini wasweka rumande kwa kuvaa suruali mlegezo
Monday, 25 October 2010 07:47


Na James Magai

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Ijumaa iliyopita iliwasweka mahabusu siku 14 wadhamini wawili wa mshtakiwa baada ya kuingia mahakamani wakiwa katika hali ambayo mahakama hiyo iliitafsiri kuwa ni nusu uchi.

Kabla ya mahakama hiyo kuamuru waswekwe rumande mwishoni ,wadhamini hao Ramadhani Bakire (19) na Mgeni Jetta (22) walifika mahakamani hapo kwa lengo la kumuwekea dhamana ndugu yao anayekabiliwa na kesi ya jinai.

Wakati wakiingia mahakamani hapo walikuwa wamevalia suruali aina ya Jeans wakiwa wamezifunga kwa mikanda chini ya makalio katika mtindo uitwao “kata k” huku nguo za ndani zikionekana hadharani.

Hakimu Wilberforce Luhwago aliyekuwa akisikiliza kesi ya ndugu yao huyo alilazimika kuacha kusoma barua zao hizo za udhamini baada ya kuona nguo zao za ndani zikiwa nje hadharani ndani ya mahakama na kuwahoji sababu ya kuingia mahakamani wakiwa wamevaa namna ile.

“Ninyi kwa nini mnaingia mahakamani mkiwa mvaa nguo huku mmezishusha namna hiyo?” alihoji Hakimu Luhwago.

“Mheshimiwa Hakimu, kosa la kwanza si kosa tusamehe tu na siku nyingine hututakuja hivi,” alijibu mmoja wa wadhani hao, Ramadhani Bakire huku akipandisha suruali yake baada ya kubaini Hakimu kutopendezewa na hali.

Hata hivyo licha ya utetezi wao huo, Hakimu Luhwago aliyeonekana kukerwa na hali hiyo aliwaambia kuwa kamwe hawezi kuruhusu Mahakama kugeuka kuwa uwanja wa kufanyia maigizo na kwamba karipio la mdomo pekee halitoshi isipokuwa kuwapumzisha rumande

“Siwezi kuwapa karipio la mdomo kama njia ya kuwafundisha jinsi ya kuingia Mahakamani kwa adabu.Nafikiri aina ya uvaaji mliouvaa umeanza kukubalika kwa baadhi ya macho ya watu na katika baadhi ya maeneo fulani fulani;

Lakini kwa hakika siwezi nikaruhusu na Mahakama nayo kuwa sehemu inayoweza kuvaliwa uvaaji wa aina hii, huu ni uhuni. Kwa hiyo mtapumzika ndani (mahabusu ) hadi kesi hii itakapotajwa tena hapa mahakamani (Novemba 5 mwaka huu)” alisema Hakimu Luhwago.

Mwanamke mmoja aliyejiambulisha kwa Hakimu huyo ni dada wa vijana wadhamini hao alimuomba hakimu huyo awasamehe kwa kosa hilo, lakini bila mafanikio.

“Umeshindwa kuwalea na kuwafudisha kuwa aina ya uvaaji huo una mipaka, najua kazi ya malezi ni ngumu, na hata viongozi wa dini hawajafanikiwa sana katika hilo;

Kwa hiyo ndio maana sasa Mahakama inasaidia ulezi huo angalau kwa siku 14 tu hawatahitaji kufunzwa tena na hawatorudia tena kuingia kihuni mahakamani,” alisisitiza Hakmu Luhwago.

Source Mwananchi
 
La - adhabu kali kweli. Siku 14 Lupango!

Naamini walistahili adhabu lakini si kubwa hivyo.
 
Back
Top Bottom