Wabunge wa CHADEMA waundiwa zengwe la kuwachafua na kuwadhalilisha

Juzi nilimsikia mar. baba wa Taifa akisema Upumbavu ni kipaji kama ilivyo ufupi, urefu n.k Sasa kuna watu humub JF wana vipaji vya upumbavu ukiwagunda wala usihangaike nao kabisa.

Du! Hivi urefu, ufupi ni vipaji??! Maneno ya Baba wa Taifa kweli?
 
Kama ni kweli kwamba TISS wanatumika ni hatari,kwa sababu nilijua kuwa sifa kuu ya kuwa mfanyakazi wa TISS ni

1.Kuwa ni mzalendo wa kweli ikiwezekana kuliko Raisi wa Nchi

2.Kuwa akili timamu na yenye upeo wa juu wa kuweza kuchanganua mambo.
3.Kuwa msiri hasa pale inapobidi kuwa msiri kwa masilahi ya Nchi.
4.Kutokuwa na tamaa ya kujilimbikizia mali

Ili nalo kama ni kweli baadhi yao bado wanaamini kwenye kulinda Serikali ambayo wao wanajua kuwa ndani yake kuna watu wanatishia usalama wa Taifa,hayo yatakuwa si maadili na uzalendo mwema wa Taifa letu.

Wasitumie msingi ya zamani ya Mwalimu ya kuwa chama ndio Nchi hakika uko kwao itakuwa si kulitendea haki Taifa,tunajua kwa zama zile za Mwalimu ilikuwa sawa lakini kwa sasa ni vyema na sahihi wao kusimamia TAIFA kwa asilimia mia kuliko kusimamia chama hata kama hawana uhakika wa vyama vya upinzani uenda vikatumika na maadui wa TAIFA lakini kuonyesha dhahili na kuacha sura ya baadhi ya watendaji wake kuonekana ni sehemu ya CCM ili ni hatari kwa TAIFA.Kwa kuwa UMMA unaweza kutengeneza maasi kama ya Libya na wao kuonekana kama ni wasaliti wa TAIFA kumbe tatizo ni kukumbatia kule ambako wao wanaona kuna uhakika wa TAIFA kuwa salama lakini kwa upeo wa umma wa kutambua hofu hizo zao haupo na kwa kuwa TAIFA ni Mali ya Umma Serikali inapokea madaraka toka kwa umma hivyo yaweza kudai Madaraka hayo wakati wowote bila kupiga hodi.

Ni vyema kuepuka makosa hayo kwa kujiandaa kama jeshi la Misri lilivyojichomoa mikononi mwa Hussein Mubarak baada ya kulitaka liingie mtaani kuwazuia waandamanaji.Kama TAIFA tujifunze mapema kabla ya matokeo,mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Zambia Mama Justice Irene alivyochomoa mipango ya Rais wa zamani wa Zambia Banda kwa kutaka kujitangazia ushindi.TISS waaanze kujenga mazingira ya utaifa waanze kujenga mifumo ambayo walioko Serikalini wajue kuwa TISS inasimamia maslahi ya vyama vyote vya SIASA na kuwa hawapo kumhujumu raia mwema ila watamwadhiibu raia yoyote mwenye kusudio au nia mbaya dhidi ya kulihujumu Taifa.

Kinachoendelea sasa kwenye vyombo vya habari vikiwa na picha hasi [Negative] juu ya chombo hicho ni mwanzo mbaya sana,ni vyema wakaanza kujirekebisha kuondoa tafsiri mbaya na kusimama upande wa wanaolitaki mema Taifa na si kusubili hatima ya umma utakapo fanya mageuzi ya lazima baada ya wao kushindwa kuzuia mabaya yaliyopelekea hasira ya umma kuchukua sheria mkononi kutaka mageuzi.Kuendelea kujidanganya kuwa umma wa Watanzania haujui ni kujitia kitanzi kibaya sana na ni kosa baya lisilostahiki msamaha na adhabu yake ni kali pale ambapo mlinda amani na uzima wa Taifa anapokuwa ndie chanzo cha uvunjifu wa uhai wa Taifa hukumu yake kwa umma wa Taifa ni kama yale ya hayati Sadam Hussein, na ndivyo itakavyotokea kwa Hussein Mubarak na pindi waaasi wa Libya watakapomkamata Rais wa Libya.

Haya mambo ni kanuni za kimaumbile ya tabia za wanadamu hasa wanapokuwa ni umma,ambao wamesimama kama Taifa,ni vyema kufuata ukweli wa sauti zao japo wengi hawajui mwelekeo lakini ni jukumu la wanausalama kutoa mwelekeo sahihi wa Taifa.Na sio sahihi kusubilia hukumu ya umma [mass] ambayo ina tabia ya kuhukumu kwa hasira kali pasipo tafakari kwa kuwa imekasilishwa na tukio au tendo liwe la zamani au la karibuni.

