Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 10,036
- 20,281
Naomba kuongea na wachungaji wa kilokole hapa, nadhani hii itapunguza na makelele ya watu kulalamika kuwa mnapiga mno kelele kwenye makanisa yenu. kuna tabia mnazifumbia macho ila sio za Kimungu zimeenea sana makanisani. Mimi ninayeongea ni mlokole, sio wa mitume na manabii, hao huwa nawahesabu ni matapeli na wezi. mimi nimeokoka na ninasali kanisa la kipentecost. tunaingia mwaka mpya, naomba Mungu atusaidie, atusamehe pale tulipokosea, atuoshe kwa Damu yake, tuishi maisha matakatifu, tuache kupoteza muda, tuukomboe wakati kwasababu muda tuliobaki nao ni mchache sana, Yesu Kristo yuaja kulichukua kanisa lake. angalia usijecheleweshwa na mambo ya dunia, ukaachwa.
Kwanza niwapongeze watu wote waliookoka, kwasababu wamechagua fungu lililo jema, ukiokoka wewe ni mtoto wa Mungu, wakati wale ambao hawajaokoka wao ni wana wa Mungu. wewe hata ukikosea, utashughulikiwa kama mtoto wa nyumbani, tofauti na mwana ambaye hakai nyumbani. Yesu Kristo ni advocate wetu kwa kupitia Damu yake, Damu yake inanena mema kwa wale waliompokea. ninyi ambao hamjampokea, hamna mwombezi/advocate, hamna Damu ya kuwaokoa, mtajiokoa wenyewe na hamtaweza. hivyo kwa hiki nitakachokiandika hapa msifikiri nawasema walokole hapana, hawa ni heri kuliko ninyi msiookoka, nataka kuwajenga tu ili waendelee na wokovu. nanyi msiookoka nawakaribisha kwa Bwana katika Mwaka hu mpya, anza na Bwana, ishi na Bwana. hakuna aliyemkimbilia akaaibika.
1. KUSIFU NA KUABUDU: kipindi hiki, mnakiweka cha muda mfupi sana, kuna dakika chache za kusifu, na dakika chache zaidi za kuabudu. kwenye kusifu mnatuwekea vijana wahuni wanaotupotezea muda, mtu umeacha kazi zako unaenda kusali unafika pale kakijana kanavaa kisharobaro kahuni tu mnakaweka pale kaabudishe, ibada inakuwa kavu tunarudi hivyo hivyo. tunataka wale mnaotuletea kusifu na kuabudu wawe wamejiandaa, wamefunga, wameutafuta uso wa Mungu akisimama pale Nguvu za Mungu ziwepo, hatuji kanisani kukutana na ninyi, tunakuja kukutana na Nguvu za MUngu.
2. AINA ZA NYIMBO: Biblia inasema "wala msiifuatishe namna ya dunia hii"..vijana mnaotuwekea kutuabudishia au kusifu na kuabudu, wanacopy namna ya nyimbo za duniani wanaleta huku, wanabadilisha maneno tu, wanacopy namna ya kucheza duniani wanaleta madhabahuni. wapo vijana madhabahuni wanacheza sebene, ndomboro, wengine wanacheza kama Diamond na hamonize kabisa, vilevile. na aina hiyo ya uchezaji ikianza, utakuta wanawake wengi wameinuka wanacheza kama wapo disco, ni kama wameamsha lile shetani la disco walilokuwa nalo zamani, wanakumbushia na kutoa stress pale, na wanaamini wanamchezea Mungu. huu ni uhuni na Mungu hawezi kuonekana mazingira hayo. Ina maana Roho Mtakatifu ameshindwa kuwatafutia tyuni, au maneno ya kuweka kwenye wimbo, au namna ya kucheza? hadi muige uchezaji na lafudhi za kina Diamond? kweli? aokoaye ni Mungu wala sio uwezo wenu wa kucheza au kuimba, kama uimbaji wenu au uchezaji wenu hauna Mungu ni kujilisha upepo.
