VodaCom Cheka Intaneti wananiibia?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Jana baada ya kufika nyumbani kwangu nikataka ku-download email zangu.Connection ilikuwa nzuri kabisa.
Hivyo nikafuata utratibu wa Vodacom kutuma ujumbe CHEKA INTANET kwenda 123.

Baada ya muda mfupi nikapata ujumbe "You have 15.00 MB available which expires on 25/07/2010"
Baada ya ujumbe huo connection haikupatikana kabisa hata nilipojaribu saa sita usiku,na Tshs 500 yangu ikawa imekwenda.

Baadaye nikagundua kuwa nimeshapigwa pick pocket na Vodacom.

Leo nimeuliza wengine wakabaki kunicheka, "we huijui voda bwana?"
 
Kwenye tangazo la VodaCom wamesema ni MB 15 tu. Sasa sioni unacholalamikia ni nini.

Madhumuni ya Cheka Internet ni kwa watumiaji wa simu za mkononi
 
Kwenye tangazo la VodaCom wamesema ni MB 15 tu. Sasa sioni unacholalamikia ni nini.

Madhumuni ya Cheka Internet ni kwa watumiaji wa simu za mkononi
Mkuu MP, sikudownload hata 0.5MB!

Natumia simu ya kisasa kidogo,Samsung GALAXY(spica) GT-I5700, bila hiyo dezo ya Voda na-download info kibao.

Hii ni tahadhari tu kwa watumiaji hizi services, jamaa wanainvest katika matangazo wakijua wengi wata tuma pesa(Tshs 500) bila kujua wanaliwa hela yao.

Kama watajaribu watu 10,000 bila mafanikio piga hesabu ya fedha inayoliwa kwa siku, momentarily.
 
Mkuu ndiyo maana lazima uwasikie wakisema- "Vigezo na Masharti kuzingatiwa" but these vigezo na masharti are never disclosed to you - hapo tia akili mukichwa, ni kununua mbuzi kwenye gunia.
 
Hata mimi nina hiyo Galaxy Spica na ninatumia Voda bila matatizo, natumia ile ya 30,000/= kwa mwezi lakini.

Umeweka APN ya Voda kwenye Settings? Bila hivo haiwezi kuconnect kwenye mtandao. APN ya voda ni "internet".

Ingia Settings>Wireless & Networks > Mobile Networks > Access Point Names > Click menu button then "New APN">
Name: weka chochote
APN: internet

>Bonyeza menu button > Save.
 
NO NO NO NO......Kwa hilo usiwalaumu Vodacom wako sahihi kabisa ni MB 15 tu na zinaisha saa 6 usiku hapo hakuna wizi labda ni matatizo ya konection yako au Computer ilianza kuji update pale tu ulipo connect moderm yako.
 
Nawashukuru wakuu, nitajaribu tena.
Hata hivyo connection ya kawaida haina matatizo , ni hii ya dezo(Tshs 500 kwa 15MB)
Nikifanikiwa nitaarifu
 
Wakuu hiyo issue ya Lole ni kweli ipo nami imenitokea mara mbili wiki iliyopita. Tatizo linakuja pale unapojisajili kuomba hiyo huduma connection inakata. Usipojisajili unapata connection vizuri. Naona mchango wa Kang ni mzuri nitajaribu nami kuufuatilia.
 
Wakuu ile cable iliyokuwa inatangazwa sana kuwa imefika Dar bado haijaanza kazi, kwani watu tunaendelea kuibiwa au kutozwa pesa nyingi kama hiyo cable imefika hapa TAnzania?
 
Ahsante mkuu Fisherscom, nikifikiri ni mimi tu.
Jamani hakuna mwana JF huko Voda atueleze mchezo unaofanyika?
Inaelekea kwa kujiunga na huduma hiyo ya Cheka Intaneti, mtandao wa mteja aliyejiunga inaelekezwa kwenye congested traffic hivyo kutopata mawasiliano, kwa kifupi hela hiyo ni kama unaitupa tu
 
Wakuu ile cable iliyokuwa inatangazwa sana kuwa imefika Dar bado haijaanza kazi, kwani watu tunaendelea kuibiwa au kutozwa pesa nyingi kama hiyo cable imefika hapa TAnzania?

Bei zimepungua, kabla ya cable kufika Voda Bomba30 ilikuwa 60,000/= now ni 30,000/= mabadiliko yapo, na cable nyingine itakapotua nadhani mambo yatakuwa mazuri zaidi.
 
Back
Top Bottom