Wabongo bana, Wanaenda Olympic na Suti,

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
311590_334156733336310_1687454565_n.jpg
 
Samahani kwa kuuliza wakuu! Huyu aliyepewa heshima ya kupeperusha bendera yetu ni nani? Harafu naona kama hatuna timu vile maana naona wote kama wanywaji wa pombe, vitambi mbele na wana umri ulioenda tofauti na inavyotakiwa katika mashindano. Sasa tusubiri wakati wa kurudi hayo mabegi yatakavyokuwa yamefuraaaaa!!.
 
Samahani kwa kuuliza wakuu! Huyu aliyepewa heshima ya kupeperusha bendera yetu ni nani? Harafu naona kama hatuna timu vile maana naona wote kama wanywaji wa pombe, vitambi mbele na wana umri ulioenda tofauti na inavyotakiwa katika mashindano. Sasa tusubiri wakati wa kurudi hayo mabegi yatakavyokuwa yamefuraaaaa!!.
Wana michezo wa 2 viongozi 12.
 
Naona vitambi tu hapo sijui hawa ndo wale wanaokwenda na vimada wao au wake za watu badala ya kuwapeleka wananmichezo
 
Ndo mpango mzima! hii ndo bongo bana! wapi al haji MINTANGA!!? I miss you!
Huyu mzee naye si alikuwa na maslahi binafsi! Hukumbuki ya Mauritias na bondia wake. Hizi zote ni impact za uongozi wa juu kupenda shortcuts. Viongozi wetu wangekuwa wanajua madhara wanayosababishia wananchi wangeachia ngazi mapema kabla ya mambo hayajaharibika na kufikia point of no return.
 
Wana michezo wa 2 viongozi 12.
Hapo ndo choka mbaya na viongozi wetu!! Wanalalamika vijana hawana kazi, Oooh vijana ni bomu la ajira, Ooooh tusipochukua hatua ni hatari! Sasa sijui wanadhani hizo ajira zitajileta? Its a bullshit slogan aka cheap politics. Wangechangisha hiyo mipesa kwa ajili ya kupeleka team Olimpics si ingeanza kutoa mwamko mapema? Sasa hivi nitashangaa mtu akisimama mbele za watu na kuanza kujinasibu Oooh nitatengeneza ajira kwa vijana wakati fursa nyingi zinapita bila kutoa uhamasishaji au hata kuonyesha nia basi ya kuwatembelea wanapokuwa kwenye makambi ya mazoezi potelea mbali wakienda kushindwa ndo kujifunza na kupata uzoefu.
 
Niliitazama parade yao jana usiku na huyo aliyeshika bendera anitwa Zakia Mrisho, mwanariadha. Lakini tazama hapa chini naona wengine wanabandika picha tofauti sijui walipita tena au ni uwanja mwingine.

488102_10150968069448173_1759852166_n.jpg
Hii ya chini kidogo imenituliza kama ni kweli ndo team yetu!!
 
Hakuna hamasa yoyote wala shauku ya maandalizi niliyoiona watu walikuwa wanatumia mabilioni mengi kwenye copa coca cola na mashindano ya kagame.footbal siyo asili yetu yamkini tungewekeza nguvu hizo kwenda mikoa ya arusha ,singida na mara kutafuta wanariadha chipukizi nathani bendera yetu ya taifa ingepandishwa na wimbo wetu ungepigwa.kenya kama mmiezi miwili kabla walikuwa wanaiandaa jamii kwa kuwqtngaza washiriki wao kupitia kbc ,sisi wapi bwana tulishajidanganya mchezo ni football tuu na vizazi vinavyozaliwa vinaamini hivyo.
 
Yaani Timu ya Tanzania inavalishwa suti za Mariedo!!!??? Kwa nini wasivalishwe angalau vazi la Kimasai ambalo huwa liko la kike na la kiume wauenzi utamaduni wetu??? Wangevaa kimasai wakaweka na sime na rungu kwa kwenda mbele, mbona timu ya Burundi waliaandamana wameshika fimbo. Wizara ya michezo hakuna ubunifu kabisa. Ebu cheki hapa chini timu ya Fiji kiongozi kavaa sketi ya makuti kuuenzi utamaduni wao, na timu ya Mexico mshiriki kavaa kavaa kofia la galoni tatu somberero kuuenzi utamaduni wao!! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!

Fiji Olympic Team.jpg


Mexico Olympic team.jpg
 
Niliitazama parade yao jana usiku na huyo aliyeshika bendera anitwa Zakia Mrisho, mwanariadha. Lakini tazama hapa chini naona wengine wanabandika picha tofauti sijui walipita tena au ni uwanja mwingine.

488102_10150968069448173_1759852166_n.jpg

Usikubali kuingizwa mjini kirahisi. Hii ni picha ya olympic ya mwaka 2004 huko Korea kusini au 2008 huko Beijing, angalia vizuri utaona washereshaji ni wasichana wa kichina au wakorea. Hatudanganyiki, wao wa mwaka huu wamevttishwa suti za mariedo kama walivyowasilishwa na mwana JF Mbuzi Mzee.
 
Tanzania first participated at the Olympic Games in Mexico 1964, and has sent athletes to compete in every Summer Olympic Games since then, except for the boycotted the 1976 Games. The nation has never participated in the Winter the Olympic Games. Tanzanian athletes have won a total of two medals, by Filbert Bay in Moscow Olympics in 1980 in 3000 metres steeplechase and by Suleiman Nyambui in Moscow Olympics in 1980 in 5000 metres men. Since then, they have never ever won any other medal, gold, silver or bronze!!!! Tanzania Oyeee!!!
 
Back
Top Bottom