3. MAHUBIRI: mnatumia muda mchache wa kuhubiri, muda mwingi mnautumia kwenye matangazo na michango. kama hamjui, ukihubiri kwa Nguvu za Mungu hauhitaji kutangaza tangazo la michango au kuhudhuria ibada za katikati kwa nguvu, watu wenyewe watajiongoza kwasababu wameona kuna Mungu. kama hakuna Mungu ndio mtakamuanaaa hadi michango midogo tu. nawashauri tafuteni Mungu, Mtafuteni MUngu na Nguvu zake, mkifanikiwa kwenye hilo vingine hivyo ni vitu vidogo sana mkiwa na Mungu.pia tumeacha shughuli zetu mfano jumapili, tumeiweka wakfu kwa ajili ya Mungu, mnaweka ibada fupi mnataka twende wapi, mnakimbilia wapi, wiki nzima tupo bise, tunataka kuabudu hadi stress zote zitoke, na mtufundishe hadi tuchoke. Roho aongoze, sio ratiba zenu. hatutaki kuabudu dini, tunataka kumwona Mungu halisi wa kitabu cha Matendo ya Mitume.
4. KUABUDU: wafundisheni watu wenu kwamba, Mungu hapatikani wakati unapopayukapayuka, Mungu anapatikana kwenye utulivu, basi hata kama unaimba kwa nguvu basi uwe wimbo wa kuabudu mzuri, sio mandombolo na masebene ya kicongo hapa. hayo manyimbo ya kicongo mnaimba kwa kunengua viuno utafikiri mnazini, mnaruka kimasai nini na nini sijui, wala Mungu hapatikani. Mungu hupatikana kwenye utulivu, hapo ndipo mahali pa siri yaani ndaniii kule rohoni sio huku mwilini unaruka kwa kutumia ugali. hata wale ambao walishawahi kumwona Mungu maishani mwao, ni wale waliofanya maombi ya kufunga mfano, wakasoma Neno la Mungu na kutafakari, wakaingia chumbani, wakafung amlango, wakafunga simu na kila kitu, wakamwabudu Mungu kidogo, wakaingia kwenye kuomba then kutafakari kwa ndaniiiii kwenye ulimwengu wa Roho, hapo ndipo Roho Mtakatifu mwenyewe huamua kuomba kwa kukusadia wewe ndani yako. Maombi pekee yenye uhakika wa kujibiwa ni Maombi ya Roho, ya kimwili hayana uhakika. wengi mtasema mbona tukiwa tupo semina au maombi ya wengi Roho Mtakatifu huwa anashuka, ndio anaweza kushuka yeye hapangiwi hana sheria atashuka wakati wowote na popote, ila mimi nilikuwa nashauri wale ambao wamepanga kwamba nataka kuongea na Mungu na Mungu aongee na mimi kabisa, hilo ni mara chache linatokea kwenye jumuiya, na hao wanaonena public kwenye jumuia wengine ni mapepo though weingine pia ni wananena kwa Roho.
DAUDI ALICHEZA HADI NGUO ZIKADONDOKA; wengi wanachukua mstari huu wakisema hata watu makanisani wacheze kwa namna zozote zile kwasababu Daudi alifanya hivyo. Ukiangalia, utakuta kwa desturi za kipindi kile, hata Daudi alikosea ndio maana watu walimshangaa, imekuwaje, na pia wale walikuwa wanaabudu Mungu kimwili, sisi tunaabudu kiroho, leteni nyimbo tulivu za kuabudu na waabudishaji wasiwe wadhaifu wa imani/wazinzi na ambao hawajajiandaa, hawatatusaidia. na nyimbo hizo za kuabudu ziwe muda mrefu watu wazame, sio mnaimbisha kidogo tu kama mnafukuzwa na nini sijui, tayari mmeshasimama mnaleta neno kidogo tu ibada imeisha. jaribuni kuweka nyimbo za staha kwa muda mrefu, hivi tukiabudu hata kwa masaa mawili au hata matatu watu wanazama tu Mungu hatashuka? au mnataka Mungu asiwe anashuka tunaabudu kwa kulipua na mchungaji umekaa hapo unasubiri sadaka. ndio maana wanatoa kidogo. hata kama Biblia inasema tunaweza kucheza tunapomsifu Mungu (Zaburi 149:3) haimaanishi tucheze kama kina awilo, kunengua viuno kuigiza kuzini hadi watu wanaamshana hisia au kuifuata dancing ya kidunia hii.
