Wabunge CCM wawafunga goli CHADEMA, Sendeka amzidi kete Mnyika

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
Wabunge wa CCM jana walifanikiwa kuzinduka na kuwazidi kete wa CHADEMA dakika ya mwisho. Hali hiyo ilitokea wakati wa kupitishwa kwa muswada wa sheria ya fedha haramu. Aliyeokoa jahazi ni kada mpambanaji wa ufisadi Sendeka. Kamanda Sendeka alifanikiwa kabla bunge kuahirishwa mpaka jumatatu kutaka muongozo wa Spika na kumweleza mwenyekiti wa Bunge Mh. Mabumba kuwa alikosea kuhoji 'kifungu kimepita pamoja na marekebisho yake?", hali ambayo iliwafanya wabunge wa CCM kujibu "NDIOOOO" kwa sauti kubwa na hivyo kujikuta wamepitisha marekebisho yaliyowasilishwa na kijana wa Ubungo John Mnyika ambayo yalitaka adhabu ya makosa ya fedha haramu pamoja na kifungo kuongezwa kuwa pia na adhabu ya mali au fedha zilizohusika kuchukuliwa kama sehemu ya adhabu.

Kiongozi wa bunge alisema kwamba yeye sio malaika hivyo anamuomba Mungu amsamehe kwa kuhoji hivyo hali iliyofanya wabunge wa CCM wakosee na kuitikia ndio pamoja na wenzao wa CHADEMA na hivyo kufanya kifungu hicho kupitishwa wakati bunge lilipokaa kama kamati. Kutokana na hali hiyo alisema kwamba maneno "pamoja na marekebisho yake' yafutwe kwenye hansard ili marekebisho ya Mnyika yasiingizwe katika sheria.

Awali baada ya kifungu hicho kupitishwa wabunge wa CHADEMA walianza kushangilia hali ambayo iliwagutua wabunge wa CCM kuwa walikosea kusema ndio. Kutokana na hali hiyo Mwanasheria Mkuu wa Zamani Mtaalamu Andrew Chenge alikwenda kwa mwanasheria mkuu wa sasa Jaji Werema, akiwa na mazungumzo naye mwanasheria wa sasa alitaka mwenyekiti ampe nafasi Sendeka ili aweze kuzungumza.

Hata hivyo mwenyekiti hakumpa nafasi hiyo awali, bunge likamaliza kukaa kama kamati muswada ukapitishwa mara ya pili, na mara ya tatu na hatua zake zote na hivyo Mabumba kutangaza kwamba ni muswada halali uliopitishwa na bunge pamoja na marekebisho yake.

Kauli hiyo ilifanya wabunge wa upinzani wakiongozwa na CHADEMA kumshangilia kwa sauti kubwa na mwenyekiti huyo akawatakia weekend njema wabunge. Kabla ya kutangaza kikao kimeahirishwa Sendeka na Werema wakata tena kuzungumza ndio kamanda alipofanikiwa kusawazisha bao katika dakika za mwisho.

Sendeka alisema kwamba bunge haliwezi kutunga sheria yenye adhabu kali inayopingana na penal code kama alivyosema mwanasheria mkuu wa serikali. Katika utetezi wake juu ya sheria kuongezewa adhabu kijana Mnyika alidai kuwa adhabu ya miaka mitatu kwa fedha haramu ni chache na penal code haiwezi kuwa kizuizi kwa kuwa haikuwa kizuizi wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipolazimisha kifungo cha watoa maoni au elimu ya katiba kuwa miaka saba jela. Hata hivyo Mwanasheria Mkuu alidai kwamba katiba ni suala la muhimu hivyo ni lazima kuweka kifungo kikali zaidi hivyo fedha haramu zizichanganywe na katiba. Kutokana na maelezo hayo, Werema akasema kifungu kipite bila marekebisho. Mwenyekiti akahoji wabunge huwa kifungu kipite pamoja na marekebisho nao bila kujua wakaitikia NDIO kabla ya Kamanda Sendeka kuokoa jahazi.

....ndiyohiyo
 
Hilo goli liko wapi humu kwenye maelezo yako? Ushabiki pembeni, weka akili mbele.
 
Upuui mtupu uliomo vichwani mwa wabunge wa CCM, kuitikia ndiyo hovyo hovyo kama viziwi vile.

Nchi hii inaharibika kutokana na upofu wa wabunge wa CCM kuendekeza ubinafsi kuliko maslahi ya taifa.
 
Nasemaga humu
kilasiku haya majamaa yanalalaga yakiamka tu
ni ndiooooo hata hayajuagi kwanini yanasema ndio!
Fools
 
mwenyewe umesikia rahaaaa......kwamba sheria imepitishwa kwa kuwekwa adhabu ya kipumbafu.

Akili ya kuku kuoga kwenye vumbi...
 
Yaani CCM ahwaoni ujinga wao? unahitikiaje "Ndioooo" bila kujua "Ndiyo" kwenye nini? Huyio Sendeka ni Mbunge wa CDM? Hakujua asemalo? WEREMA ni Mwana CCM?
 
mwenyewe umesikia rahaaaa......kwamba sheria imepitishwa kwa kuwekwa adhabu ya kipumbafu.

Akili ya kuku kuoga kwenye vumbi...

Mkuu mimi ni mtetezi wa haki za wanyama. Naomba nikueleze kuwa umewakosea kuku kwa kitendo chako cha kuwalinganisha na kilaza wa namna hii. Kuku ni mnyama mwenye akili na mwenye utashi wa kulinda jamii yake. Mnyama mwenye thread hii ni zuzu
 
Hali ya ushabiki na kufungana magoli imesababisha wabunge wa ccm wapoteze muda mwingi kujipanga jinsi gani watapinga na kuwashinda wapinzani kwa ndiyoooo! Bila kujali ni kitu gani kinajadililiwa.......watu wanapiga soga tu wanangoja waulizwe ili waitike ndiyooo! Heading yako nilidhan timu ya wabunge wa CCM ilikuwa ikicheza na wabunge wa CDM
 
Tuliofungwa goli ni watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao, lakini kama hao wanapatikana CDM tu, basi mwandishi atakuwa sahihi.
 
Nasemaga humu
kilasiku haya majamaa yanalalaga yakiamka tu
ni ndiooooo hata hayajuagi kwanini yanasema ndio!
Fools

Angekuwa wa maana angesema wabunge wa CCM jana wameonyesha umbumbumbu wao, wamekubali kupitisha muswada kwa kitu wasichokijua.
 
kulikuwa na mashindano pale mjengoni jana ???

Tunapaswa tujadili mabadiliko ya sheria hizi na manufaa yake kwa taifa letu siyo nani kasema nini kamzidi vipi yule haisadii jipange upya mkuu wangu ndiyo maana akina Lwakatare hawatupendi
 
Mkuu mimi ni mtetezi wa haki za wanyama. Naomba nikueleze kuwa umewakosea kuku kwa kitendo chako cha kuwalinganisha na kilaza wa namna hii. Kuku ni mnyama mwenye akili na mwenye utashi wa kulinda jamii yake. Mnyama mwenye thread hii ni zuzu

Hii imekaa vizuri kiasi.
 


Dalili zinaonyesha kuwa hao wabunge wa CCM hata wangeulizwa tena kwa kwa wazo tofauti na hilo, wangejibu "NDIOOO" kwa maana hilo ndo jibu pekee wanalolijua, wanafanya hivyo bila kujali maslahi ya taifa... Waliamua kubadilisha kwa kuwa waliona hizo adhabu zinawahusu kwa sababu hizo biashara za fedha haramu zinafanywa na wao wenyewe!!
 
Back
Top Bottom