Wachina Wakamatwa Wakichimba Kokoto Kwa Kikwete, Msoga..!!!!!

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Wachina wakamatwa wakichimba kokoto Msoga
Thursday, 19 July 2012 18:46


Nora Damian
IDARA ya Uhamiaji, mkoani Pwani, imewakamata raia 12 wa China,saba miongoni mwao wakiwa hawana vibali vya kuishi nchini.

Raia hao walikuwa wakifanya kazi katika Kampuni ya Tansino, inayojishughulisha na uchimbaji wa kokoto katika Kijiji cha Kinzagu, Kata ya Lugoba, Chalinze.

Akizungumzia tukio hilo jana, Ofisa Emmanuel Bujumuro, alisema raia hao walikamatwa katika msako uliofanyika katika eneo la uchimbaji wa madini hayo.

Alisema baada ya kuwatia mbaroni raia hao wa kigeni, walihojiwa na kubaini kuwa saba miongoni mwao walikuwa hawana vibali vinavyowaruhusu kufanyakazi nchini.

Kwa mujibu wa afisa huyo, operesheni hiyo ilifanywa kwa ushirikiana na viongozi wa Tarafa ya Msoga na vyombo vya dola, baada ya taarifa kuwa wageni hao walikuwa wanachimba kokoto huku wakijificha kwenye makontena.

Alisema katika msako huo walibaini kuwa ni wageni watatu tu, waliokuwa na vibali.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kinzagu, William Makumu, alisema tangu aingie madarakani mwaka 2009 hajawahi kupata ushirikiano kutoka kwa mwekezaji huyo.

Ofisa Tarafa ya Msoga, Mbwana Madeni, amesimamisha mara moja shughuli za uchimbaji wa kokoto katika eneo hilo."Siwazuii kufanya kazi lakini lazima wafuate taratibu na kwa sasa nasimamisha shughuli zao hadi taratibu zitakapofuatwa,"alisema Source Wachina wakamatwa wakichimba kokoto Msoga
 
Mods hii sio habari ya siasa,ondoa peleka jukwaa la habari mchanganyiko
 
Back
Top Bottom