Wachambuzi wa soka kama edo kumwembe ni hatari kwa soka letu....................

Kwa hapa bongo mtu nineyemuona anajua mpira kiasi ni Adolf Richard kwani anaweza kuelezea technically jinzi mpira unavyochezwa.
 
Wewee!!!!!! Edo ni mchambuzi mzuri sana. Jichunguze inawezekana wewe ndo unayeleta ushabiki!
 
Katika watu ambao walikuwa hawajui kitu Mzirai ni mmoja wapo tena afadhali hata ya edo, mzirai alikuwa ni mtu wa majungu na fitna tu ya kuwahonga kina ngasa na mgosi wasifunge kwenye timu ya taifa ili maximo aonekane mbaya

If he (RIP) real was doing that for sure I am so sad for Tanzania football otherwise his contribution to our soccer was such an erasable memory!
 
Nijuavyo mimi uchambuzi wa kitu sio lazima usome darasani,inawezekana edo anasoma kwenye mitandao na magazeti ya nje,na kuwa mchambuzi sio lazima ujue kila kitu.Ricky abdallah ameitwa DR.sio kwa kucheza wala kukaa darasani kusomea mpira ni mapenzi na uelewa wake wa soka.Mziray (late)huyu hajawahi kucheza mpira ni mtaaluma wa elimu ya viungo na hakuwahi kuwa mchambuzi wa soka bali mwalimu wa soka na vituo vya tv vilitumia elimu yake ya ukocha.Superspoti wachambuzi wao sio wasomi wa darasani ni wachezaji wa zamani.Labda kama unalililojificha.

Bold ya kwanza
Na ndo kitu ambacho jamaa analalamikia,

Bold ya Pili
Na ndo maana wachambuzi wa SS unafaidi wanapokuwa wanafanya analysis, coz wenzetu Kucheza mpira ni taaluma na wanakaaga darasani.

Jose Morinho Hajawah kucheza mpira ila unaona impact ya elimu aliyoipata

Funguka taaluma ni muhimu sana kwenye kila kitu kitu ambacho waafrica walowengi hawakikubali sana,

Utasikia Ninakipaaaji mimi!

Talent without education islike toilet without a hole!
Asnte
 
Tena Shafii Dauda ndo hajui kitu kabisaaaaaaaaaaaaaaa. Yani yeye anajua historia tu ya mpira lakini si mpira unavyochezwa

Unajua watanzania tunapenda kutetea ujinga,

Safi sana. Nimewasikiliza sana, wao wanadhani kujua historia ya timu au wachezaji ndo kila kitu kwenye analysis!

Worokoso!!!!!!
 
Hawa wanojiita wachambuzi wa soka wa bongo akiwepo edo wanaboa bado wanapotumia mitazamo ya kizamani katika kuchambua soka.Siku zote soka haliko general.Wao wanachambua soka kwa ujumla wake lakini hawawezi kuchambua soka kimfumo.Kifupi wanapenda kutumia hisia binafsi badala ya kufahamu mifumo ya timu ikoje na wanachezaje.ukitaka kuliona hili wasikilize mtazamo wao wanapoichambua timu iliyofungwa utagundua wanasema kitu kimoja na zaidi kwa hisia binafsi.Mchambuzi halisi kama wenzetu wa ng'ambo (na mimi) wanazisoma kwanza mifumo ya timu husika ili aki komenti akomenti kulingana na falsafa inayotumiwa na timu husika.
Sio ajabu kukuta mchambuzi anailaumu timu inayotumia falsafa ya kaunta attack kuwa haijaposesi mpira kwa asilimia kubwa!!!hiyo ndio falsafa yao wamejipangia hivyo.Hata edo hili linamsumbua,aongeze bidii hapo na ajitoe ktk kutumia hisia binafsi
 
Hao wooooote mliowataja wana afadhali, kulikuwa na jamaa mmoja akiitwa Hussein Sapi...............kichefuchefuuuuuu!!!
 
hawa wanojiita wachambuzi wa soka wa bongo akiwepo edo wanaboa bado wanapotumia mitazamo ya kizamani katika kuchambua soka.siku zote soka haliko general.wao wanachambua soka kwa ujumla wake lakini hawawezi kuchambua soka kimfumo.kifupi wanapenda kutumia hisia binafsi badala ya kufahamu mifumo ya timu ikoje na wanachezaje.ukitaka kuliona hili wasikilize mtazamo wao wanapoichambua timu iliyofungwa utagundua wanasema kitu kimoja na zaidi kwa hisia binafsi.mchambuzi halisi kama wenzetu wa ng'ambo (na mimi) wanazisoma kwanza mifumo ya timu husika ili aki komenti akomenti kulingana na falsafa inayotumiwa na timu husika.
Sio ajabu kukuta mchambuzi anailaumu timu inayotumia falsafa ya kaunta attack kuwa haijaposesi mpira kwa asilimia kubwa!!!hiyo ndio falsafa yao wamejipangia hivyo.hata edo hili linamsumbua,aongeze bidii hapo na ajitoe ktk kutumia hisia binafsi

wakuu mbona mechi ya simba alichambua vizuri, kwa tanzania yeye ni namba moja.
 
Ukitaka kuelewana na Watz wasifie hata kama hawawezi. Ndo maana mambo ya Simba na YAnga nilishayaacha kitambo. Timu moja ikifungwa eti mgogoro unaanza. Huu si upuuzi? Mpira wa magazetini na vijiwe vya kahawa. Ah, bora nizungumzie habari za sayansi, hakuna ubishi, ni hoja tu.
 
Unajua watanzania tunapenda kutetea ujinga,

Safi sana. Nimewasikiliza sana, wao wanadhani kujua historia ya timu au wachezaji ndo kila kitu kwenye analysis!

Worokoso!!!!!!

Umesema jambo moja muhimu sana. Wengi wa wachambuzi wetu wanapenda sana kukariri matukio na historia za vilabu na wachezaji wa Ulaya. Unaona kabisa jinsi mtu anavyokuwa na raha amavyodadavua historia ya mchezaji ama klabu fulani ya Ulaya, raha ambayo inakosekana pale mchambuzi huyo anapoelezea suala la hapa nyumbani. Uchambuzi wa soka ni zaidi ya kukariri historia za vilabu na wachezaji wa Ulaya, jamani!

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom