Vyama vya wafanyakazi vimekosa tija kwa sababu ya kuongozwa na makada wa CCM

Unapolaumu kwamba vyama vya wafanyakazi vinaongozwa na makada ukumbuke kwamba unaowatuhumu hawakujiteua kuwa viongozi bali walishinda katika chaguzi huru ndani ya vyama husika.
Soma kwanza uelewe mada kabla ya kuchangia, ukichangia kwa mihemko huwezi kuelewa.
 
Asilimia kubwa ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi ni waajiriwa wa serikali, that means their stomach are still attached to the dam gonv.

Sasa kwa hali hiyo unatagemea nini watakifanya kudai stahiki za wafanyakazi?

"the highest risk should give maximum profit"
 
Vyama vya wafanyakazi hamna kitu ni nembo tu na makato yetu yanayokatwa kila mwezi bila msaada wowote kwa mtumishi anaepata tatizo awapo katika utumishi hamna lolote Hasa Tukta ni fedheha tupu Yani hoi.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana nashauri vyama hivi vifutwe badala ya kuendelea kuwakamua wafanyakazi fedha wakati haviwasaidii chochote.
 
Vyama vya wafanyakazi hamna kitu ni nembo tu na makato yetu yanayokatwa kila mwezi bila msaada wowote kwa mtumishi anaepata tatizo awapo katika utumishi hamna lolote Hasa Tukta ni fedheha tupu Yani hoi.

Post sent using JamiiForums mobile app
Vyama hivi vinakosa mwelekeo kwa sababu vimejaa ukada...badala ya kuwasaidia wafanyakazi dhidi ya unyanyasaji na ukandamizaji unaofanywa na serikali, wanasaidiana na serikali kuwakandamiza wafanyakazi.
 
Vyama vya wafanyakazi nchini tanzania ni vya kitutusa sana. Nenda Kenya uone jinsi vyama vyao vinavyopiga kazi ya kuwatetea wafanyakazi.
 
Ukweli ni kwamba vyama vya wafanyakazi vimegeuzwa mawakala wa serikali ya CCM kuwakandamiza wafanyakazi badala ya kuwakwamua na dhuluma dhidi ya serikali.

Mkuu kwa serikali hii tuliyo nayo sahau kwamba itatokea kiongozi wa chama cha wafanyakazi asiegemea ccm, narudia tena sahau! ndio maana binafsi sijawahi amini kwamba eti kuna chama cha wafanyakazi ambacho kinaweza tetea maslahi yangu.
 
Vyama vya wafanyakazi nchini tanzania ni vya kitutusa sana. Nenda Kenya uone jinsi vyama vyao vinavyopiga kazi ya kuwatetea wafanyakazi.
Mkuu hata Zambia vyama vya wafanyakazi viko very strong na kiongozi akileta fyoko fyoko anapigwa chini, Tz si ndio chama cha waalimu kiliipa hela serikali katika uchaguzi wa mwaka 2015! sasa hapo unategemea nini!!!!
 
Mkuu kwa serikali hii tuliyo nayo sahau kwamba itatokea kiongozi wa chama cha wafanyakazi asiegemea ccm, narudia tena sahau! ndio maana binafsi sijawahi amini kwamba eti kuna chama cha wafanyakazi ambacho kinaweza tetea maslahi yangu.
Lakini sasa inabidi wafanyakazi waangalie namna ya kujiondoa kwenye vyama hivi ili wasiendelee kukamuliwa michango wakati vyama havina tija kwao.
 
Mkuu hata Zambia vyama vya wafanyakazi viko very strong na kiongozi akileta fyoko fyoko anapigwa chini, Tz si ndio chama cha waalimu kiliipa hela serikali katika uchaguzi wa mwaka 2015! sasa hapo unategemea nini!!!!
Mkuu umenishtua sana. Ina maan CWT ndio waliifadhili CCM mwaka 2015? Mwafwaaaaaaaaaaaa!
 
Mpaka sasa hivi ni mwaka wa pili wa Magufuli kukaa madarakani lakini hakuna mshahara ulioongezwa au watumishi waliopanda vyeo. Inauma sana CCM kupenyeza mikada yake kila taasisi.
 
Nadhani ile sheria iliyowekwa kwa ajili ya TLS ifanye hivyo kwa TUCTA pia
Vyama vya wafanyakazi nchini havifungamani na chama chochote cha siasa.

Hata hivyo siyo dhambi kwa vyama hivyo kuwa na viongozi wanaoshabikia CCM na wengine wakawa washabiki wa Ukawa, ila cha msingi wanachotakiwa wao ni kusimamia haki za wafanyakazi bila kuyumbishwa na serikali iliyoko madarakani.
 
Tatizo Hivi vyama vya wafanyakazi vilianzishwa na serikali chini ya chama Tawala wakati ule wa Chama kimeshika Utamu. Kwa ujumla, u-JUWATA, JUWATA bado umo .................!!
 
ccm.jpg

Salaam wakuu,

Niende kwenye mada moja kwa moja. Siasa imepenya kila mahali. Hadi kwenye mimbari na madhabahu za makanisa siasa zimefika. Vyama vya wafanyakazi ni moja ya taasisi ambazo CCM, kwa ustadhi mkubwa sana, wamefanikiwa kupenyeza mapandikizi wao kwa maslahi yao binafsi na mapana.

Kiongozi wa TUCTA aliyemaliza muda wake, ndugu Nicolaus Mgaya, ni kada wa CCM kindakindaki. Huyu bwana katika Uchaguzi Mkuu uliopita alijitosa kugombea Ubunge katika jimbo moja la uchaguzi nchini lakini aligalagazwa vibaya na kada mwenzake katika kura za maoni. Mrithi wa Mgaya TUCTA, ndugu Tumaini Nyamhokya, ni kada maarufu wa CCM. Aidha, Katibu Mkuu wa TUCTA Dr Yahya Msigwa ni kada maarufu wa CCM na anashikilia nafasi kubwa ya uongozi ndani ya CCM mkoani Iringa.

