Vodacom - Mawakala wa M-Pesa - A shame!

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
7,076
2,445
Kwa muda sasa nimekuwa mtumiaji wa huduma ya M-Pesa. Pamoja na matatizo ya mara kwa mara ya "network"! lakini bado imekuwa ikisaidia sana katika kutuma pesa...

Tatizo lililopo ni kuwa hawa "mawakala" ni "wababaishaji" wakubwa sana - kila mara ukienda pale wanakwambia kuwa "hawana credit"!

Kama wamiliki wa Vodacom wanaingia hapa JF ni wakati muafaka mkaaza ku-review uwakala wa M-Pesa!
 
nakubaliana na wewe, je unahisi ni nini haswa wanafanya??
 
baba enock,nimekua nikiongea na baadhi ya mawakala juu ya hili tatizo wemgi wanadai kuwa kuna wateja wamchezo wa chuma ulete,hivyo kujikuta wanapata hasara kwahiyo wakikujua au wakiwa na mashaka na wewe wanakujibu simpo sina credit.je wewe ni mmojawapo?
 
Kwa muda sasa nimekuwa mtumiaji wa huduma ya M-Pesa. Pamoja na matatizo ya mara kwa mara ya "network"! lakini bado imekuwa ikisaidia sana katika kutuma pesa...

Tatizo lililopo ni kuwa hawa "mawakala" ni "wababaishaji" wakubwa sana - kila mara ukienda pale wanakwambia kuwa "hawana credit"!

Kama wamiliki wa Vodacom wanaingia hapa JF ni wakati muafaka mkaaza ku-review uwakala wa M-Pesa!

Sio ubabaishaji mitaji inawakaba
 
nakubaliana na wewe, je unahisi ni nini haswa wanafanya??

Tatizo mawakala wengi wamevamia hii biashara bila kuwa na mtaji wa kutosha, matokeo yake ndo hayo ya kufulia kila muda. Hata mie huwa nakumbana na utata huo wa kuishiwa salio mara nyingi sana nikienda kwa mawakala.
 
Ishu ni kwamba mitaji ni ishu. Vilevile suala la usalama wa pesa zenyewe. Ni risk kuwa na pesa nyingi sana kutokana na issue ya security
 
Ishu ni kwamba mitaji ni ishu. Vilevile suala la usalama wa pesa zenyewe. Ni risk kuwa na pesa nyingi sana kutokana na issue ya security

Mkuu wewe umemaliza, wakala ukiwa na pesa nyingi watu hawakucheleweshi. Kuna jamaa yangu alichukuliwa 5M magomeni saa 06:30 jioni na watu wanashuhudia.

Ni kweli wababaishaji wapo , lakini usalama pia ni suala lingine. Mtu anakwambia nataka kutoa 1M unamwambia toa, katika mchakato anagairi na anaondoka baada ya mda kidogo wazee wa kazi wanafika.
 
Back
Top Bottom