Vyoo vya Uwanja wa Taifa

Mwiyuzi

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
846
432
Habari za asubuhi wanajukwaa!

Jana nilienda Uwanja wa Taifa katika tamasha la Krismas. Sasa ikafika wakati nikataka kwenda haja jamani! Nikakutana na hali hii:

  1. Hakukuwa na maji kwenye vyoo
  2. Hakuna dust bin za kuwekea uchafu katika vyoo vya wanawake
  3. Kwa hiyo vyoo vilikuwa ni vichafu mno kiasi kwamba watu wengine wanakojoa chini tu
Kwa kweli hali ya vyoo uwanja wa Taifa ni mbaya mno!

Mi nilighairi kwa kweli ikabidi nivumilie tu mpaka wakati wa kutoka. Kuna watu waliokuwa hawawezi kujizuia wakijisaidia hivyo hivyo kwenye vyoo vichafu.

Ninaomba uongozi husika wa Uwanja wa Taifa washughulikie jambo hili mara moja kwani ni kero na linashusha hadhi ya huo uwanja!
 
Kwa sisi wazoefu wa shida tunaona kawaida ila vumilia ukombozi unawadia bado mwaka na miezi tu chichiemu out chadema in choo kama ulaya tu
 
Ndio nchi yetu ilipofikia, na hapo kila mechi au tukio likifanyika serikali inaweza kiasi fulani cha fedha kibindoni lakini hawawezi kitunza vyoo...
 
Tunaokwenda Taifa kuangalia mechi tunajua ,,,vyoo vichafu kupita maelezo ,,,sisi ndio wabongo bana

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ndio nchi yetu ilipofikia, na hapo kila mechi au tukio likifanyika serikali inaweza kiasi fulani cha fedha kibindoni lakini hawawezi kitunza vyoo...

Yaani! Imagine mikojo ilikuwa ikichuruzika kutoka vyooni hadi njiani (kwenye kibarabara) coz watu walikuwa wanaona kinyaa kuingia ndani ya vyoo! Ni kero sana!

Am sure kiasi cha kuweka maji ndani hakiwezi hata kuzidi robo ya faida wanayoikusanya kwa mechi moja kama ya Simba vs Yanga!
 
hivi serikali inachukuliaje suala hili mbona Simba S. Club walipovunja viti wakawapga fain kwa siku moja.?
 
Ukitaka kujua ustaarabu wa mtu ingia chooni kwake usimwangalie kujipamba kwake na tai yake.
 
Mitanzania hovyo sana mbonaa hata viti yanang'oa ni serikali gani hiyo itafatilia hata yenye akili yakajifanya mataahira, hatukuwa na uwanja mzuri leo tunao eti tunaharibu mpaka viti vya kukalia wenyewe ushabiki gani huo si mkavunje makochi na tv zenu majumbani mwenu ila kwa kuwa mnataka kila kitu serikali na akili zenu hazifanyi kazi zimeganda.
 
Ni jambo dogo saana ktk taifa kulisimamia lkn ni MUNGU pekee anayeweza kushusha malaika zake waje watukomboe, jiulize Mh MKAPA alivyotoa hotuba yake wakati wa kukabidhiwa rasmi uwanja huo.alisisitiza mzee yule kwa sauti yake kakamavu.tujivunie uwanja ule kwani umejengwa kwa ushirikiano kati ya TANZANIA NA CHINA kwa kuchangia nusu kwa nusu
hivyo inatupaswa tujivunie na tuulinde tukiuonea fahari.
lkn kwa wale wanaoenda uwanjani pale kila mara watakubaliana nami ufisadi ni mkubwa mno, na kuna kitu kubebana kwa kuweka vikampuni fake vya mfukoni vinavyosimamia usafi.mwanzo wake ilisemwa kabisa tenda itatangazwa ili uwanja ule usimamiwe na kampuni binafsi lkn mwanangu ulaji utatoweka weka mtoto wa mjomba mpaka watakapostuka haaaaatumekula vya kutosha. lkn jiulize hayo yote yanatokea ktk mkoa ambao viongozi wote wa nchi wanaishi.kuna usalama kweli,kwanini? tembo,vifaru,twiga,pundamili na wanyama wote madini na vitu vyote vya thamani visiporwe kama usimamiajai nchi uko hivi. ni mola pekeee ataweza kulifanya taifa hili lijitambue wenyewe tumejishindwa.
 
Achana na ule uchafu wa watu kutokuflash vyoo! Pale hakuna maji! So what do you expect when there is no water in the toilet?

Kama hamna maji ya nini kushusha mzigo? si ndio uchafu wenyewe?
 
Back
Top Bottom