5. UJAZO WA ROHO MTAKATIFU: Uzima wa kanisa ni Roho Mtakatifu, Yesu alisema siwezi kuwaacha peke yenu, nitawaachia msaidizi, huyo Roho atokaye kwa Baba, ndiye anayetutia kwenye kweli yote. huyu ndiye Roho anayetusaidia kuomba, analia Aba yaani Baba, kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, na yeye anaijua nia ya roho na hutusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukiomba kwa akili utaomba kwa kuomba mahitaji ya mwili bila hata kujua impact yake, unaomba gari kumbe hujui kama gari hiyo inaweza kukuua mwenyewe, ila ukiomba kwa Roho utaomba kwa yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu. ni furaha kubwa namna gani kuomba na kupata yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu, kuliko yale yaliyo mapenzi yetu sisi wanadamu! hivyo, HAMASISHENI WATU WENU WAJAZWE ROHO, hapo ndipo mtakuwa na kanisa. bila Roho mtakatifu hata maombi yatakuwa mzigo, kutoa sadaka na michango au kuinjilisti itakuwa mzigo, ila wakiwa na Roho Mtakatifu watafanay bila kuambiwa na ninyi, Roho atawaongoza tena maeneo sahihi. waambieni wafunge, wasome Neno, watafute uso wa Mungu na kuacha njia mbaya hadi pale watakapojazwa na kutembea na Roho Mtakatifu, hao ndio wakristo hai. wengine wote ni mizigo na mtakuwa mnaogoza watu ambao hamna uhakika kama wataenda mbinguni, kwasababu wale wenye Roho tu ndio watu wa Mungu. na Yesu atakapokuja kunyakua atanyakua wale wenye Roho tu, wasio na Roho wa Mungu hatawanyakua. WALAKINI AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA HUYO ROHO WA KRISTO, HUYO SIO WAKE. mkristo yeyote ambaye hana Roho Mtakatifu, huyo hana Mungu, na kuwepo kwa Roho hat akama wengi mnajifariji kwamba unaweza kuwa naye bila kunena, ila aliye naye anajijua anaye, na kunena ni ishara ya udhihirisho. ukienda kanisa ukaona mwezi wa kwanza, wapili hawahubiri na kuhamasisha ujazo wa Roho Mtakatifu, hapo kimbia, hakuna Mungu, kuna dini. msingi wa kwanza wa mpentecost ni ujazo wa Roho tena kunena kwa lugha kama kitabu cha matendo ya mitume. na ndilo agizo la Yesu.
6. SEMINA NA MAFUNDISHO; mnazidiwa na manabii na mitume wa uongo wanaouza mafuta kwasababu hamfundishi Neno, wekeni semina, fundisheni watu, na wakati unafundisha, usiende iviivi, jiandae kiroho ili ukiwa pale usihubiri wewe, bali Roho aongee kupitia wewe, hayo ndio mahubiri na mafundisho yanayookoa, elimu yenu ya chuo haiokoi, hata kama mmesoma theologia hadi PHD. ila tone moja tu la Roho wa Bwana linatosha kubadilisha Roho. Roho Mtakatifu ni mhuri, akikufikia tu ni kama amekupiga mhuri, kama ni wimbo au Neno hilo utalikumbuka. au kama ndoto kama ni ya Kimungu utaona ni kama umepigwa mhuri, hautaisahau. maishani mwangu kuna ndogo na maono niliyaona miaka 20 iliyopita, ila hadi sasa nakumbuka kila kitu ni kama nimeota au kuona jana. huyo ndiye Mungu. na huwezi kusema labda havikutoka kwa Mungu, Nooo, msidanganyike, labda kama haujawahi kukutana na Mungu au kusikia sauti yake, Yesu alisema Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nao wanifuata. akija mwizi wakiita kondoo wanajua huyo sio mchungaji, ila akija mchungaji akiita sauti moja tu unajua huyo ndiye. ndivyo ilivyo, Mungu anajulikana kwetu kama tumejitoa kwake.
nimetoa haya machache, wengine watasema kwanini nimetolea hapa naaibisha kanisa, hapana, nimeona bora niweke hapa ili ifikie wachungaji wengi, kwasababu wapo humu. Mungu aliokoe kanisa lake.