Wabara wanaoishi Zanzibar kupewa vitambulisho vya wageni Zanzibar

Hapana; binafsi nataka wabara walioko Zanzibar wagome kupokea vitambulisho hivyo wala kuvitumia tuone Zanzibar watafanya nini

Sijui watafukuzwa kwenye nchi ya watu?

Hii ni dhana ya chako ni chakwangu lakini chakwangu ni changu
Kila Mzinzibari ni Mtz lakini si kila Mtz ni Mzanzibari

Huu muungano haupo bali kuna dhana ya muungano tu
 
Mbona hili halina shida; na hao Watanzania watakaoklubali kupewa vitambulisho vya uraia kama wageni Zanzibar watakuwa wapuuzi!!
Wewe ungekataa hicho kitambulisho? Mbona enzi zile za kwenda Zenji na Passport walibeba hizo Passport?
Inajulikana wazi Zanzibar wana Rais, Wana Bendera, wana Wimbo wao wa Taifa na sasa wanawataka wageni (watanganyika) mpewe vitambulisho sawa na wageni wengine!

Kwa sirikali hii ya JK, hayo yoote yatafanyika na kufanikiwa!
 
Hapana; binafsi nataka wabara walioko Zanzibar wagome kupokea vitambulisho hivyo wala kuvitumia tuone Zanzibar watafanya nini

Watachukuliwa hatua za kisheria kama wageni wengine wanaovunja sheria za Nchi. Naona hawa jamaa wanazidi kumchongea Pinda kwenye Bunge lijalo, tusubiri.

Kadiri usiku unavyokuwa mzito, asubuhi inazidi kuwa karibu.
 
Juzi nimewakuta Wazanzibari weusi wanaitana Muarabu, wakiwa serious kabisa kila mmoja alijifanya Mwarabu mara anyooshe pua mara abane pua anapoongea na mimi Mtanganyika pure wa makabila heavy wamesema ninaonekana ni maji ya kiarabu, basi kwa wabara weupe kama Lowassa, Kikwete au Mtume Slaa watakuwa Wadhungu:) Tanzania 1 Nchi 1 Serikali 1 niko tayari kumtoa mtu roho kwa hili litimie
 
Zanzibar ni nchi inayojiendesha na kufanya maamuzi yake yenyewe ndiyo maana inataka kujua wageni waliopo zanzibar wanaishi wapi na wanafanya kazi wapi/gani. Wabara ni watu kutoka nje ya nchi ya Zanzibar. Panya inafax tembo then panya inamuuliza tembo vp inauma eeh tembo inapepesa masikio tu haisikii.
 
Hapana; binafsi nataka wabara walioko Zanzibar wagome kupokea vitambulisho hivyo wala kuvitumia tuone Zanzibar watafanya nini

Mwanakijiji,

Hawa wazanzibar ni wabinafsi sana binafsi nilikuwa nawaunga mkono but kadri siku zinavyokwenda ndivyo navyowaona wabinafsi kupindukia. Hii ni moja ya dalili unapowaambia wabara wapewe vitambulisho na je wazanzibar nao wapewe vitambulisho bara vya ugeni??? Binafsi naunga mkono wabara wagomee hivyo vitambulisho tuone watafanya nini.
 
Ivi CDM wakichukua nchi muungano utakufa ? ISije ikawa ZNZ wanajiandaaa

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Zanzibar ni Nchi.

Na itaendelea kuwa nchi milele. Wacha ndugu zetu Watanganyika wapige kelele kwa mambo madogo madogo kama haya ya Vitambulisho. Mambo ya msingi hawayasemi, kwao sawa tu. Ha ha ha. Daini Tanganyika yenuuuu, acheni longolongo. Mkuu Boflo amemaliza maneno ha ha ha.
 
Hapana; binafsi nataka wabara walioko Zanzibar wagome kupokea vitambulisho hivyo wala kuvitumia tuone Zanzibar watafanya nini

" nyinyi tushakuzooeni kusema ndio kwenu, vitambulisho vitatoka kwa wote ambaye si MZANZIBARI atachukua na kuvitumia itakiwavyo, si mumeuwa Tanganyika nyie? tutakuchezesheni kindumbwendumbwe tutakavyo, tumevumilia muda mrefu sasa ni wakati wa vitendo, bila Zanzibar nyinyi hamuendi ng'o! he he he, mtalijua jiji mwaka huu!"
 
Mwanakijiji,

Hawa wazanzibar ni wabinafsi sana binafsi nilikuwa nawaunga mkono but kadri siku zinavyokwenda ndivyo navyowaona wabinafsi kupindukia. Hii ni moja ya dalili unapowaambia wabara wapewe vitambulisho na je wazanzibar nao wapewe vitambulisho bara vya ugeni??? Binafsi naunga mkono wabara wagomee hivyo vitambulisho tuone watafanya nini.

" kama kudai mamlaka yetu kamili yaliyoporwa ni ubinafsi, haya tuiteni mutakavyo. who cares?! al muradi yetu yanatuendea kama tulivyopanga. hao waZanzibari waliopo huko mnaweza kuwataka nao wachukue vitambulisho pale tu mtakapokuwa na Tanganyika yenu. nyinyi kazi kusema tu. rejesheni Tanganyika yenu kwanza ndio muwe na midomo ya kusema ala! otherwise ....ZANZIBAR ni yetu waZanzibari na hiyo Tanzania ni yetu sote. Kila mZanzibari ni mTanzania lakini si kila mTanzania ni mZanzibari... (samahanini waZenji wenzangu najua wengine mnachefukwa mkiitwa waTanzania, ila hadi sasa hiyo ndio reality!"
 
Sijui watafukuzwa kwenye nchi ya watu?

Hii ni dhana ya chako ni chakwangu lakini chakwangu ni changu
Kila Mzinzibari ni Mtz lakini si kila Mtz ni Mzanzibari

Huu muungano haupo bali kuna dhana ya muungano tu

" nakusahihisha kidogo sijui umekosea ama kwa makusudi .... ni kwamba "kila mZanzibari ni mTanzania ila si kila mTanania ni mZanzibari, hiyo ndio reality, japo kuna waZanzibari wengi tu hawautaki uTanzania na waTanzania wengi tu wanajiita waZanzibari ....solution pigania Tanganyika yako urudishe utaifa wako"
 
Very good.
 
Hakuna cha Muungano wa mkataba, wala cha Muungano wa serikali tatu. Nchi moja, Serikali moja, Tanzania moja. Kama sivyo, let Znz go!
 
Back
Top Bottom