Wadau hii Pre-Order ya Phantom6 Kutoka Tecno Veepee? Mi nimeipenda.

Wanazo mbili, hii Phantom 6 na 6+ hii ya 6+ ndio naskia ina MP21.
Sio unasikia bali kuwa muwazi kwamba wewe ni mfanyakazi wa techno upo hapa kwa ajili ya sales promotion kwa brand yenu mpya,hii pia itasaidia watu kukuamini hiki unachotangaza na pia kujibu maswali ya watu na kuondoa hofu yao juu ya simu hizi za Techno.
 
Eti wanasema ukiagiza Phantom6 yenye ukubwa wa ROM 32GB,RAM 3GB,kamera mbili za nyuma zenye 13MP na 5MP,muonekano wa kuvutia pamoja na uwezo wake wa ajabu wa kuingiza chaji kwa haraka unapewa mizawadi kibao.

Bei ya kuagiza yaani Pre-Order ni 50,000/= (Elfu hamsini) Halafu baadaye unamalizia kiasi kitakachokuwa kimebaki, unapewa zawadi na simu yako.

fetch

Kilichonivutia zaidi ni kwamba na Mshkaji Alikiba atakuwepo na mtu anayeagiza hiyo Phantom6 yao anapiga nae picha.
fetch

Mi nimeona kwenye mtandao wao tu na wanasema hii itafanyika kuanzia saa 8 kamili mchana kwenye viwanja vya City Mall Posta Dar siku ya jumamosi ya tarehe 8 Oktoba 2016.

Du!!! Kuna watu bado mnatumia mchina w tecno n uyo mshikaji wako nae anaitumia iyo tecno kweli JPM kabana.
 
Sio unasikia bali kuwa muwazi kwamba wewe ni mfanyakazi wa techno upo hapa kwa ajili ya sales promotion kwa brand yenu mpya,hii pia itasaidia watu kukuamini hiki unachotangaza na pia kujibu maswali ya watu na kuondoa hofu yao juu ya simu hizi za Techno.
Kwasabu mi napenda simu za Tecno huwa ni mfuatiliaji sana na mara nyingi hata kama mtu simu ya Tecno inamsumbua, naweza kumwelekeza. Kwa ufupi sifanyi kazi Tecno ila napenda sana Tecno na nafahamu mambo mengi kuhusu Tecno. Wazo lako ni zuri sana Frank Wanjiru, nashukuru aise, ila ukitaka kuuliza we niulize.
 
Mleta mada analipwa kwa Mwezi,ni mwajiriwa wa Techno.
Wabongo acheni hizo, mi kuwashirikisha fursa hii tu nimekosea? Ndio maana madili yakitokea watu huwa wananyamaza. Mi nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa simu za Tecno, kama unahitaji kuuliza we niulize kwani kuna wakati huwa hata narekebisha settings.
 
Tecno ya kuzidi laki 2 bora niende brand ya kueleweka
Ukijaribu kutumia Tecno ya zaidi ya laki mbili ndio utaamini ubora wake, ukitaka kitu rahisi utapata kisicho na ubora mi nilinunua Tecno Camon C9, ndio ninayotumia sahivi ni simu moja ninayoipenda sana! Usinunue za laki laki.
 
Wewe ni mfanyakazi mbea kwani tecno si wana account yao haya matangazo waacheni walete wenyewe walipie JF ifike mbali kuitangazia kampuni kama tecno ni upumbavu
 
Ukijaribu kutumia Tecno ya zaidi ya laki mbili ndio utaamini ubora wake, ukitaka kitu rahisi utapata kisicho na ubora mi nilinunua Tecno Camon C9, ndio ninayotumia sahivi ni simu moja ninayoipenda sana! Usinunue za laki laki.
Kama mtu kweli una matumizi hasa ya smartphone mbali ya kupiga na kupigiwa simu na kutuma SMS techno sio simu ya kutumia.
 
Kama mtu kweli una matumizi hasa ya smartphone mbali ya kupiga na kupigiwa simu na kutuma SMS techno sio simu ya kutumia.
Hayo ni maoni yako mbona watu tunatunmia hadi kutumiana madocument makubwa, lakini hata hazisumbui, tatizo inawezekana either hujui kutumia smartphone au unayo ya laki.
 
Back
Top Bottom