Wabunge wetu nao watajwa katika ubadhirifu wa pesa zetu

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Wakuu,
Tangu jana nimekua nikiisoma ripoti ya Serikali Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2010/2011 yenye kurasa 191. Nilipofika ukarasa wa 90 nikashtuka kuona baadhi ya wabunge wetu wametajwa kuchukua pesa za Perdiem kwa ajili ya vikao vya Bungeni mjini Dodoma wakati hawakuwepo Dodoma. Sehemu ya ripoti inasomeka hivi:

Vote 42: National Assembly
Allowances amounting to Shs.6,960,000 were paid to Members of Parliament as per diem during the Parliamentary sessions while they were not in Dodoma and Shs.20,915,126 were paid to various officers and MPs contrary to Standing Orders and staff circular.

Sasa mimi najiuliza kama ripoti imepelekwa kwa Wabunge ili watoe hukumu wakati baadhi yao wanatumiwa ndani ya ripoti. Je tutarajie nini? Nafananisha kesi hii na ule msemo wa kesi ya Ngedere unampelekea Nyani.
 
bunge kama taasisi haihusiki na ubadhirifu huo hivyo wabunge wanaweza kabisa kuwawajibisha wenzao waliohusika.
 
bunge kama taasisi haihusiki na ubadhirifu huo hivyo wabunge wanaweza kabisa kuwawajibisha wenzao waliohusika.

Sawa nakubaliana na wewe lakini ni lazima wakati ripoti hiyo inajadiliwa watumiwa watoke nje ya Bunge maana Bunge halitakuwa la Maana kuwawajibisha wenzao waliohusika wakati wahusika wameshiriki katika Kikao cha Maamuzi ya kuwawajibisha.
 
Wakuu,
Tangu jana nimekua nikiisoma ripoti ya Serikali Kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha 2010/2011 yenye kurasa 191. Nilipofika ukarasa wa 90 nikashtuka kuona baadhi ya wabunge wetu wametajwa kuchukua pesa za Perdiem kwa ajili ya vikao vya Bungeni mjini Dodoma wakati hawakuwepo Dodoma. Sehemu ya ripoti inasomeka hivi:

Sasa mimi najiuliza kama ripoti imepelekwa kwa Wabunge ili watoe hukumu wakati baadhi yao wanatumiwa ndani ya ripoti. Je tutarajie nini? Nafananisha kesi hii na ule msemo wa kesi ya Ngedere unampelekea Nyani.

Natamani majina na vyama wanavyotoka wabunge husika yawekwe bayana na kisha tushinikize wajiuzuru kwa kutokuwa waaminifukwa umma.
 
Inasikitisha sana jamaa wanalipwa kwa kusinzia na kupiga makofi bungeni.
 
Natamani majina na vyama wanavyotoka wabunge husika yawekwe bayana na kisha tushinikize wajiuzuru kwa kutokuwa waaminifukwa umma.

Na kama kungekuwa na wagombea binafsi?????
Kwenye ukweli na tuujadili bila itikadi ya vyama. Tusipokuwa makini hii dhambi itakuja kutula kama udini na ukabila.......ushaambiwa wamekula posho na hawakuwepo wewe unaleta hoja ya chama mtu anachotokea isaidie nini wakati mwivi ni mwivi tu hata kama hana chama

Mytake; Yangewekwa majina yao hao wadaiwa wetu ili tuwajue at a personal level na sio kwa vyama vyao
 
Natamani majina na vyama wanavyotoka wabunge husika yawekwe bayana na kisha tushinikize wajiuzuru kwa kutokuwa waaminifukwa umma.

Usishangae siku majina yakitajwa ukaambiwa Lusinde a.k.a chizi wa kuzaliwa yumo!
 
Yamepita mengi yakiwepo Richmond, EPA, RADAR, NDEGE YA RAIS,KUUZA TEMBO NA TWIGA UARABUNI YA MPONDA NA NKYA NA HILI LINAPITA TUUU!!SISI TUANDIKEANDIKE HAPA ,MASAA YAENDA TULALE!!
 
Nadhani watakuwa wa magamba, kwani bibi kiroboto alikuwa anawabania wabunge wa CDM wasisaini ili wasilipwe
 
Sina utaalamu wa sheria, lakini nakumbuka sheria mama inatutaka watanzania wote tulinde rasilimali za nchi hii, waqnasheria wetu si mutusaidie kuwashtaki hawa majamaa? Hii ni aibu yetu sote!
 
Back
Top Bottom