Usiruhusu makosa ya kawaida kwakuwa hatima yake huwa ni haya tunayo jadili hapa.
Sasa hivi hapa namsikia msomaji wa habari toka 88.5 MHz anasema matanki ya mafuta katika kinu cha kuzalisha umeme nchini Palestina yameRIpuka
Wakati huohuo Mwananchi.co.tz kwenye habari yenye kichwa cha habari "Ajali yaua Baba na mwana .... Badala ya kuandika Toyota Coaster wameandika Coastal
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Ajali-ya-gari-yaua-baba--mwanaye/-/1597296/2402590/-/12bbh7bz/-/index.html
zaidi hapo ni ukanjanja tu....Fani ya Habari imevamiwa, sijui watangazaji wanaokotwa wapi, ladha ya taarifa za habari iliyokuwepo enzi hizo (namkumbuka mtangazaji mmoja wa RTD alikuwa anaitwa Christine Chakunegela) haipo tena.
Sasa hivi ni Radio stations chache na Magazeti machache tu ndivyo vyenye habari zenye mvuto, vinginevyo lugha mchosho habari mchosho
Yale yalee.Kiongozi aliandika hakusema.Au unakuta wanasema Dochwelle badala ya Deutchwelle
Jana nilikua nasikiliza taarifa ya habari ambayo ilikua inasomwa na mtangazaji fulani wa kituo cha radio cha pride fm Mtwara wakati anasoma habari fulani akakosea baadhi ya neno ila cha kushangaza huyo mtangazaji akaanza kucheka...kwa kwel nilishangazwa sana na kitendo hiki, yaan napata taabu kuamini kama huyu mtangazaji kwel ana jua taratibu za kazi yake.......
1. nilikuwa
2. anajua
3. Baadhi inatumika katika wingi .....ilipaswa kuwa baadhi ya maneno
4. Hicho
5. Tabu
Nahisi hakuna tofauti kubwa kati yao na wengi wetu humu.