Wakiongozwa na SUS, (Sendeka, Umi na Serukamba).
Ni kusogeza siku mbele kwa kujadili mambo yasio na umuhimu na kuhailishailisha bunge pasipo umuhimu wowote leo ni siku ya 20 bado wanatunga kanuni mara seminar
TZ ni nchi ya pekee sana katika uso wa Dunia.
Umeonaee hawa wametumwa maalumu kwa kazi hiyo. Watanzania kuweni na huruma na kodi zenu basi. Ni kama wanacheza mchezo wa mduara wanazunguka wanarudi palepale, siku zinaenda tu. Wao wanapata chao shida yao iko wapi?
Wajube wa baraza la wawakilishi na wajumbe wengine (wasio wabunge) ndio wanaoongoza kwa kutojali muda, wakiongozwa na Kificho.
Wapo kitalii zaidi.
mimi nafanya mchakato wa kusaka uraia wa SOMALI uzalendo wa kujiita mtanzania umefikia kikomo.
Hapo ndipo utapojua Kuwa Wabunge wa Zanzibar ni wajanja sana wanajua jinsi ya kuvuna posho za Watanganyika huku posho zao kule Visiwani wavuna peke Yao tu hata katiba Yao walatunga peke Yao na posho walijilipa pesa hii inayotoka Tanganyika na Hakuna mbunge wa Tanganyika alishirikishwa kwenye katiba ya ZNZ na Mpaka sasa wanajiuliza watazitumia vipi katiba mbili yaani hii mpya inayokuja na ile ya kwao ambayo inatumika sasa .
mimi nafanya mchakato wa kusaka uraia wa SOMALI uzalendo wa kujiita mtanzania umefikia kikomo.
Dah! pole sana ila ilo chaguo lako bado tunakusihii baki hapa hapa manake bunge bongo halijawahi kuwa la lamaana kwa watanzania kutokana wanafanya mambo ya kawaida sana na Sasa tulidhani hili ndio lingekuwa tofauti lakini kuna najisi ile ile ikajumuishwa humu tena.
Achana na habari zao kabisa hata ukiona katika gazeti usisome TV amia citizen na supersport mpaka siku 70 zipite katiba Warioba alishatengeneza hivyo vichwa 600 havina input yeyote ya maana sana sana wataongeza koma na nukta tu.