nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
*Wadai unanuka rushwa, siasa
KUTOKANA na kusuasua kwa uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), wabunge wamelishukia shirika hilo wakisema limejaa rushwa na maamuzi ya kisiasa. Wamesema shirika hilo pia kwa sasa halina shughuli ya kibiashara inayofanyika kutokana na kuwa na ndege moja inayotoa huduma, huku likiwa na wafanyakazi 155.
Kauli hizo zilitolewa jana, wakati kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokutana na uongozi wa wizara za Uchukuzi na Ujenzi. Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele (CCM), alisema uongozi wa ATC unanuka rushwa na kwamba, anashindwa kuelewa zilikopelekwa fedha zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kulipia madeni ya ndani, ili shirika liweze kujiendesha.
.
"Bodi na menejimenti ya ATC sijui zinafanya kazi gani, ni bora zikavunjwa na watu wakaacha kufanya kazi kwa mazoea. Wanalitia hasara shirika, kwa nini tunawekeza fedha nyingi kwenye viwanja vya ndege wakati hatuna hata ndege moja, viongozi wa ATC ni wala rushwa na hawawezi kufanya lolote," alidai.
Masele alisema menejimenti ya ATC ni tatizo kubwa, kwani inapatiwa fedha na inazitumia vibaya, huku hakuna hatua zinazochukuliwa licha ya jambo hilo kufahamika. Kwa mujibu wa Masele, iwapo viongozi wa bodi na menejimenti wataondolewa na kuwekwa wengine, hali inaweza kuwa nzuri na mabadiliko yataonekana.
Naye mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Mohamed (CCM), alisema tatizo kubwa linaloyagharimu mashirika ya umma ni kuendeshwa kisiasa, hivyo alishauri viongozi kuwa makini na kutanguliza maslahi ya taifa mbele. Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Ruhwanya (CHADEMA), kwa upande wake alitaka kufahamu mikakati iliyowekwa na serikali katika kulifufua shirika hilo. Alitaka pia kufahamu zilikokwenda fedha za nauli zilizolipwa na abiria waliosafiri na ndege za shirika hilo.
Naye Lucy Owenya, Viti Maalumu (CHADEMA) alitaka kufahamu shirika hilo lina wafanyakazi wangapi na ndege ngapi. Akijubu maswali hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Injinia Omar Chambo, alisema shirika hilo lina hali mbaya, na kwamba, serikali haitawekeza tena, bali mkakati uliopo ni kufanya kazi kwa ubia. Injinia Chambo alisema shirika hilo lina ndege mbili, moja ikiwa ya kukodi. Hata hivyo, alisema kati ya hizo, moja ipo Afrika Kusini kwa matengenezo, ambapo dola za Marekani 700,000 (zaidi ya sh. bilioni moja) zinahitajika.
Alisema ATC ina wafanyakazi 155 na kuna mpango wa kuwapunguza. Kuhusu menejimenti na bodi alisema taratibu zinaangaliwa ili kuchukua hatua. Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Zainab Vullu, aliutaka uongozi wa wizara kutoa maelezo ya sh. milioni 40 zinazotumika kulipa pango la jengo.
Alisema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa, na kuhoji kwa nini hawana jengo, wakati pesa zinazokusanywa ni nyingi. Chambo alisema ATC haina fedha za kujenga ofisi.