Wadau msaada unahitajika

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,314
1,366
Hope mmekuwa na j2 njema

Wadau niko kwenye ndoa mwaka wa tano sasa. Hatujabahatika kupata mtoto na wife. Katika hili sijaona shida kubwa kozi tunamwamini Mungu, tunaimani siku moja tutapakata mtoto.

Shida yangu iliyopelekea kutaka maoni yenu ni kwamba, kwa mda sasa mke wangu amepoteza kabisa kuniamini.

Tukiwa outing au ata church nikimsalimu mwanamke yeyote ujue case hiyo itaisha baada ya mwezi.

Ameanzisha tabia ya kuperuzi cm yangu sana. Ata ni add jina jipya... Lazima ntaambiwa huyu ni nani... Nisiposema ugomvi unazuka. Baadae atachukua cm na atatumia huduma za mpesa au tigo pesa kujilizisha jina la mhusika.

Kazini kwangu kaniwekea ma-spy .yote niliyofanya job, nakuta ana taarifa A-Z

Hata hivyo, naomba kukiri , amewahi kukuta chatting ambazo zimejaa matani ya chumbani sana....kwa nyakati tofauti na baadhi ya marafiki zangu au wafanyakazi wenzangu wa kike.

Kwa kweli maisha haya naona yamekuwa kama kitanzi. Uhuru umekosekana, japo ni mke ila kama binadamu nafikiri nahitaji private fulani hivi.

Wadau plz Naombeni uzoefu wenu wa kudili na hali kama hii... Coz nahisi kusafocate wakuu.
 
Wife ana stress kaeni chini muyajenge. Labda kuna vitu vya tofauti ameviona kwako ndio maana amekua hivyo
 
Mke wako atakuwa na wasiwasi wa wewe kutafuta mtoto mahali pengine, maana yeye anaona ni muda mrefu umepita hajapata, na haamini kama wewe una subira unayoionesha, huenda anaona unaact
 
Mkuu;
Bado hujapata stress, ngoja mama yako au dada zako wakutembelee waliamshe dude. Utatamani ardhi ipasuke ikumeze. Huu sio wakati wa ku chart na wanawake wa nje. Huu ndiyo wakati wa kutiana moyo na kwenda kwenye maombi zaidi wewe na mkeo. Kamwe usimzungumzie habari za kuchelewa kwa vyovyote kurudi home. Kamwe usimzungumzie habari za kuchoka sana kwa kazi kiasi cha kuikosa dozz yake ya kila siku.
Uwe karibu sana naye na kumwambia kuwa, hukuenda kuoa watoto bali ulienda kumuoa yeye. Mhakikishie kuwa, mmepata watoto ni shukrani kwa Mungu, mmekosa watoto mtamshukuru Mungu. Asijaribu tu kuchepuka kwani akifanikiwa huko nje, ni balaa kwako na maisha yako.
Heku uwe siriasi kwa maombi kwani yanalipa. Na kwenda hospital kufanyiwa uchunguzi
 
Wanandoa wengi mnajisahau na kuanza kuishi kwa mazoea, kama you are always on the phone hata mimi ningekupekua simu yako kila nipatapo muda

May be she just need your attention. . Mpe muda wako zaidi urudipo nyumban, trust me she wont hv tym kukimbizana na hiyo simu
 
Asante sana
 
Mkuu;
Bado hujapata stress, ngoja mama yako au dada zako wakutembelee waliamshe dude. Utatamani ardhi ipasuke ikumeze. Huu sio wakati wa ku chart na wanawake wa nje. Huu ndiyo wakati wa kutiana moyo na kwenda kwenye maombi zaidi wewe na mkeo. Kamwe usimzungumzie habari za kuchelewa kwa vyovyote kurudi home. Kamwe usimzungumzie habari za kuchoka sana kwa kazi kiasi cha kuikosa dozz yake ya kila siku.
Uwe karibu sana naye na kumwambia kuwa, hukuenda kuoa watoto bali ulienda kumuoa yeye. Mhakikishie kuwa, mmepata watoto ni shukrani kwa Mungu, mmekosa watoto mtamshukuru Mungu. Asijaribu tu kuchepuka kwani akifanikiwa huko nje, ni balaa kwako na maisha yako.
Heku uwe siriasi kwa maombi kwani yanalipa. Na kwenda hospital kufanyiwa uchunguzi
Ubarikiwe, kuna kitu nimejifunza
 
Back
Top Bottom