Wachina wampuuza Magufuli ujenzi barabara ya Mbagala

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Wachina wampuuza Magufuli ujenzi barabara ya Mbagala Wednesday, 18 May 2011 20:12

anatoasomomagufuli.jpg

Dk John Magufuli

Ummy Muya
Mwananchi

KAMPUNI ya Chico ambayo ilishinda zabuni ya kujenga barabara ya Zakhiem hadi Tanita, imeshindwa kutekeleza agizo la Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, kutaka iwe imeanza kazi ndani ya siku kumi.

Mei 7, mwaka huu, Waziri Magufuli alitoa siku kumi kwa kampuni hiyo iwe imeanza kazi, vinginevyo serikali ingefuta zabuni hiyo na mkandarasi kulazimika kulipa faini na kufutiwa kibali cha kufanya kazi nchini.

Hata hivyo, hadi jana kampuni hiyo ilikuwa haijatekeleza agizo hilo wala kuweka vyombo eneo la kazi.
Taarifa zilizopatikana jana zilieleza kuwa, Dk Magufuli alimwandikia barua mkandarasi huyo kumjulisha kusudio la serikali kusitisha mkataba wake kutokana na uzembe. Kwa mujibu wa taarifa hizo, baada ya hapo wizara inaandaa taratibu za kisheria kushughulikia suala hilo, baada ya mhandisi huyo kushindwa kutekeleza agizo la waziri.

Msemaji wa Wizara wa Ujenzi, Martin Ntemo, alisema alisema mkandarasi huyo hajaanza kazi, licha ya waziri kumtaka kufanya hivyo ndani ya siku kumi. “Mkataba ni kama mahakama, kwa hiyo mkandarasi huyo siyo kwamba anaogopwa, bali tayari taratibu za kimkataba zitachukuliwa kama alivyosema waziri,” alisema Ntemo. Ntemo alikiri mkandarasi huyo kutopeleka vifaa eneo la kazi, licha ya kupewa karipio kali na waziri Magufuli.

”Ameandikiwa barua kwa mujibu wa sheria kwa sababu suala la mkataba lilifanyika kisheria, hata hili la kusitisha mkataba wake kwa kushindwa kufanya kazi kwa wakati na kutozingatia karipio alilopewa pia linafanywa kisheria,” alisema. Mei 7, mwaka huu, akiwa kwenye ziara ya kukagua barabara, Waziri Magufuli alimwagiza mkandarasi huyo ambaye tayari amelipwa Sh1.27 bilioni kati ya Sh5 bilioni za kujenga barabara yenye umbali wa kilomita 1.5.

Dk Magufuli alishangaa kuona ujenzi haujaanza miezi saba tangu mkandarasi huyo alipwe fedha hiyo. Mkataba huo ulisaniwa Novemba mwaka jana.
 
Huyu waziri ni makini sana katika kazi zake. Naona tumpe nchi au siyo masela

fisadi tu, hatujasahau alivyouza nyumba za serilali kama njugu hadi kwa dada zake na kuchomea wajasirimali nyavu huku wazalishaji na wafanyabiashara wakisamehewa kodi ili watajirike zaidi. kifupi huyu ni waziri wa kucheza na media tu, hana lolote, aende huko na magamba yake
 
Kikwete na Pinda hawachelewi kumkaripia hazadhari, bila ubabe na kufuata sheria hakuna nchi yoyote inayoweza kuendelea duniani mnamremba mremba mkandarasi kumbe iyo pesa ataitumia kweny biashara zake , zikifa si itakula kwetu
 
Alipwa November mwaka jana? hatari sana mhmm haya bwana pangu pa kavu
 
kweli hana jipya kazi yake ni kucheza na media tu alishindwa kumpa notice badala ya kutoa siku 10 kwenye media?
fisadi tu, hatujasahau alivyouza nyumba za serilali kama njugu hadi kwa dada zake na kuchomea wajasirimali nyavu huku wazalishaji na wafanyabiashara wakisamehewa kodi ili watajirike zaidi. kifupi huyu ni waziri wa kucheza na media tu, hana lolote, aende huko na magamba yake
 
Hivi ninyi mu watu gani msiokuwa na shukurani au kusifu pale mtu alipofanya vizuri? nani ni msafi sasa? wewe ama? Hata sisi wananchi ni mafisadi tu hatutumii akili, tungekuwa na akili tusingechangua upupu.

Acha tuburuzwe tutie akili.
 
Duh..sasa ERB wamemsimamisha Eng. Wa Baria na wa Nimeta kwa gharama 4.5km kwa 9 biln. Kumbe 2011 kuna barabara ya 1.5 kwa 5 bilioni?
 
Back
Top Bottom