Wabunge wa CCM chapeni kazi kwa bidii kukiheshimisha chama kwa Watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,301
9,727
Ndugu zangu Watanzania,

Napenda kutumia jukwaa hili kuwashauri wabunge wote wa ccm kuchapa kazi kwa bidii,uzalendo ,uadilifu na kujitolea kwa ajili ya Watanzania,wabunge wa CCM fanyeni kazi kwa kusikiliza sauti za watanzania zinataka Nini na zinatarajia Nini, wasilisheni bungeni na kutoa hoja zenye maslahi kwa Taifa letu na watanzania, msizungumze mambo yenu binafsi yasiyo na maslahi kwa Taifa letu.

Jioneni mmepewa heshima ya kipekee kabisa kuwepo katika jengo hilo la heshima kabisa kati ya mamillioni wenye sifa za kuwepo hapo, tambueni kuwa ukiwa mbunge au kiongozi haimaanishi kuwa unaakili kuliko wote waliokuchagua na wasiokuchagua, hivyo kuweni wasikivu kwa Watanzania, kuweni wanyenyekevu, Fanyeni utatiti wa kina kabla ya kuwasilisha au kuchangia hoja yoyote Ile ili kujuwa hoja husika itawanufaisha watanzania au kuwaumiza Watanzania.

Wateteeni watanzania na siyo kutetea maslahi yenu binafsi ,Haipendizi na haifai sheria inapitishwa bungeni halafu baada ya wiki inarudishwa Tena bungeni kufanyiwa marekebisho baada ya kelele nyingi za watanzania kutoka mitaani,Hii haileti picha nzuri na inajenga chuki kwa kuwa inakuwa inaonyesha kuwa mpo bungeni kwa maslahi yenu binafsi, Hamsomi kinachokuwa kimewasilishwa bungeni,Hamuwatetei watanzania mpaka wasimame kujitetea wenyewe na kutetewa na Rais wao,Hamjali maumivu ya watanzania, Hamguswi na chochote kisichogusa maslahi yenu na Wala ninyi siyo sauti za Watanzania na hampo bungeni kwa ajili ya Watanzania.

Kila mmoja wenu ajitahidi kuzungumza na wapiga kura wake na kujuwa kero zao na kuzitafutia suluhisho la haraka katika mamlaka husika na zile ngumu zipelekeni bungeni, jiwekeni karibu zaidi na wananchi ili mpate kujuwa na kusikia sauti zao, fanyeni mikutano na wapiga kura wenu bila kusubiri mpaka wakati wa ziara za viongozi wetu wa kitaifa wa chama na serikali katika majimbo yenu.

Tambueni ya kuwa chama chetu kitampa nafasi mtu kugombea na kupeperusha bendera zetu yule atakaye kuwa anakubalika na wanachama na wananchi wote kwa ujumla,yule atakaye kuwa amefanya kazi kubwa na yakutukuka katika jimbo lake,yule ambaye kwa kushirikiana na serikali yetu atakuwa amehakikisha ilani ya CCM imetekeleza vizuri na wananchi wamepata huduma Bora na nzuri,yule atakaye kuwa wakati wote amekuwa karibu na wananchi ,lazima mjuwe kuwa ni yule atakaye kipa chama kazi ndogo ya kumnadi jukwaani kutokana na kukubalika kwake ndiye atakaye pata ridhaa ya chama chetu.

Lazima mfahamu kuwa CCM ya Rais Samia haitambeba mtu ambaye anakuwa Ni mzigo na atakipa chama wakati mgumu wa kumnadi jukwaani ,haita mpa nafasi mtu Ambaye hakubaliki na wanachama na wananchi, ambaye Ni fisadi mla Rushwa hatapewa nafasi na CCM ya mama yetu mpendwa kipenzi Cha watanzania mama Samia suluhu Hassani.

Hakuna atakaye nunua ubunge maana chama hakita mpitisha kugombea, hivyo asiwepo wa kuwaza kutafuta fungu la pesa kuwanunua wajumbe maana atapoteza pesa zake na hatapewa nafasi ya kugombea ndani ya CCM, hivyo kazi zenu na kukubalika kwenu ndiyo iwe ngao na nguzo yenu na ndizo zitakazo wabebeni.

Mama yetu Rais Samia na Mwenyekiti wetu wa chama Hana utani katika Hilo ,Hana huruma kuutupa mzigo mzito utakaokipa shida chama kwenye kampeni,Fanyeni kazinili kazi zenu ziwasemee na kuwateteeni.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom