Wabongo hatuna misaada kabisa wakati wa ajali na majanga

dracular

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
737
1,036
Habari za mchana ndugu zangu wana jf.. huku tukiendelea na maombolezo ya msiba mzito ulio likumba taifa napenda ku share na nyinyi kisa kimoja nilichokishuhudia live mimi mwenyewe..
Nisiwachoshe ngoja niende kwenye kisa moja kwa moja..
Ilikuwa ni mwaka 2016 enzi hizo nikiwa Dar kwa shughuli za kimasomo.. ilikuwa ni majira kama ya saa kumi jioni nikiwa katika harakati zangu mitaa ya keko pale barabara ya taifa karibu kabisa na chuo cha duce..
Nilimuona kijana mmoja aliekuwa mbele yangu mita kadhaa (akiwa anatembea kwa mguu) akijaribu kumsemesha mtu mmoja aliekuwa ndani ya gari.. Lakini inaonekana yule mtu aliekuwa na gari ilibidi asogeze gari pembeni ili apate kumsikiliza vizuri yule kijana...
Ghafla yule kijana alitoa wembe na kumkata usoni yule jamaa aliekuwa ndani ya gari.. Yule dogo akaanza kumshambulia jamaa kwa viwembe jamaa nae wenge likamka mjaa akafungua mlango wa gari akimbie...
Mi nikatoka mbio kwenda kumpa msaada jamaa.. ebana eeh.. kumbe wale madogo wapo zaidi ya kumi walikuwa wanamzia yule jamaa..
Yaani bro kutoka kwenye gari kakutana na jiwe mi nae ikabidi nifunge break kwanza..
Kumbuka hapo linafinyika hilo tukio kuna kituo cha bodaboda na wapo zaidi ya kumi wanaangalia tu..
Jamaa alikuwa bishoo katupia t-shirt white yaani imelowa damu chepe chepe.. jamaa akawa analia anaomba msaada watu wamsaidie lakini hakuna hata mmoja alie jishughulisha..
Mi nilijitahidi sana kumsaidia jamaa japo niliishia kupata jeraha mgongoni..
Jamaa alikatwa katwa na viwembe na kuchomwa bisibisi kwa takribani dk 15.. Alafu watu wanapita tu na magari yao jamaa analala barabarani ili magari yasimame apate msaada lakini magari yanasimama tu kwa muda then yanaendelea..
Nilikimbia kituo cha polisi keko magurumbasi nikaja na polisii ndo pona ya jamaa..
Tulimkuta jamaa hata kuongea hawezi sura imepigwa viwembe haitamaniki..
Polisi waliwawakamata madogo wawili na walipowabana sababu ya kufanya vile walidai jamaa huyo ni daktari na anamchukua mke wa mmoja kati yao..
Lakini baadae jamaa alisema yeye sio daktari bali ni mfanyakazi wa bandari na alionyesha kitambulisho chake cha kazi..
Kumbe tabia ya wale madogo huwa ni kusingizia ugoni ili wapate hela na jamaa hata hawamjui..
Nilikumbuka hii baada ya kuona ajali ya Moro watu wanachuka video wakati mwenzao anaungua mbele yao tena akilia kwa uchungu kuomba msaada...
 
Kuna methali zingine tuzifute maana huenda ndio chanzo eti ''kufa kufaana'' vinginevyo itafsiriwe vizuri
 
Kuna methali zingine tuzifute maana huenda ndio chanzo eti ''kufa kufaana'' vinginevyo itafsiriwe vizuri
Yaani ile clip mtu aungua alafu wengine wapo bize kurekodi inaniuma sana aisee.. yaani nlitamani hata simu niimwagie mchanga labda naweza uzima ule moto
 
Back
Top Bottom