Wabunge na mtindo wa "taarifa" wakati mchangiaji akiongea ni mchezo au matumizi mabaya ya kanuni?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,147
7,721
Nafahamu kuwa kutoa taarifa ipo kwenye kanuni za Bunge letu lakini katika Bunge hili la 11 linalo endelea naona kamtindo ka kutoa taarifa wakati mzungumzaji akichangia hoja kameshamiri kiasi kwamba kamekuwa kama kero au kamchezo ka shule!

Imekuwa kero na usumbufu.

Swali. Je, Wabunge wetu wanao toa taarifa kwa mzungumzaji/mchangiaji inamaana au wanatumia vibaya kanuni, tunamuomba Spika na wasaidizi wake watoe muongozo kwa wabunge waache kuchezea kanuni.
 
Unaangalia hili bunge ambalo mchangiaji dakika 8 dakika10 maneno yake ni Samia,mama yetu,serikali ya awamu ya sita imefanya makubwa zinarudiwa karibia mara 40 na anachokichangia pia kwa hizo dakika 2 bado hakijui.....bunge la uchawa uchawa na wajinga wajinga tu.
Umesema kweli sana! Wabunge wapuuzi Sana hawa. Jiwe ndio alileta hawa wapuuzi akawajaza huko mjengoni!
 
Unaangalia hili bunge ambalo mchangiaji katika dakika 8 kati ya dakika 10 maneno yake ni Samia, mama yetu, serikali ya awamu ya sita imefanya makubwa zinarudiwa karibia mara 40 na anachokichangia pia kwa hizo dakika 2 bado hakijui.....bunge la uchawa uchawa na wajinga wajinga tu.


Kinachonichosha zaidi.... Mtu akikohoa, Makofiii,. Akiwa anajirambulisha, Makofiii, hata kama ni salam au chochote ambacho hakihusiani na hoja yake, Makofiii.



Aisee tuna bunge la kipumbavu sijawah ona !!.
 
Unaangalia hili bunge ambalo mchangiaji katika dakika 8 kati ya dakika 10 maneno yake ni Samia, mama yetu, serikali ya awamu ya sita imefanya makubwa zinarudiwa karibia mara 40 na anachokichangia pia kwa hizo dakika 2 bado hakijui.....bunge la uchawa uchawa na wajinga wajinga tu.
Ila watu wanajua kujikomba na kusujudu sijapata kuona.
 
Mnapeleka wapumbavu bungeni mwategemea nini?

Kuna wabunge 110 wa viti maalumu hawana msaada wowote ule
 
Back
Top Bottom