Mafno wa hukumu ya umma [mass] unaweza kuiona kupitia kibaka, mwizi au jamabzi aliyecholopoa pochi au simu ya mkononi ya raia,na pindi atakapokamatwa na umma hukumu yake uwa ni mbaya sana yenye kila aina ya unyama mkali utokanao na mchanganyiko wa mkusanyiko wa mauzi ya matendo mbalimbali yaliyojirimbikiza mioyoni mwa raia wengi kutokana na matendo ya vibaka na wezi kwenye majumba ya raia na kuwa kila wanapopiga kelele vyombo vya dola vinavyohusika kuwachukulia hatua wezi hao wamekuwa wakiona hakuna uchukuaji wowote wa sheria toka vyombo vya dola hivyo jamii hiyo ya umma uibuka na jibu la moja kwa moja kuamua kuchukua sheria mikononi.

Vivyo vivyo kwa kuwa Usalama wa Taifa kwa kuwa wao ndio wenye jukumu la kulinda usalama wa Taifa na kukabiliana na matendo na mambo ya watu wanaochafua jamii na Taifa na wenye kuwa na sifa mbaya za matendo ya kifisadi na rushwa kwenye mali ya umma.Kushindwa kwao kuwakabili na kuwadhibiti ndio kuunda makusanyiko ya makovu ndani ya mioyo ya wanajamii, amabyo ni sawa na yale ya kushindwa kwa vyombo ya vya dola kama polisi Kukabiliana na vibaka, wezi na majambzai wa mali ya umma mmoja mmmoja.
 
Kwaiyo bila hawa watatu chama kinakufa?
Sasa hivi ni wakati wa Chadema acheni mbinu zenu chafu....tutumie jukwaa la kisiasa kueneza sera siyo kuua watu hovyo kama mnavyofanya hoko Igunga.....
 
Ni Tundu Lissu, Godbless Lema & Freeman Mbowe (KUB).

Mkakati huo unafadhiliwa na watu wa usalama wa taifa na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na umma, ambavyo hivi karibuni vimekuwa vikifanya kazi ya CCM.

Imetakiwa itumike kila njia kurudisha harakati za CHADEMA nyuma kabla ya 2013 na huku wakisema kwamba ni lazima waiangamize CHADEMA kwa kuangamiza wabunge wake machachari. (Kikao kimeka Girrafe Hotel Dar)
Watakapokutana tena wapelekee salamu za pole. Waambie kuwa wataqnzania wa leo si wa jana, wanajua kuopembua pumba na mchele. Hizo mbinu za kuchafuana ziliwezekana wakati ule ule Kikwete alipokuwa anawania uraisi kwa udi na uvumba (yeye mwenyewe ameshakiri kuwa alitumia miaka kumi kujiandaa). Tuliona jinsi wapinzani wake walivyocvhafuliwa, hatukuelewa wakati ule lakini sasa tunajua. waje na mbinu nyingine mpya, si kurudia za zamani.
Lakini pia watambue kwua anayerusha matope kwa mwingine, baadhi ya matone yatarudi kwake nasi tutawatambua kwa matone hayo ya matope wanayorushia wenzao
 
nyie wanachadema vipi? mbona mnaishi kwa dhana, hofu, mashaka, woga na kutokujiamini? halafu ndio mnataka kuchukua nchi nyie? mtaweza kweli kudumisha amani, upenndo, umoja na utulivu wa watanzani uliopo sasa kama ccm walivyoulinda kwa miaka 50? acheni kujadili mambo yasiyo na ushahidi, mtakuwa hamna tofauti na wazee wa vijiweni!
Utakuwa umechanganyikiwa upendo huu mliuonyesha huko Igunga ndiyo mnajivunia....!?
 
Imetakiwa itumike kila njia kurudisha harakati za CHADEMA nyuma kabla ya 2013 na huku wakisema kwamba ni lazima waiangamize CHADEMA kwa kuangamiza wabunge wake machachari. (Kikao kimeka Girrafe Hotel Dar)

hahahhahhahhaaaaaaaa...........

Mbona mnanichekesha hivi jamani?

Baada ya kikao bil ilikuwa $ 6,750

Mnakumbuka kile kingine tulichoambiwa kilikaa Moven peak? bil ilikuwa $ 12,500

Nnachowapenda TISS ni kuwa baada ya kuona bado mda mfupi CHADEMA waingie madarakani, wamekuja na mkakati wa kuzikusanya ela na kuzitafuna mapema...

