Shaycas
JF-Expert Member
- Feb 13, 2009
- 906
- 110
Nakubaliana na wewe kidogo ZITO afadhari kwa mambo ya Kitaifa. Ni hata Zito ndugu yangu wapiga kura wake amewasahau kabisa. Hivi unajua wapiga kura wake wamelipwa hela kiduchu sana tena bila hata uthamini kufanyika kupisha ujenzi wa barabara kwenda manyovu.
Sijamsikia hata akinyenyua mdomo wake mh ZITO. Hajui kama sisi ndio tumempeleka bungeni. watu wameitwa tu kuchukua cheque benk hawajui hata zina shilingi, mh Zito kimya kabisa na niwapiga kura wake kabisaaa.
LAKINI MAMBO MENGINE ANAONGEA MNO TENA KWA POINT KABISA.
HEBU ANGALIA SWALA LA DOWNS, ANASEMA NCHI ITAKUWA GIZANI, HIVI SISI KIGOMA TUNA UMEME? HALIONI HILO, HILO SIYO GIZA?.
HAYA NDIO MATATIZO YA KUCHAGUA WENYEJI WA DSM, ANGEKUWA HAPA KIGOMA GIZA TOTORO TUNALO KILA SIKU HAPA.
LENGO SI KUMCHAFUA LAKINI KUNA HAJA YA KUTUTETEA NA SISI WAPIGA KULA WAKE
HIVI KWA JINSI ZITO ALIVYO MSEMAJI MZURI ANASHINDWA HATA KULISEMEA KWA NGUVU SWALA LA USAFIRI WA RELI KWELI?
USAFIRI KIGOMA UKIENDA DIRISHANI HUPATI TIKETI. KILA SIKU WANAKWAMBIA ZIMEISHA ILI WAZIRUSHE. DAR-KIGOMA DARAJA LA TATU BILA LAKI MOJA HUPATI. HIZO ZOTE NI KERO KWA WANAKIGOMA WANAHANGAIKA KWELI. SASA TUNAHITAJI WATU WATUSEMEE NA WAYAKEMEE HAYA. LABDA KWA KUWA WAKO JIJINI DAR BASI NDIO HIVYO TENA KIMYA TU.
ZITTO alifanya kampeni yake kisomi zaidi.alikuwa na CHECK LIST ya mambo ambayo angefanya kama akichuguliwa kuwa Mbunge.
Aliwagawia wananchi hiyo Check list na kuwaambia wawe wana 'tick' kila atakachofanya na kama haja fanya wa muulize.
Mpaka mwaka jana alipo kuwa Kigoma 99.5% ya aliyoahidi yalikuwa yamekamilika.
Ktk kipengele cha umeme na mawasiliano haikuwepo kwenye Check list yake na Hata alipo ulizwa kwenye kampeni kuhusu hayo alijibu kuwa yapo nche ya uwezo wake ila atajaribu kuona atafanyaje.
Kwa sasa anapigania DOWANS au umeme wa GRID ya TAIFA kwa sababu anajua hilo likitatuliwa hata KIGOMA itapata umeme wa jenereta kwa uhakika.
Kama mnakumbuka mwaka 2005/2006 Tanzania ilikumbwa na tatizo la umeme lakini KIGOMA hakukuwa na tatizo hilo kwa sababu KIGOMA haitumii GRID yaTAIFA na MAFUTA MENGI YALIELEKEZWA KIGOMA NA MTWARA ili kuendesha mitambo hiyo ambayo haipo ktk GRID YA TAIFA.
Mwisho,ZITTO HAWEZI KULETA MAENDELEO KIGOMA KUPITIA SERIKALI LABDA WAFADHILI BINAFSI KAMA ANAVYO FANYA DR.SLAA,HII NI KUTOKANA NA SERIKALI KUTAKA KUONESHA KUWA UPINZANI HAUWEZI KULETA MAENDELEO BALI CHAMA TAWALA.LAKINI NI JUKUMU LA SERIKALI KUHAKIKISHA MAENDELEO YA JAMII NZIMA.
MKITAKA KUJUA SERIKALI INAHUJUMU MAENDELEO YA WANANCHI ANGALIA KIPINDI HIKI AMBACHO NI ZAMU YA CCM KUONGOZA HALMASHAURI YA KIGOMA,WATAFANYA MAMBO MENGI MAZURI ILI IONEKANE KUWA CHADEMA WALISHINDWA.
Tayari wameshaanza na treni la haraka kutoka DSM-KGM.
KIGOMA MSIFE MOYO CCM INAKARIBIA KUFA KWANI SASA HAINA UELEKEO.KILA MTU ndani ya CCM,ANAFANYA NA KUONGEA MAMBO YAKE.