Wabunge waulipua uongozi wa ATC

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Wabunge waulipua uongozi wa ATC

Thursday, 24 March 2011 20:06 newsroom



*Wadai unanuka rushwa, siasa
* Ina ndege moja, watumishi 155
NA KHADIJA MUSSA
KUTOKANA na kusuasua kwa uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), wabunge wamelishukia shirika hilo wakisema limejaa rushwa na maamuzi ya kisiasa. Wamesema shirika hilo pia kwa sasa halina shughuli ya kibiashara inayofanyika kutokana na kuwa na ndege moja inayotoa huduma, huku likiwa na wafanyakazi 155. Kauli hizo zilitolewa jana, wakati kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokutana na uongozi wa wizara za Uchukuzi na Ujenzi. Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele (CCM), alisema uongozi wa ATC unanuka rushwa na kwamba, anashindwa kuelewa zilikopelekwa fedha zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kulipia madeni ya ndani, ili shirika liweze kujiendesha.
air.jpg

"Bodi na menejimenti ya ATC sijui zinafanya kazi gani, ni bora zikavunjwa na watu wakaacha kufanya kazi kwa mazoea. Wanalitia hasara shirika, kwa nini tunawekeza fedha nyingi kwenye viwanja vya ndege wakati hatuna hata ndege moja, viongozi wa ATC ni wala rushwa na hawawezi kufanya lolote," alidai.
Masele alisema menejimenti ya ATC ni tatizo kubwa, kwani inapatiwa fedha na inazitumia vibaya, huku hakuna hatua zinazochukuliwa licha ya jambo hilo kufahamika. Kwa mujibu wa Masele, iwapo viongozi wa bodi na menejimenti wataondolewa na kuwekwa wengine, hali inaweza kuwa nzuri na mabadiliko yataonekana. Naye mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Mohamed (CCM), alisema tatizo kubwa linaloyagharimu mashirika ya umma ni kuendeshwa kisiasa, hivyo alishauri viongozi kuwa makini na kutanguliza maslahi ya taifa mbele. Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Ruhwanya (CHADEMA), kwa upande wake alitaka kufahamu mikakati iliyowekwa na serikali katika kulifufua shirika hilo. Alitaka pia kufahamu zilikokwenda fedha za nauli zilizolipwa na abiria waliosafiri na ndege za shirika hilo.
Naye Lucy Owenya, Viti Maalumu (CHADEMA) alitaka kufahamu shirika hilo lina wafanyakazi wangapi na ndege ngapi. Akijubu maswali hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Injinia Omar Chambo, alisema shirika hilo lina hali mbaya, na kwamba, serikali haitawekeza tena, bali mkakati uliopo ni kufanya kazi kwa ubia. Injinia Chambo alisema shirika hilo lina ndege mbili, moja ikiwa ya kukodi. Hata hivyo, alisema kati ya hizo, moja ipo Afrika Kusini kwa matengenezo, ambapo dola za Marekani 700,000 (zaidi ya sh. bilioni moja) zinahitajika.
Alisema ATC ina wafanyakazi 155 na kuna mpango wa kuwapunguza. Kuhusu menejimenti na bodi alisema taratibu zinaangaliwa ili kuchukua hatua. Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Zainab Vullu, aliutaka uongozi wa wizara kutoa maelezo ya sh. milioni 40 zinazotumika kulipa pango la jengo.
Alisema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa, na kuhoji kwa nini hawana jengo, wakati pesa zinazokusanywa ni nyingi. Chambo alisema ATC haina fedha za kujenga ofisi.

Last Updated ( Thursday, 24 March 2011 20:31 )
 
Serikali yatua rasmi ‘zigo' la ATCL Send to a friend Thursday, 24 March 2011 21:23

Fidelis Butahe
SERIKALI imesema haiwezi kutoa fedha za kusaidia uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na badala yake, inatafuta mwekezaji wa kuliendesha shirika hilo.

Pia, imesema mkakati ulipo sasa ni kupunguza wafanyakazi 153 wa shirika hilo na kutafuta Dola 700,000 za Kimarekani kwa ajili ya kulipia matengenezo ndege moja iliyopelekwa Afrika Kusini. kwa matengenezo.

Msimamo huo ulitangazwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo, baada ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, kumtaka aeleze mikakati ya serikali katika ukusanyaji wa mapato na uboreshaji wa shirika hilo.
Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Zainab Vullu, pamoja na mambo mengine, ilisema moja ya sababu za kuzorota kwa shirika hilo ni Bodi na Menejimenti ya ATCL na kuitaka serikali iivunje bodi hiyo.

Akijibu hoja hiyo, Chambo alisema kwa sasa hali ya ATCL ni mbaya na kwamba hiyo inatokana na kuwa na ndege tatu, moja ikiwa ya kukodi.Kwa mujibu wa katibu mkuu, ni ndege mbili tu kati hizo ndizo zinazomilikiwa na shirika.
"Hivi sasa anatafutwa mbia wa kuendesha ATCL, ila serikali haiwezi kutoa tena fedha kwa ATCL, mkakati ulipo ni huo wa kutafuta mbia na kupunguza wafanyakazi," alisema Chambo,


Alisema serikali pia sasa iko katika mchakato wa kutazama utendaji kazi wa Menejimenti na Bodi ya ATCL na kwamba ikijiridhisha, itachukua hatua stahiki.

Mbali na ATCL wabunge hao pia walitaka kupata ufafanuzi kuhusu mkataba wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ambayo serikali ina hisa ya asilimia 49 wakati Kampuni ya Rites ya India, ikiwa na asilimia 51 ya hisa.

Akitoa ufafanuzi suala hilo, Chambo alisema serikali ipo katika hatua za mwisho za kununua hisa zote za Rites ili kampuni hiyo iongozwe na Watanzania na kwamba nguvu kubwa itawekwa katika uwekezaji ili kuboresha zaidi usafiri wa reli ya kati.

Pamoja na majibu hayo wajumbe,waliokenaka kutoridhishwa na Mbunge wa Nkasi, Ali Mohammed Kessy (CCM), aliwataka wabunge wenzake wasimbane Chambo kwa kuwa hivi sasa siasa zimeingilia utendaji wa serikali.

"Hapa makatibu wakuu mnawaonea bure, unajua siasa zimekuwa zikiwekwa mbele zaidi kuliko utendaji, kila kitu siasa tu, siasa tu, umefikia wakati wa kuweka fedha mbele siasa nyuma," alisema Kessy.
 
Tanzania nchi ya SIASA tu hakuna kufuata utaalam, leo mwanasiasa anaweza akaibuka na kitu cha ajabu na kikafuatwa kuliko Mtaalam aliyebobea katika fani hiyo akisema yeye hatasikilizwa. SIASA zimetumalizaaaaa
 
Maskini nchi yangu, wameua Mashirika yote kwa maslai yao, ipo siku nitaingia na mabaruti huko magogoni au dodoma tumalizane huu ni ujinga :embarassed2:
 
Back
Top Bottom