Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,957
- 20,511
Nakubaliana na wewe.Wananchi ni waelewa,
Ingawa viwango vya uelewa vinatofautiana,
Ndio sababu sisi tuliobahatika kupata uelewa kidogo, tunatumia uelewa huo kidogo Kutoa ELIMU ya uraia ambayo ni HAKI ya wananchi ambayo Watawala wasingependa wananchi waipate.
Lakini njia moja na pekee kabisa kuonyesha kuwa wapiga kura ni waelewa ni kufanya mabadiliko katika masanduku ya kura jambo ambalo litaweza hata kuwastua wanasiasa kwamba hawakuchaguliwa wao katika majimbo yao bali vyama vingine.
Kwa mfano jimbo la Kawe wakisema hatumtaki tena Mbunge fulani kwa sababu hakufanya hivi na hivi, ni lazima wapiga kura wafanye hivyo kwenye sanduku la kura.
Mwaka wa 2025 watakiwa kuwa ni mwaka wa mabadiliko katika kupiga kura ambayo hayakuwahi kutokea tangu nchi ipate uhuru.