Wabunge wa CCM hatarini kukwamisha Mswada wa marekebisho ya sheria ya Katiba Mpya

Acha waje na ujinga wao.adhabu watakayopata awa wabunge wa ccm hawataisahau.nchi ikiingia kwenye machafuko watu watatarget vitu vyao kwa kuwa ndio matajiri na ndugu zao. Nalisema ili nikiona yaliyoko mbele yetu.machafuko yakiwa kama ilivyokuwa kenya,hapa itakuwa mbaya zaid kwani watz watachanganya na ujinga iwe genocide mbaya.kenya walikuwa weled lakin waliuana tu sembuse sisi wenye elimu kiduchu?
 
Jamani tuwe wakweli, hata kama wabunge wa CCM watafanya kama wanavyopanga, hakuna mtu yeyote atakayeingia barabarani wala nini. Hizi story za sijui watakiona cha mtema kuni, mara watapambana na nguvu ya umma ni porojo tu za humu JF; hakuna mtu yeyote mwenye ujasiri wa kuingia barabarani, tusidanganyane.
Hizi faraja za kujilinganisha na Misri, Tunisia na Libya ni blah blah tu, hakuna lolote litakalofanyika hapa Tanzania.
 
Sitashangaa wabunge wa CCM wakifanya hivyo maana wao huwa hawaangalii maslahi ya Taifa isipokuwa maslahi yao. Kosa alilofanya JK ni kuusaini ule mswada. Kama angekuwa ni mwerevu angekubaliana na ushauri wa CHADEMA wa kutokusaini, na kisha angeurudisha bungeni kuwa hakubaliani nao, na wabunge wangelazimika kuujadili upya. Kama wangeng'ang'ania, alikuwa na uwezo wa kuvunja bunge na kurudi kwenye uchaguzi. Wabunge wengi wasingekubali kufika huko kwa sababu ya hofu ya kutokuchaguliwa tena.
Lakini wakiyagomea mapendekezo ya marekebisho yaliyoletwa na serikali yao, ambayo kimsingi ni ya Rais, watazidi kujimaliza, madhara yake yatakuwa makubwa zaidi kuliko aibu wanayoihofia. Hata hivyo sioni kama wabunge wa CCM wana heshima yeyote mbele ya jamii kiasi cha kufikiria kuwa wamevunjiwa heshima (heshima ambayo tayari hawana).

nimekupata, wabunge wa ccm hawana heshima kwa jamii, wasihofu kuipoteza. angalau wafikirie kuitafuta.
 
Tanzania siasa uchwara Rosta Azizi Uko sahihi nakupa Big up kubwa siasa TZ haina mbele wala nyuma mswada wa katiba TZ inaenda inarudi katiba uchwara Bora wangerudi wazungu Watubige viboko kama mang'ombe.:canada:
 
source ni wewe toa upupu wako kajipange urudi tena

Wewe ndio unaandika upupu mtoa mada kasema wazi hizi ni tetesi na ndio maana kaleta hapa member tujadili.Sasa wewe ulitaka afanyeje? Au inawezekana wewe ni miongoni mwa hao wabunge wapuuzi ambao mnapanga huo uhuni wenu na hamkutaka hii habari ivuje.Shame on you magamba
 
Labda kosa la jk ni kutowashirikisha wabunge wake kwenye mamuzi aliyoafikiana na cdm. Lakini kama kitu kitu ccm wangeshangilia ni hayo makubaliano. Nasema washangilie kwakuwa hakuna chochote cha maana ambacho cdm wamefanikiwa kubadilisha. Yani ni afadhali cuf walikuwa wakiingia kwenye dialogue na ccm wanatoka na kitu kuliko cdm. Aibu tupu.
 
Labda kosa la jk ni kutowashirikisha wabunge wake kwenye mamuzi aliyoafikiana na cdm. Lakini kama kitu kitu ccm wangeshangilia ni hayo makubaliano. Nasema washangilie kwakuwa hakuna chochote cha maana ambacho cdm wamefanikiwa kubadilisha. Yani ni afadhali cuf walikuwa wakiingia kwenye dialogue na ccm wanatoka na kitu kuliko cdm. Aibu tupu.
Jaribu kufafanua cuf walitoka na nn? na ni hoja ngapi za CHADEMA zilizokataliwa? Je marekebisho ya sheria yameletwa na nani?

 
WanaJF ni kweli habari yenyewe ipo kwenye gazeti la Tanzania daima na Mtanzania
 
Inahitaji uelewa mdogo sana na wala si nguvu kubwa kujua kuwa wabunge wa ccm hawapo kwa maslahi ya taifa ila yao binafsi kwa mgongo wa mitandao yao. Mbaya zaidi wamejisahau na kujiona ni miungu watu. Najua mwisho wao utakuwa mbaya sana.
 
Kwenye RFA, kipindi cha Magazeti, imeelezwa kwamba katika kikao cha jana usiku cha wabunge wa CCM, kulijadiliwa mambo matatu: Mswada wa marekebisho ya sheria ya uundwaji katiba mpya ya JMT, mgogoro wa madaktari na ukosefu wa maadili uliooneshwa na mbunge Dr. Kigwangala.