Kesho mtasikia kingine kilikaa New Africa hotel, kesho kutwa xxx hotel n.k.

Kuleni hizo pesa wakuu, bado kitambo kidogo hamtazipata tena...
 
Watashindana nasi, lakini hawatashinda

kwa maana tu kama upepo twa tokea kila direction na tunaonekana tufikapo sehemu na sehemu bila kujua tumeingia vipi na tunatoka vipi....I love the God of Israel who said ...surely there is no enchantment against Jacob neither is there any divination against Israel: according to this time (2015) it shall be said of Jacob and of Israel what has God wrought Num:23:23!

Alleluya acha ni preach sasa......Jaribu kujiuliza nani ni Jacob na nani ni Israel? Are they two different people? Jacob alikuwa tapeli na Israel alikuwa mtu mwenye haki mbele za Mungu; yaani mtu yule yule kwa personality tofauti. Lakini Mungu hapa anajiapiza kwakusema SURELY yaani kwa haki ya Mungu ambayo inazidi uhakika wowote duniani na mbinguni hakuna uchawi/usani/ubaya/ hila ama chochote juu ya huyu mtu tapeli Jacob wala hakuna uganga/mbinu chafu/mtego ama chochote kinachofanana na hicho kitakacho weza kumpata mwenye haki wangu Israel.

Kwa maana pana zaidi ni kuwa Mungu akikuchagua whether wewe ni tapeli ama ni mwenye haki mission yake lazima iwe accomplished na hakuna anayeweza kui abort.

...Aahaaa basi hao mumiani waelewe kuwa whether hao wabunge wanasifa stahiki ama hawa stahili mbele za Mungu; Mungu lazima awafikishe kwenye destiny yao kwani wanafanya mission ya kimungu kutetea wanyonge wa Tanzania....Watu waliofisadiwa kwa miaka zaidi takribani 30 tangu kuondoka madarakani kwa mtumishi wa Mungu Mwl J.K Nyerere ambaye kwa matunda yake tumemtambua kuwa hakika alikuwa mtumishi wa Mungu....Hatusemi kwa mdomo tu kwamba anacho chakuonyesha kuwa alikifanya bali kila mwenye macho alikiona na wengine bila yeye leo wasingekuwa hapo walipo. Lakini kwakukosa utu wamegeuza favour walioipata kuwanyonga wenzao na kunywa damu zao kwa tamaa ya mali za wizi na madaraka yasiyo na heshima!
 
Ni Tundu Lissu, Godbless Lema & Freeman Mbowe (KUB).

Mkakati huo unafadhiliwa na watu wa usalama wa taifa na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na umma, ambavyo hivi karibuni vimekuwa vikifanya kazi ya CCM.

Imetakiwa itumike kila njia kurudisha harakati za CHADEMA nyuma kabla ya 2013 na huku wakisema kwamba ni lazima waiangamize CHADEMA kwa kuangamiza wabunge wake machachari. (Kikao kimeka Girrafe Hotel Dar)

CHADEMA itajiangamiza yenyewe. Suala si kuwachafua WABUNGE wa CHADEMA, tatizo ni CHAMA CHENYEWE NI KICHAFU. Ni swala tu la wakati wa Usalama wa Taifa na VYombo vya habari kufungua mafaili yao yenye ajenda kibao za CHADEMA na kuyarusha hewani.

Hiki ni chama kinachoongozwa na kupata umaarufu kwa kutumia PROPAGANDA ZA UONGO. Kikitembea Tanzania nzima, katika taasisi za kibinafsi na za kidini, Makabila na kutumia uongo kama mtaji wao wa kushinda chaguzi tofauti.

Sasa hatima yao imefika mwaka 2013 ndio Stop. Tuna siku 1400 mpaka uchaguzi mkuu 2015, lakini tumeugawanya katika makundi makundi. Awamu ya kwanza inahitajika itoe matunda yake mwaka 2013, nayo itawalenga wabunge wao, Viongozi wa juu wa CHAMA na wafadhili wa kipesa. Awamu ya pili itajishughulisha sana na kitengo cha habari ikiwa pamoja na mitandao, TV, Radio na wapambe. Haya yote yatafanywa kwa kuzingatia sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania katika uenezaji wa habari (maadili ya uandishi n.k). Awamu ya tatu ni Siri na sitoieleza hapa.

Mkitaka kuepukana na hayo acheni PROPAGANDA ZA UONGO.
 
Wana Mageuzi....nilisema neno moja... narudia..Mungu akikuweka juu utabakia kuwa juu na kama ni mwanadamu amekuweka juu utashuka kabisaaa..Sasa imani yetu ni CDM Mungu amekiweka juu na si vinginevyo
 
a
CHADEMA itajiangamiza yenyewe. Suala si kuwachafua WABUNGE wa CHADEMA, tatizo ni CHAMA CHENYEWE NI KICHAFU. Ni swala tu la wakati wa Usalama wa Taifa na VYombo vya habari kufungua mafaili yao yenye ajenda kibao za CHADEMA na kuyarusha hewani.

Hiki ni chama kinachoongozwa na kupata umaarufu kwa kutumia PROPAGANDA ZA UONGO. Kikitembea Tanzania nzima, katika taasisi za kibinafsi na za kidini, Makabila na kutumia uongo kama mtaji wao wa kushinda chaguzi tofauti.

Sasa hatima yao imefika mwaka 2013 ndio Stop. Tuna siku 1400 mpaka uchaguzi mkuu 2015, lakini tumeugawanya katika makundi makundi. Awamu ya kwanza inahitajika itoe matunda yake mwaka 2013, nayo itawalenga wabunge wao, Viongozi wa juu wa CHAMA na wafadhili wa kipesa. Awamu ya pili itajishughulisha sana na kitengo cha habari ikiwa pamoja na mitandao, TV, Radio na wapambe. Haya yote yatafanywa kwa kuzingatia sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania katika uenezaji wa habari (maadili ya uandishi n.k). Awamu ya tatu ni Siri na sitoieleza hapa.

Mkitaka kuepukana na hayo acheni PROPAGANDA ZA UONGO.

Samahani dada sijui wewe unaamini wapi lakini imani yangu inasema kuwa wakati wa mfalme wa Babel aliyekuwa anaitwa Nebuchadnezzar alitengeneza sanamu yake isujudiwe na kuabudiwa katika ufalme mzima wa Babel wakati huo....Walikwepo watatu waliokataa kufanya hivyo wakijua haimpasi mwanadamu kuabudu sanamu ila Mungu aliye hai pekee na wakawa tayari kutokufanya hivyo kwa garama ya hata ikibidi wao kupoteza kwanza vyeo vyao pili maisha yao lakini wabai katika imani yao.

To cut short the story lakini kwa detail unaweza msoma Daniel kwenye Biblia sura yake ya 3. Yule mfalme akatengneza tanuru la moto litakalo wateketeza hao maadui wake wakisiasa katika ufalme wake. Kuhakikisha kuwa wanatambua nguvu na uwezo wake wakifalme akaamuru moto huo uchochewe makali yake mara saba kama umesoma science kidogo basi ufikie rangi ya blue. Matokeo yake wale watatu Meshack Abednego na Shadrack walikuwa wakionyeshwa kila hatua ya moto kuchochewa na huku rangi ikibadilika from red yello yaani rangi saba kama upinde wa mvua kila mara wakiulizwa kama wako tayari kugairi maamuzi yao...Walimwambia mfalme maneno haya....'Tunahakika Mungu wetu atatuokoa katika mikono yako na hata kama ikatokea akaacha kutuokoa basi tuko tayari kuangamia kuliko kuinamia sanamu lako'

Kwako wewe dada CDM mimi nikiwa mwanachama tunasema hivi uwongo wetu tulioueneza kama unavyodai (kupinga ufisadi wa chama na serikali yenu kuendelea kututawala) hatutaacha kuusambaza nakuungana nanyi kuwafisadi wana nchi kwani tunajua kwa hakika Mungu atatuokoa na mikono yenu miovu nahata kama hatatuokoa ni bora tufe tukiwa tunasimama kuliko tukiwa tunakisujudia chama chenu.

Matokeo ya ukiri wa hao jamaa siyo agenda ya leo lakini unaweza kujisomea mwenyewe hicho kitabu cha Daniel....
 
Ni Tundu Lissu, Godbless Lema & Freeman Mbowe (KUB).

Mkakati huo unafadhiliwa na watu wa usalama wa taifa na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na umma, ambavyo hivi karibuni vimekuwa vikifanya kazi ya CCM.

Imetakiwa itumike kila njia kurudisha harakati za CHADEMA nyuma kabla ya 2013 na huku wakisema kwamba ni lazima waiangamize CHADEMA kwa kuangamiza wabunge wake machachari. (Kikao kimeka Girrafe Hotel Dar)

Watu hawa walidiriki juzi kuziblock email za viongozi kadhaa wa chama, kwani kila wakijaribu kutaka kuingia kwenye email zao walishindwa kwa muda wa siku mbili..... ila hatutavunjika moyo wala kurudi nyuma katika harakati tulizo zianzisha.
 
Back
Top Bottom