Waamuzi wazidi kumbana Ferguson

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Waamuzi wazidi kumbana Ferguson

Mkuu wa chama cha waamuzi nchini Uingereza ametaka meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson afungiwe kutokana na madai yake kwamba mwamuzi Alan Wiley hakuwa imara inavyotakiwa.
Ferguson amekwishaomba msamaha kwa kauli yake baada ya mchezo baina ya timu yake na Sunderland ambapo timu hizo zilifungana mabao 2-2.
Lakini Alan Leighton, mkuu wa chama cha waamuzi, ameiambia BBC, msamaha wa Ferguson ni wa "kijuujuu tu".
Amesema Leighton, adhabu kali kama zinazotolewa na Uefa za kumfungia meneja wa timu ndio zinamfaa Ferguson kuliko tu kumzuia asikae na timu yake na kutoa maelekezo uwanjani.

Source:http://www.bbc.co.uk/swahili/football/story/2009/10/091015_adhabu_fergusson.shtml
 
kazidi sana kidomodomo huyu mzee.kwanza afungiwe maisha kufundisha soka aende akalee wajukuu
 
kazidi sana kidomodomo huyu mzee.kwanza afungiwe maisha kufundisha soka aende akalee wajukuu

Matatizo yenu hayawezi kumalizwa au kuisha kwa kufungiwa kwa SAF, siku zote Dua la kuku....................'
 
haya malumbano "saikolojikale" yatawapa wakti mgumu sana/yatawaathiri waamuzi pindi watakapokuwa wanachezesha mpira unaohusu mashetani wekundu na timu nyingine...........especially akiwa kwenye bench...........kweli Babu SAF inabidi afungiwe for the rest of the season...........
 
Back
Top Bottom