Katika mswada wa marekebisho ya sheria ya uundwaji katiba mpya, wabunge wa CCM wameupinga, na kutamka kuwa kama utapelekwa bungeni, wataususia na kutoka nje.

Kwenye suala la mgomo wa madaktari, wamependekeza kuwa Waziri wa Afya na watendaji wake wakuu waachie ngazi.

Kwenye suala la Dr. Kigwangala, lipelekwe kwenye kamati ya maadili ya CCM.

Mambo ya Kujiuliza:
Je, kama wabunge wa CCM wametoa tishio hilo, serikali itaupeleka mswada huo bungeni? Kama serikali itaupeleka mswada huo bungeni, na wabunge wa CCM wakatoka nje kama walivyotishia, wabunge wa CHADEMA na NCCR, wao pekee yao, watakuwa na uwezo kisheria wa kuupitisha bila ya kuwepo wabunge wa CCM ambao ni wengi maradufu?
Pamoja na tishio la wabunge wake, endapo JK atasimamia kutaka kuupeleka mswada huo bungeni, itakuwa ni mwanzo wa JK kujipatia umaarufu kwa Watanzania? JK akiogopa kuupeleka mswada wa marekebisho bungeni kwa kuwaogopa wabunge wake na CCM, Watanzania wafanye nini ili kuhakikisha wanapata wanachokitaka?

Kwenye suala la mgomo wa madaktari, kitendo cha wabunge wa CCM kuungana na madaktari kutaka waziri wa afya na watendaji wengine wa Wizara ya Afya, waachie ngazi, na kitendo cha wabunge wa CCM kukwamisha miswada miwili iliyoletwa na serikali yao, ni namna moja ya kumkomoa JK na serikali yake?
 
Watoke nje muswada ujadiliwe na wabunge wa cdm na nccr, naona itapendeza manake hawa zzm hawana cha maana cha kuongezea make walishapitisha madudu. Labda kisheria sijui kama itawezekana na spika atakubali kuendesha kikao na maginius wa cdm patachimbika.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Dr Kingwangwala anapelekwa mbele ya kamati ya maadili ya ccm kwa lipi? Kwa kukataa posho? Kama jibu ndiyo kwa nini wasimpeleke January Makamba kwenye hiyo kamati ya maadili? Why Dr Kingwangwala na sio Makamba? wanaogopa nini?

Pili kama hoja ni posho wabunge wa ccm wamesoma na kama wamesoma wameelewa kuuelewa mpango wa maendeleo wa taifa 2011-2016? maana mpango unasema wazi kuwa posho zifutwe. Hawa wabunge walikuwepo Dodoma wakati wa uzinduzi na kupiga makofi mengi kila alipokuwa anaongea rais. Sasa wanaleta tabia zao za kinyonga? wananchi tumechoshwa na watu wanapita kila kona kuahidi honey & milk lakini wakipata kura wanafanya tofauti.

Kwenye muswada wa katiba. As it is, muswada na sasa sheria ya kutunga katiba mpya ni matusi kwa watanzania. Hauendani hata kidogo na matakwa ya watanzania wengi. Sasa, wabunge wa ccm waamue moja, ama waumiliki huu mchakato wote wa katiba na hivyo kupata katiba yao au wafanye marekebisho yanayokidhi matwaka ya wananchi. And this time around hawatakutana na watu 48 tu walioko bungeni, huku mtaani hakutakalika.

Mwisho, tumechoka kuwa viongozi na wasioweza kufikiria zaidi ya centimeter 5 mbele. Nchi nyingine za Afrika Mashariki zinatupita na hawana hata robo ya rasilimali tulizonazo, sisi hapa tumeishia kufuga wala posho. Tunataka katiba inayotupa sisi wananchi mamlaka ya kusimamia rasilimali zetu, na nguvu ya kuwajibisha wezi na wazembe hasa wabunge wanaozembea. Enough is enough.
 
Hivi kwa siasa za tanzania unaweza kutenganisha vipi shughuri au utendaji wa serikali, wabunge wa ccm(bunge). Kwasababu spika wa bunge ni ccm na tumeona spika huwa anasisima kabisa upande wa serikali kwenye miswada ya serikali, mawaziri wote ni wabunge wa ccm na ndiyo serikali yenyewe. Nionavyo chadema na watanzania tutapigwa changa la macho hakuna jipya si jk wala bunge
 
Piga ua, wabunge wa CCM hawana ubavu wa kususia mswada wowote uliowasilishwa na serikali na kutoka nje! sana sana serikali itafyata mkia na kuuondoa ili kujenga mwafaka wa chama chao kwanza!! Wakifanya hivyo watakuwa wanawapa umaarufu CHADEMA hasa Tundu Lissu ambaye walimjadili ktk kikao kilichopita badala ya kujadili mswaada wa Katiba, na sasa itakuwa ni dhahiri kuwa anawaparanganyisha kwa hoja
 
Pamoja na yote niliyoandika, kimoyomoyo natamani wabunge wa ccm wakatae marekebisho ya hii sheria ya katiba mpya. Kataeni na ikiwezekana tokeni nje! Lakini mkae mkijua tarehe 1/1/2016 kama malaika mlinzi atawasaidia basi hamtazidi 15 bungeni. mtazama na hii sheria!
 
Back
Top Bottom