Nimekuwa nikufuatilia kwa ukaribu sana sanaaa taarifa zetu za habari hapa nyumbani tz,Kenya na hata Uganda lakini nika note kitu kwamba kuna mapungufu makubwa sana katika uwasilishaji nikajua ni kawaida kwetu kusingizia bado tupo chini kiteknolojia, lakini nikafanya uchunguzi kwa ukaribu kujua tofauti ya vifaa wanavyotumia, lakini nikagundua kuwa vina ubora mmoja kama kutuzidi basi nivifaa vichache sana. Mwisho nikajua hatuna watumiaji wa zuri wa vifaa hivi! Je hata wanaoripoti nao wanahitaji teknolojia....??? Leo nimeangalia taarifa ya habari ya Citzen wakawa wanariport mazishi ya Waziri wa Kilimo bwana John Njiku, yaani ukiona smartnes ya reporter na mtiririko wa Habari unaelewa kila kitu na kuguswa na tukio kiukaribu sana....