Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 119,024
- 221,637
Kwenye Ibada Maalum ya kumbukumbu ya miaka 23 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, iliyofanyika huko Mkoani Kagera, Viongozi kadhaa wa Kitaifa wamehudhuria, akiwemo Mh Rais Samia Suluhu na Makamu wake, Dr Philipo Mpango , Tunawapongeza kwa jambo hilo.
Sitaki kurudia yaliyotokea ili nisiwachoshe, lakini Kitendo cha Rais na Makamu wake kuingia na Viti vyao vya enzi ndani ya kanisa kimepingwa na wadau wengi, huku wakitahadharisha viongozi kuacha kujiona ni wa kipekee, ukweli ni kwamba HAWANA UPEKEE WOWOTE, ukiachilia mbali vyeo walivyo navyo hawana tofauti yoyote nyingine na sisi wengine.
Kitendo cha kuingia na Masofa yao Kanisani ni DHARAU KWA WAUMINI na Kanisa kwa ujumla, na kinapaswa kukemewa ili kisirudiwe tena, kama hawataki kukaa kwenye mabenchi ya kanisa, basi wasiingie kwenye Makanisa, waishie nje na hotuba zao.
Ziko Picha kadhaa zikiwaonyesha Joe Biden wa Marekani na Haikainde Hichilema wa Zambia wakiwa wameheshimu madhabau na kukalia Mabenchi ya kanisa, mbona walishiriki ibada na wakamaliza kwa amani tu, hawa viongozi wetu wana upekee gani hawa?
Angalizo: Sina chuki yoyote na viongozi hawa.