Viwavi jeshi kwenye jamii forum

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,358
4,304
Kuna jamaa yangu amenieleza kuwa aliandika mchango wake hivi karibuni katika jukwaa moja.

Anasema alifanikiwa kuuona machango wake kwenye thread na kuusoma mara kadhaa.

Anasema ilikuwa usiku mkubwa alipotuma mchango wake. Alikwenda kulala na alipoamka akakuta viwavi jeshi wameshalimaliza shamba lote. Hakuona mchango wake wala thread aliyochangia.

Basi jamaa alimalizia kusema "duu! Hata jamii forum wapo mods magamba?
Au nzige na viwavi jeshi wamevamia JF?

Alinifurahisha sana! Nilimwambia hilo ni jambo la kawaida tu hapa JF ni vyema aweke kumbukumbu ya michango yako ili viwavi wakifanikiwa kula michango yake, awabandikie tena.

Jamaa yangu akasema, "yes..sasa umenipa maujanja..watanikoma!"
 
Back
Top Bottom