Uwepo wa makada hawa katika nafasi za juu za vyama vya wafanyakazi haijatokea kwa bahati mbaya. Huu ni mkakati maalumu uliosukwa na CCM kupenyeza makada wake ndani ya vyama vya wafanyakazi kwa lengo la kupoza makali ya madai ya wafanyakazi, ambao mara nyingi hudai madai yao kwa mtindo wa migomo na maandamano. Kuthibitisha hili, kwa mwaka mmoja sasa tangu makada hawa waanze kuongoza TUCTA, hawajawahi kuonekana hadharani kuishinikiza serikali yao ya CCM kuwalipa wafanyakazi stahili zao mbalimbali, ikiwemo nyongeza za mishahara za kila mwaka, malimbikizo ya mishahara, na madai mengine mengi ambayo wafanyakazi wanaidai serikali.

Chama cha Walimu (CWT) kimefanikiwa kwa kiasi fulani kutetea maslahi ya walimu ijapokuwa bado kinapata upinzani mkubwa kutoka TUCTA, inayoongozwa na makada wa CCM. Ndio maana CWT kinaonekana kuwa na nguvu kuliko vyama vingine vya wafanyakazi.

Akitokea kiongozi wa chama cha wafanyakazi asiyekuwa na chembechembe za CCM, hupata misukosuko ya hapa na pale ili kumkwamisha na ikibidi hata “kumpoteza”. Sote tunafahamu kilichomkuta kiongozi machachari wa chama cha TRAWU, ndugu Silvester Rwegasira. Serikali siku zote imekuwa ikijitahidi kuwapachika makada wake ndani ya vyama vya wafanyakazi ili kutimiza azma yake ovu ya kukandamiza maslahi na haki za wafanyakazi hapa nchini.

Nini kifanyike?
  • Inashauriwa mwanachama yeyote yule anayetaka kugombea uongozi wa TUCTA na vyama vingine vya wafanyakazi achunguzwe kama ni kada au la. Na ikiwa itafahamika kwamba mwanachama huyo ni kada, basi hicho kiwe kigezo kikubwa cha kumnyima kura au hata kumuangusha kwenye kura za maoni ili asipenye uongozini na kusaidiana na serikali yake kukandamiza haki na maslahi ya wafanyakazi.

  • Wafanyakazi wasikubali kukatwa fedha za michango ya uanachama kwa kuwa fedha hizo zinaenda kuwanufaisha makada wa CCM ambao wamewekwa pale kwa maslahi mapana ya chama na serikali yao ghairi ya maslahi ya wafanyakazi.

  • Wafanyakazi waangalie uwezekano wa kuunda vyama vipya vya wafanyakazi na kuachana na vyama vilivyopo kwani vimeshindwa kutetea maslahi yao kwa muda mrefu sana.

  • Wafanyakazi waadilifu waliopo wafanye mapinduzi ya kuwaangusha viongozi waliopo na kisha kuwachuja kwa misingi ya ukada, ambapo wale makada dhahiri waondolewe moja kwa moja na makada nyemelezi watupiliwe mbali pia.
Nawasilisha.

Naomba kujua. TLS NA THRC nacho kinaongozwa na kada zipi? Bi simba kijo kamuachia anna henga .tunaomba ufafanuzi pia. Mlitaka waongoze wakina nani ili kuwa na uzuri? Ccm imeanza kuongoza nchi miaka ipi hadi ikose kada kila sekta?
 
Mkuu hii ni mada mpya. Hivi ulivyotaja hapa sio vyama vya wafanyakazi ijapokuwa nakubaliana nawe kuwa sio rahisi kuwatambua makada wote waliomo ndani ya vyama vya siasa. Lakini kuna baadhi ya vyama makada wake wanajulikana wazi, ama kwa matendo yao au kwa itikadi zao. Mfano mzuri ni TUCTA ambako viongiozi wake wa juu (rais na katibu mkuu) ni makada maarufu wa CCM. Ndio maana mara zote watu hawa husimama upande wa wakandamizaji (serikali) wafanyakazi wanapodai maslahi yao. Hii nchi sasa tumefika mahali pabaya sana.
Naomba kujua. TLS NA THRC nacho kinaongozwa na kada zipi? Bi simba kijo kamuachia anna henga .tunaomba ufafanuzi pia. Mlitaka waongoze wakina nani ili kuwa na uzuri? Ccm imeanza kuongoza nchi miaka ipi hadi ikose kada kila sekta?
 
Bi kijo simba kamuachia anna henga. Lissu kamuachia fatma. Hawa ni kada ipi? Ccm wameongoza nchii kuanzia miaka ipi? Watakosa sekta ipi kuwamo? Ili mambo yaende vyema ni makada wa chama kipi ndo wanatakiwa kuongoza? Hizi mimi kwa mtazamo wangu naona post hii ametoa mtu anaeishi kwa matumaini.na matumaini ukiyaishi hadi unakufa hutaona ukitumainicho😄😄😄tuwaunge mkono wanaotuongoza ili na wao siku ukibahatika wakuunge mkono tunaijenga tanzania 1
 
Sasa kama rais na katibu wa chama ni makada unadhani wanaweza kwenda kinyume na serikali ya chama chao katika kukandamiza wafanyakazi?

Mfano mzuri ni Dr Msigwa ambaye amekiri hadharani kuwa alishirikiana na serikali bega kwa bega ktk kutunga sheria mpya ya pensheni inayowapora wastaafu mafao yao yote.

Back
Top Bottom